Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Hapo katikati real estate ilikuwa imekuzwa thamani kuliko kawaida. Taasisi za serikali ziliwekeza pesa nyingi kwenye hii miradi bila kuangalia uhitaji au uchumi wa nchi. Zilikuwa zinashindana kujenga maghorofa.

Wakati wa kupangisha umefika wanakuta uchumi haukubali bei zao za kwenye makaratasi.
 
Hapo katikati real estate ilikuwa imekuzwa thamani kuliko kawaida. Taasisi za serikali ziliwekeza pesa nyingi kwenye hii miradi bila kuangalia uhitaji au uchumi wa nchi. Zilikuwa zinashindana kujenga maghorofa.

Wakati wa kupangisha umefika wanakuta uchumi haukubali bei zai za kwenye makaratasi.
Mnazunguka zunguka, ishu ni kwamba private sector imekufa na purchasing power ya watu haipo

Kujizungusha zungusha kote huko kwa nini? Jiwe kaua biashara na wala sio Dar pekee kila sehemu ya nchi

Yaani saizi ukiuza shamba utapata mnunuzi kwa bei yenye nafuu kuliko kuuza kiwanja au nyumba
 
Kuna siku niliwapigia simu wale jamaa wa Victoria Apartments kuhusu Ghorofa Lao [emoji3][emoji3][emoji2] Duuh eti single bedroom inagharimu 250 Millions [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Kwa sehemu ile na aina ya nyumba bei siyo kubwa. Sema wabongo wengi tumezoea ''nyumba'' za milioni ishirini. Nikuhakikishie kuwa nyumba nyingi tunazoishi hazina hadhi ya kuitwa nyumba. Nyingi ni muunganisho wa matofali na sementi na bati juu. Hakuna utaalam wowote kwenye kujenga.
 
Hio China Plaza si iko Kariakoo? Mbona kuna thread ililetwa humu Kariakoo watu wako tayari kutoa 30m(nje ya Kodi) kupata fremu?!!
Sio sasa hivi ilikua kipindi cha nyuma na mitaa mingi unaingia kwa kulipa kodi tuu na frem zipo nyingi sana Kkoo na biashara imeyumba kutokana na covid kwa hiyo mambo yamekuwa magumu pande nyingi mno...
 
Unajua mimi huwa nasema Magufuli japo hajafanya vizuri lakini kuna lawama nyingine anatupiwa bure. Hebu angalia vitu kama frem za maduka. Ilifikia kipindi kila anayejenga ni lazima aweke frem za maduka.

Kariakoo nyumba zote zikageuzwa frem. Kimsingi mitaa yote ya Dar nyumba za mbele zimepambwa na frem za maduka. Kwa hali hii hata uchumi uwe mzuri kiasi gani lakini nyingi ni lazima zitakosa wapangaji.
 
Sio sasa hivi ilikua kipindi cha nyuma na mitaa mingi unaingia kwa kulipa kodi tuu na frem zipo nyingi sana kkoo na biashara imeyumba kutokana na covid kwa hiyo mambo yamekua magumu pande nyingi mno...
Okay
 
Sio sasa hivi ilikua kipindi cha nyuma na mitaa mingi unaingia kwa kulipa kodi tuu na frem zipo nyingi sana kkoo na biashara imeyumba kutokana na covid kwa hiyo mambo yamekua magumu pande nyingi mno...
Kariakoo ya sasa mbona wenye frem watakugombea kama mpira wa kona? Ile jeuri yote imeisha. Kwanza zilijengwa nyingi kupita mahitaji. Zimebaki sehemu chache zenye movement nzuri ya wateja ndiyo labda kidogo frem inaweza kuwa shida.

Kuna sehemu kama pale Mwenge stendi miaka ya 2010 mpaka 2015 mtu ulikuwa hugusi frem na wenye nyumba walikuwa na jeuri ya ajabu. Mwenye nyumba akikohoa kidogo kama umepangisha kwake unakimbilia kumuuliza kama unaweza kumpa msaada. Kwanza kupata frem ilikuwa ni kama kushinda bahati nasibu ya mamilioni. Nenda siku hizi uone... frem hazina watu
 
Unajua mimi huwa nasema Magufuli japo hajafanya vizuri lakini kuna lawama nyingine anatupiwa bure. Hebu angalia vitu kama frem za maduka. Ilifikia kipindi kila anayejenga ni lazima aweke frem za maduka. Kariakoo nyumba zote zikageuzwa frem. Kimsingi mitaa yote ya Dar nyumba za mbele zimepambwa na frem za maduka. Kwa hali hii hata uchumi uwe mzuri kiasi gani lakini nyingi ni lazima zitakosa wapangaji.
Hii sasa ndio kuangalia tatizo nje ya siasa.
 
Ukiongoza nchi kwa hofu na vitisho ukajaza usalama wa Taifa kila kona pasipo lenga unataka nini basi juwa mwisho mambo kama haya lazima yatatokea. Hicho kinaitwa task force kitawapa majibu wanayo yataka baada ya kumaliza kuziuwa bihashar zote na sote kuw wachuuzi barabarani.
 
Cha kustaajabisha ni pale jengo linakaa bure mmiliki hataki kushusha kodi na anaona ni bora likae tupu hata miaka kumi ilipaswa kwa wakati huu sisi wanyonge tukalie haya maghorofa
Tatizo linakuja pale unapopangisha jengo kwa kodi ndogo kiasi ambacho mpangaji akiondoka pesa uliyopata haitoshi hata kufanya ukarabati.

Wako wapangaji wastaarabu, wanatunza jengo; Ila wako pia ambao siyo wastaarabu na wanaharibu sana jengo. Kutofautisha ndiyo tatizo.
 
Back
Top Bottom