Toka uchaguzi wa vyama vingi uanze 1992 sijaona mwamuko wa kisiasa kama ninaoshuhudia leo, hii ni ishara ya mabadiliko makubwa kutokea siku ya kupiga kura ambapo wananchi wote watashirikishwa kufanya utafiti tofauti na utafiti wa REDET na Synovate unaowahusisha watu 2000 tu. People will prove REDET and Synovate wrong na aibu itaenda kwa mashirika hayo. Nina kila sababu:
Kukubalika kwa vyama vya upinzani hasa vijijini tofauti na miaka ya nyuma ambapo vilikuwa vinajulikana mijini tu, wananchi kuanza kuwakataa waziwazi wabunge wasiowataka ni ishara kubwa kuwa elimu ya uraia imefika kwao.
Vyama vya upinzani vilianza maandalizi ya uchaguzi mapema refer Operation Sangara ya Chadema na Operation Zinduka ya CUF. Kwa mara ya kwanza upinzani umeweka wagombea ubunge karibu majimbo yote hivyo kuonyesha ukaribu wake kwa wananchi.
Kuweka wagombea wanaouzika hasa ujio wa Dr. Slaa ulivyowashangaza wengi hata CCM hawakutarajia kwa hiyo hawakujiandaa kupata upinzani mkubwa. Imesababisha
- CCM kuanza kutumia mbinu chafu badala ya kutangaza sera mfano kuzungumzia maisha ya ndani ya Slaa.
- CCM kulitumia jeshi la wananchi badala ya Polisi ni dhahiri wameona nguvu ya upinzani ni kubwa.
Kwa mara ya kwanza viongozi ndani ya chama tawala kupinga wazi tena mbele ya vyombo vya habari utawala na uongozi wa Kikwete eg
- Tamko la MNF-kushindwa kuchukua maamuzi magumu
- Kutengwa kwa Kikwete na wanamtandao waliomuingiza ikulu
- waasisi wa chama hicho kujitenga na kampeni na kuiachia familia ya Kikwete.
Udhaifu wa kiutendaji wa Kikwete kwa miaka mitano na udhaifu wa kiafya(inajieleza).
CCM is not united again
- makundi yanayoendelea chini kwa chini na mengine waziwazi.
- maandalizi hafifu ya kura ya maoni ya CCM imebomoa badala ya kujenga chama
- wanahujumiana wenyewe kwa wenyewe
Kuvuja mapema kwa siri za wizi wa kura, mbinu gani kina nani wako wapi tofauti na miaka iliyopita, baadhi ya TISS kuhusishwa.
Jamii na wanaharakati wa haki za binadamu ikiwa ni pamoja na viongozi wa dini kuhamasisha waumini wao kujitokeza kupiga kura na baadhi ya ibada kubadilishwa.
- mfano makanisa ya Kakobe kusali Jumamosi badala ya Jumapili
- baadhi ya makanisa kufupisha ibada
- baadhi ya wanaharakati kutumika kujibu matamko refer Ananilea Nkya kumjibu Nsimbo.
Kama ilivyozoeleka wapinzani kuanzisha fujo safari hii CCM ndiyo imekuwa kinara wa kuanzisha vurugu(matukio ya hivi karibuni).
Kikwete kuzikataa hadharani kura za wafanyakazi na ujio wa kizazi kipya ambacho hakikupiga kura mwaka 1995 ni ishara kitafanya mabadiliko yatokee.
Pamoja na mambo mengine, haya ni baadhi ya mambo kwa mawazo yangu na uzoefu wangu kwenye mambo ya siasa huenda mwaka huu kukatokea mabadiliko makubwa Tanzania.
Angalizo: Mabadiliko hayo yanaweza kutokea kwa njia ya sanduku la kura endapo NEC watataka iwe hivyo au madadiliko hasi kwa njia mbadala.
Naomba kutoa hoja.