The Evil Genius
JF-Expert Member
- Mar 21, 2014
- 6,017
- 19,506
Biashara ya kujenga na kupangisha Tanzania inaelekea kufa kabisa. Sasa hivi hii biashara inapumulia mashine ICU.
Kwa wakazi wa Dar es Salaam mtakuwa mashahidi, malls nyingi na majengo mengi ni matupu miaka sasa, Mkuki house sasa inaanza kujaa panya, Quality Centre and Plaza mnajua kinachoendelea pale.
Ukija jengo refu kuliko yote barabara ya Sam mujoma hapa karibu na Chuo /Mlima city iko wazi miaka sasa, hakuna wapangaji.
Ukienda zile flat za NHC zilizoko Morocco ziko tupu, China plaza Kariakoo inaelekea kuwa tupu, discount center wakitoka mle inakua gofu.
Ukienda mjini, Posta majengo mengi wameandika space to let, Rent here, space available.
Naona jengo jipya la Palm Village Millard Ayo amepewa kazi ya kupiga debe masaa 24, sina hakika kama wataweza kuhimili.
Je, hii inatokana na nini ama inaashiria nini kwenye uchumi huu wa kati?