Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

Real estate business Tanzania inaelekea kufa kabisa, kwa sasa inapumulia mashine

TZ bei za nyumba ni kubwa sana,ukiangalia Fine Living - House Hunters utaona nyumba hadi za milioni 400 USA nzuri zipo hadi ufukweni.
Unaipata kwenye king'amuzi gani hiyo channel?, Azam tv kama wameiondoa hivi.
 
Biashara ya kujenga na kupangisha Tanzania inaelekea kufa kabisa. Sasa hivi hii biashara inapumulia mashine ICU.

Kwa wakazi wa Dsr es Salaam mtakuwa mashahidi, malls nyingi na majengo mengi ni matupu miaka sasa, Mkuki house sasa inaanza kujaa panya, Quality Centre and Plaza mnajua kinachoendelea pale.

Ukija jengo refu kuliko yote barabara ya Sam mujoma hapa karibu na Chuo /Mlima city iko wazi miaka sasa, hakuna wapangaji.

Ukienda zile flat za NHC zilizoko Morocco ziko tupu, China plaza Kariakoo inaelekea kuwa tupu, discount center wakitoka mle inakua gofu.

Ukienda mjini, Posta majengo mengi wameandika space to let, Rent here, space available.

Naona jengo jipya la Palm Village Millard Ayo amepewa kazi ya kupiga debe masaa 24, sina hakika kama wataweza kuhimili.

Je hii inatokana na nini ama inaashiria nini kwenye uchumi huu wa kati?
Hii sio ishu ya corona ,1.vyuma kukaza 2.serikali kuhamia dodoma.
Hii hali hata dodoma ipo ,ukuaji wa sekta sio kiivo dodoma,serikali inatumia nguvu nyingi kujenga mji.

Ila ni mpito , mazani after 7 years to come real estate itakuwa vizuri maradufu.

Kwa sasa kama unahela nunua viwanja ,nyumba ,nk ......property maeneo mengi zimekuwa undervalued ,baadae unaweza uza mara 3-10 ya bei ya sasa

mf viwanja ,bei elekezi /average kutokana na wizara ya ardhi minimum na maximum, unakuta bei imepungua below minumum price
 
Lakini mbona mdororo juu ya mdororo na hakuna hope
yawezekana pia mimi na ww hatuioni hyo hope kulingana na mawazo yetu ila wao wanaiona kulingana na mawazo yao, tujichunguze na tuwachunguze katika mtizamo tofauti! huenda tukapata majibu fikirishi na ridhishi
 
Unajua mimi huwa nasema Magufuli japo hajafanya vizuri lakini kuna lawama nyingine anatupiwa bure. Hebu angalia vitu kama frem za maduka. Ilifikia kipindi kila anayejenga ni lazima aweke frem za maduka.

Kariakoo nyumba zote zikageuzwa frem. Kimsingi mitaa yote ya Dar nyumba za mbele zimepambwa na frem za maduka. Kwa hali hii hata uchumi uwe mzuri kiasi gani lakini nyingi ni lazima zitakosa wapangaji.
Kariakoo kipindi chote hata uongeze frem 100 zinajaa. Mfan pale kariakoo sokomi nnje ya jengo kulikuwa na space wazo pembeni ,wakaamua design viduka vidogo,vilijaa in advance....................

Ukuaji wa uchumi wa kati bado hauja reflect kwa mtu mmoja mmoja, umeanza kwa wachache ambao ndio wameshika uchumi.

Alienacho ataongezewa kwa sasa asienacho ,Hata kile kidogo ulichonacho utanyamgany'wa.

Ni kupambana kulata hata kile kidogo

Sahizo atleast watumishi mambo yanaenda bila wasi, kwenye biashara asilimia kubwa kujikongoja..

Maoni tu
 
Sasa hivi watu wana store zao majumbani kisha wapo mitandaoni kutangaza biashara
Hizo biashara ndogo ,ambazo hata frem posta kulipa rent ni ngumu......hapa tunazungumzia real estate maeneo ya biashara zaidi mjini ,huwezi niambia una store furniture ndani kwako na cement unauzia mtandaoni......majumbani mtaani huku adhari sio kubwa sana ,athari property za biashara ambazo zimejwngwa kwa mkopo au kwa mtaji mkubwa .mfano uwanja tu Sqm.500 umenunua mil 500 umeweka ghorofa yako barabarani for lease,na uswahilini nyumba za kupanga hakuna shida sana.....
 
Tatizo biashara nyingi ni kuigana tu, copy and paste. Hakuna tafiti za kina za biashara kwenye soko na uendeshaji. Biashara za mdomoni tu...ukisikia fulani ana duka faida kwa siku laki 2 bhas na wewe haraka haraka unafungua duka kama hilo with same products, same location wateja ndio wale wale unategemea nini?

Angalau kuwe na kuongeza ka ubunifu kidogo, market segmentation kuendana na location ya duka na aina ya wateja katika eneo hilo. Pia source ya bidhaa izingatiwe.

Ukikosa hivi ndio unatumbukia kwenye uswahili...nadhani nimeeleweka..hapi ndio kwenye fitina na uzandiki mweusi mweusi na kuharibiana biashara. Shida ni kukurupuka kuingia kwenye biashara bila kufanya tafiti ya kutosha. Kuanzisha biashara sio swala la kuwa na mtaji tu..yahitaji taarifa nyingi za ziada.

Wengi wanakimbia kwa sababu hiyo, biashara zimekufa nyingine zinayumba..yote tatizo ni hilo. Na pia kikubwa kodi sasa hivi zinalipwa. Mwanzoni wasafirisha parcel kutoka China huko walikuwa wanateleza tu. Ile kampuni ya mapazia na kapeti iliinua wengi sana.
 
Kwa sehemu ile na aina ya nyumba bei siyo kubwa. Sema wabongo wengi tumezoea ''nyumba'' za milioni ishirini. Nikuhakikishie kuwa nyumba nyingi tunazoishi hazina hadhi ya kuitwa nyumba. Nyingi ni muunganisho wa matofali na sementi na bati juu. Hakuna utaalam wowote kwenye kujenga.
Tunajua nyumba tunazoishi mkuu na ndio maana hua tunasema nimejenga ka 'kibanda' kule pale bunju.
 
Assets economy inapoanguka huwa ni jambo baya sana maana assets ndizo mitaji na ndizo zinazolinda uchumi wa nchi hata na mtu mmoja mmoja zisisumbuliwe sana ili zibakie kama dirisha la kupumulia
Hayo mnayajua wachumi,bwn yule cha msingi ye anaona miradi yake ya ujenzi inaendelea anaona fresh tu labda ile mpk ikwame ndio atakaa chini asikilize mtu.
 
Biashara ya kujenga na kupangisha Tanzania inaelekea kufa kabisa. Sasa hivi hii biashara inapumulia mashine ICU.

Kwa wakazi wa Dsr es Salaam mtakuwa mashahidi, malls nyingi na majengo mengi ni matupu miaka sasa, Mkuki house sasa inaanza kujaa panya, Quality Centre and Plaza mnajua kinachoendelea pale.

Ukija jengo refu kuliko yote barabara ya Sam mujoma hapa karibu na Chuo /Mlima city iko wazi miaka sasa, hakuna wapangaji.

Ukienda zile flat za NHC zilizoko Morocco ziko tupu, China plaza Kariakoo inaelekea kuwa tupu, discount center wakitoka mle inakua gofu.

Ukienda mjini, Posta majengo mengi wameandika space to let, Rent here, space available.

Naona jengo jipya la Palm Village Millard Ayo amepewa kazi ya kupiga debe masaa 24, sina hakika kama wataweza kuhimili.

Je, hii inatokana na nini ama inaashiria nini kwenye uchumi huu wa kati?
kwani real estate ni majengo marefu tuu. mbona nyumba karibia zote zina wapangaji. kila siku watu wanajenga nyumba za kupangisha na wapangaji wapo
 
Back
Top Bottom