Hujaona sifa zake binafsi, wanasema havuti wala hanywi na ni mtu wa kwenda church kila jumapili
, hiyo jana kawasili Madrid kasindikizwa na familia nzima, baba, mama na kaka zake. Anaoneka mtu wa familia zaidi, sema huwezi jua, watu wanabadilika baada ya account kunenepa.
Kama ni hivyo, dimba la kati limepata mchezaji.
Game ya juzi Khedira alikuwa anazunguka tu pale kati, sasa hivi dogo atasimama na Kroos, na Modric akiwa fit yeye na Illara wote wanapigwa bei. Hapa sasa tunataka mpiga mabao wa kubadilishana na Benzema tu pale mbele, na yule Chicharito arudi kwa Man U.
.Kwahyo huyu lucas anakuja kumtoa james katika 1st 11?
.
James itategemea na kati ya Ancelotti na Kroos, kwasababu Kroos alikuwa anataka kucheza na Khedira. Ni mapema mno kusema nani atakuwa first eleven lakini kaa ukijua pale kuchukua namba kazi ipo. Ndio maana nakwambia Illara na Khedira wanasubiri msimu uishe tu, sasa hivi wapo wanasikilizia offer tu.
Nilisoma makala flani katka gazeti la Marca, wanadai Lucas Silva anakuja kua kama understudy wa Kross. Kipindi hicho understudy wa Modric, Isco ameshaiva na yupo tayari kumchalenge for 1st 11. Kuhusu Illara na Khedira, ni offer tu ndo zinasubiriwa..
Nadhani pia tunahitaji watu wa nguvu wa kuichallenge safu yetu ya ushambuliaji na si hawa kina Chicharito.
Lucas Silva: "I will train with my new team mates today. It's a dream for me to play with my idol Cristiano Ronaldo."
Kauli yake inaonesha ni kwa jinsi gani alivyo "humble" kwa kaka zake.. Hopeful idol wake CR7 atampa ushirikiano wa kutosha.
xyz123 umenena vyema ila nadhani ni vyema ukafanyika usajili wa players watakaoweza kuwapush kina bale na benzema ili wapambane zaidi. Kama ambavyo sasa modric atakavyobidi kuperform mara 2 zaidi ili kulinda nafasi yake maana isco wa sasa si yule wa kipindi msimu unaanza.
Hakuna wa kumweka james nje. James ni complete player, ana uwezo wa kupokonya mipira ( Sio kukaba), anauwezo wa kudrive timu, anaassist, anacheza long balls, anaposses mpira. So far hakuna wa kumweka benchi kwa sasa. Though udhaifu niliouona kwa james ni kuwa anapotea sana katika tough na physic games. Game zote na atletico alipotea kabisa uwanjani.
Lucas silva kwa nilivyoona clips zake ni mtu wa kunyanyua sana mipira. Ana consistency kubwa sana katika mipira ya juu na kuhamisha mipira toka upande mmoja kwenda mwingine kama ilivyokuwa kwa Alonso. Hivyo anachezesha timu akiwa chini, ana tackling skills nzuri so atasaidia.
Nionavyo kikosi cha kwanza kitaendelea kubaki vilevile modric akirudi
Iker, carvajal, ramos, pepe, marcelo, modric, kroos, james, bale, benzema, cristiano.
Isco na lucas silva, jesse wataendelea kutokea benchi.
Dogo anasema kweli kwamba alikuwa na ndoto za kuja kucheza Bernabèu, we kafika jana leo anataka kuanza maezoezi. Kwenye negotiation Cruzeiro walikuwa wanakomaa, dogo ikabidi kwenye hela zake apumguze euro millioni moja na nusu, kuwapa ili apate kusaini mkataba.