Real Bamako Kuna wachezaji wazuri kuliko Tulionao Simba, Uongozi ulifanyie kazi

Real Bamako Kuna wachezaji wazuri kuliko Tulionao Simba, Uongozi ulifanyie kazi

mlambaji asali

Senior Member
Joined
Jan 30, 2023
Posts
150
Reaction score
505
Natoa wito Kwa uongozi wa klabu yangu ya Simba kupitia scouting ya timu uwamulike hawa wachezaji wa As Real Bamako. Humu tunapata wachezaji wengi wazuri kwa bei nafuu sana

Nimeona wachezaji wenye uwezo zaidi ya hawa kina baleke, kyombo, sakho, boko, Banda Saido na mauchafu mengine mengi tuliyoyajaza klabuni kwetu.

Ushauri wangu uzingatiwe

Simba nguvu moja
 
Nimeona wachezaji wenye uwezo zaidi ya hawa kina baleke, kyombo, sakho, boko, Banda Saido na mauchafu mengine mengi tuliyoyajaza klabuni kwetu.
Basi muwe mnaotoa ushauri unaoendana na uhalisia. Sasa wachezaji wote wa Bamako wakija Simba watakuja kama wachezaji wa kigeni.

Lakini cha ajabu unawataja Kyombo na Bocco ambao ni wazawa. Nafasi za wageni zitatoka wapi iwapo utaondoa wazawa?

Hivi unadhani ukiangalia hapa nchini, kuna strikers gani wanaowazidi Bocco na Kyombo? Nafasi ya mzawa inachukuliwa na mzawa, mgeni na mgeni. Pitia upya uzi wako
 
Mkuu hili ndio tatizo letu la msingi, mido unatakiwa kila muda uutamani mpira, yaani unaufata upewe Sasa sisi watu wanaogopa mpira [emoji848][emoji848]
Wakitoa pasi, alaf wanajificha wasipasiwe tena 😅😅😅
 
😅😅😅 Acha kuwasagia kunguni Mzee 😅😅
Huo ndio ukweli mzee,duniani midfielder muda wote anautaka mpira,sasa zetu zinaukimbia,inonga ana mali mguuni,kanoute anageuzq mgongo, mwishowe mpira unaenda kwa kapombe,unarudi kwa inonga unabutuliwa.
 
😅😅😅 Ila Mzamiru yupo humu, akiona hatojisikia fresh.

Sema huwa nakereka mtu akitoa pasi, badala ya kufungua ili apewe tena, anajifichaa 😅😅
 
Back
Top Bottom