Redd's ina madhara kwa mjamzito?

Illuminata Rodgers

JF-Expert Member
Joined
Nov 25, 2015
Posts
2,845
Reaction score
2,024
Hellow jf,hivi kuna madhara yoyote yanayoweza kutokea kwa kiumbe kilichopo tumboni endapo mjamzito atakuwa anakunywa redd's kipindi cha ujauzito?
 
Redd's ina alcohol...

Alcohol inaweza kupita kwenye damu ya mama na kumfikia mtoto...

Madhara yake ni huwa inaathiri ukuaji wa chembe hai za ubongo, chembe hai za uti wa mgongo na chembehai nyingine za mtoto mwilini..

Hii ni kutokana na mtoto kutokua na uwezo wa kupambana na alcohol sababu ini linakua bado halijatengemaa kwa kazi hio
 
Hellow jf,hivi kuna madhara yoyote yanayoweza kutokea kwa kiumbe kilichopo tumboni endapo mjamzito atakuwa anakunywa redd's kipindi cha ujauzito?

Madhara ni lazima kwa sababu pombe inaingia kwenye mzunguko wa damu ambayo ndio inapeleka chakula na oksijeni kwa mtoto pia; hivyo nae atakuwa analewa wakati ule ubongo wake upo kwenye process ya kukua hivyo ukuaji kuathirika; na kuna uwezekano mkubwa wa kuwa mzito darasani, kufikiri, na hata kuwa na mental retardation.

Sitisha mitungi mpaka huyo kiumbe aingie duniani akiwa vizuri la sivyo itakula kwako. Badala ya hizo Redds, kunywa maziwa kwa wingi, na 'Ribena' ili upate mtoto bora kimwili na kiakili. Kwa maelezo zaidi kaulize clinic ingawaje wahusika watakushangaa sana!!
 
Nimekuelewa mkuu,ahsante sana!
 
Okay mkuu nimekuelewa,nashukuru sana kwa maelezo yako.
 
we dada ukijifungua nitaomba nimuone mtoto wako hata kwa kulipia au hata kuwa baba mlezi
 
Maziwa fresh or mtindi?
 
umemwanzishia nyuzi nyingi sana mpaka nimetokea kumpenda
Sawaa mkuu tuombe uzima,me jf ndo my best place ndo maana mengi yanatonitatiza nayaleta humu coz huwa napata ushauri mzuri wa kunituliza akili japo penye wengi pana mengi.
 
Pombe za nini?

Ukiwa mjamzito kula vyakula vyenye virutubisho.....ukipata kiu kunywa maji au juicy ya matunda ya kutengeneza mwenyewe

Hebu wajalini hao binadamu mnaotarajia kuwaleta
 
Pombe za nini?

Ukiwa mjamzito kula vyakula vyenye virutubisho.....ukipata kiu kunywa maji au juicy ya matunda ya kutengeneza mwenyewe

Hebu wajalini hao binadamu mnaotarajia kuwaleta
Sawa mkuu nimekuelewa but nilikua natumia kipindi siko mjamzito tangu niwe mjamzito sijawahi tumia ndo maana nikauliza ili nijue kama ni sawa kutumia hata katika kipindi hiki au lah,i real care.
 
Sawa mkuu nimekuelewa but nilikua natumia kipindi siko mjamzito tangu niwe mjamzito sijawahi tumia ndo maana nikauliza ili nijue kama ni sawa kutumia hata katika kipindi hiki au lah,i real care.
Sema kakiu kamekubanaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…