Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Kuna siku niliwapigia simu wale jamaa wa Victoria Apartments kuhusu Ghorofa Lao [emoji3][emoji3][emoji2] Duuh eti single bedroom inagharimu 250 Millions [emoji1787][emoji1787][emoji1787]
Hii ni bei ya kununulia
 
Sasa kama kipindi hicho fremu, hasa katikati ya jiji na maeneo yaliyochangamka, zina very high demand kwa nini watu wasiongeze supply kwa kujenga mafremu mengi? Biashara ilikuwa kubwa na wanunuzi wengi mpaka kutoka nchi jirani. Cha kujiuliza ni why biashara zinakufa...
 
Hio China Plaza si iko Kariakoo? Mbona kuna thread ililetwa humu Kariakoo watu wako tayari kutoa 30m(nje ya Kodi) kupata fremu?!!
China plaza iko pembeni kule karibu na karume na ..imekaa kwa aina flan ya biashara tuu ..sogea k.koo katkati uone balaa lake ...usikariri
 
Wanaona heri yabakie bure kuliko kuokota chochote kile - nilazima kwa sasa watu wakajifunza kuhusu nguvu ya soko yaani soko linataka pakodishwe kwa kiasi gani?na kiasi hicho ndicho kile kilichokubalika hii mambo ya kupimiana kwa [[ square foot]] kwa sasa haiwezekani tena
 
Mh Mbezi beach hio ni kodi ya nyumba ya kawaida sana. Nina mtu wangu kahangaika sana kupata angalau two bedroom kwa 350,000/- kakosa kaishia Mbezi upande wa juu.

Nenda kwa mwenye nyumba. Achana na madalali. Madalali hawataki kuonyesha bei za nyumba zimeshuka. Nimpo Mbezi Jogoo. Fully furnished two bedroom complex.
 
Yani hata nyumba za kupangisha Dar hali tete kbs, wapangaji hakuna , Kodi zimeshuka na bado tunatakiwa tulipe Kodi ya majengo. Wapangaji wenyewe wanalipa miezi 3 au kila mwezi , sijui itakuwaje.
 
Wenye nyumba wana tabia ya kupangisha nyumba bei ghali.


Achilia mbali hayo maghorofa, hata frame za kawaida zina bei ambayo haina uhalisia.

Chukulia mfano hapa Dodoma Frame ndogo tu ya duka Tsh 600k mwezi. Ukija nje ya mji kwenye maeneo yaliyochagamka kidogo unakuta kodi 300k kwa mwezi. Ukitathimini biashara yako unaona haiwezi kulipa.

Ndio maana miaka ya hivi karibuni mabanda ya kutengeneza yamekuwa mengi sana mijini.
 
Chakustaajabisha ni pale jengo linakaa bure mmiliki hataki kushusha kodi na anaona ni bora likae tupu hata miaka kumi ilipaswa kwa wakati huu sisi wanyonge tukalie haya maghorofa
Mpate kumtia hasara zaidi za matengenezo, maana kodi mnayolipa haitoshi, gharama za matengenezo ziko pale pale. Bahati mbaya wanyonge hawana busara ya utunzaji, ni uharibifu tu.
 
Shughuli za kiserikali zimehamia Dodoma. Sasa hivi Dodoma pamekucha
Dodoma hapajakucha kiivo , tungeona malls dodoma kuonyesha kuwa zimekuwa replaced na hizi za dar.
Au unataka kuniambia watu wanafunga malls na kwenta kufungua maduka ya kuchuuza dodoma ? Mana ndo yaliyojaaa huko.
 
Chakustaajabisha ni pale jengo linakaa bure mmiliki hataki kushusha kodi na anaona ni bora likae tupu hata miaka kumi ilipaswa kwa wakati huu sisi wanyonge tukalie haya maghorofa
Mkuu hii biashara imeanguka ghafla bin vuu, kuna watu walitia pesa nyingi wakidhani mambo yatakuwa kama yalivyokuwa , walipomaliza majengo ndo wanakutana na huu mdororo, naukute ilikuwa ni pesa ya benki ndo balaa
 
Sio kwamba hawawezi kushusha kodi, wenye hizo nyumba wametumia hati kupata mikopo mikubwa bank na kuanzisha biashara nyingine zinazowaingizia vipato kuliko hizo nyumba za kupanga
Hivo kuliko ashushe bei ya pango ni bora aiache ikae gofu hivo hivo kwa maana yeye ana uhakika wa rejesho na biashara zake zingine zinaenda.

Lakini hua hakumbuki maintenance cost ya hiyo nyumba isiokaa na mpangaji mwaka mzima.
 
Back
Top Bottom