Elections 2010 REDET & Synovate hamtaweza kuzuia mabadiliko...

Wabongo bana nimewavulia kofia.. hizi tafiti uchwara zinashikiwa bango kana kwamba ni kijito cha maji jangwani. Kweli uono wa typical mbongo unaeza kweli hauzidi pua yake.

Hamjapata urais mnatutukana wabongo namna hivi, sasa je tukiwapa si mtakunya katika vichwa vyetu.

Jamani hawa wenzetu bado wanahitaji muda, maana ni wachanga, tena wachanga kweli kweli.

Mmmm ninamashaka na hawa wenzetu!!!!!
 
Mapungufu ya utafiti wa Synovate

Wakuu kwa mujibu wa tovuti ya wavuti, nimeona nachoweza kukiita matokeo rasmi ya utafiti wa Synovate. Bofya Hapa for further details. Kinachoshangaza kuna utitiri wa makosa ambayo aidha yanaipunguzia hadhi ripoti hiyo au kuifanya ionekane ya kupikwapikwa fasta fasta. Kwa taasisi kama hiyo yenye kaulimbiu inayoonyesha iko makini na ya kuaminika this is absolutely no good.

Kwa kuperuzi upesiupesi nimekutana na mushkeli zifuatazo.

  1. Typos. Ripoti ina utitiri wa typos as if imechapishwa na vile vi-secretarial bureau vya sinza. Mifano:
  • Ukurasa wa nane una swali kuhusu baadhi ya vijana waliojitokeza na wenye vipaji vya uongozi kuwa maraisi. Cha kushangaza kuna jina la Jakaya Kikwete na amekuwa wa mwisho with only 1% na kukubalika kwake in urban centers ni 0%. Sasa Synovate mtuambie hiyo 61% amepataje?
  • Ukurasa huo huo wa nane, who is Shyrose "Bhange"
  • Ukurasa huo huo tena wa 8 who the f**k is DR/RTA nafasi ya tatu
  • Ukurasa wa 11, who is "Chris" Mziray?
  • Ukurasa wa 11, who is "Fahoni" Dovutwa
  • Ukurasa huo huo wa 11, who is this Mutamwega "Mugaiwa"
  • Uk wa 12, who is "Wasila"
  • Uk wa 12 tena, who is "Nemroid" Mkono
2. Ukurasa wa 3 ni kuhusu utendaji wa serikali katika masuala ya jamii. Wakati JK na Kapuya wanatamba kuzalisha ajira zaidi ya 1,200,000. Utafiti huo wa Synovate unaonyesha 82% ya wananchi hairidhiki kabisa na utoaji wa ajira. Cha kushangaza zaidi watafiti wanasema eti watanzania wameridhika sana na utoaji elimu ya msingi na sekondari kutoka serikalini. Lakini ukiangalia jedwali uk wa 3 it is otherwise. Mimi nilifikiri kuridhika sana ni "Very satisfied" kama watafiti walivyoainisha kwenye jedwali lao.

3. Ukisoma uk. wa 12 inaonekana ni wazi watanzania hawaridhiki na utoaji wa huduma za jamii kwa serikali, on average approva iko on some 45%. Sasa inakuwaje kiongozi wa serikali hiyo hiyo aonekane yeye ni mchapa kazi???

4. Ukurasa wa 4 watafiti wanasema watanzania 78% wanaridhishwa na utendaji wa JK, na 77% na utendaji wa Shein (Kwa lipi?). Na kama hii nni kweli sasa mbona hii inakinzana na suala zima la uwajibikaji kama ambavyo watafiti wenyewe wameainisha. Inakuwaje watanzania hao hao wasioridhika na utendaji wa taasisi za serikali na na kuuona uko chini ya average of 45% waridhiswe na viongozi wa serikali hiyo hiyo????

5. Uk wa 4 kuna swali linauliza unaziamini vp taasisi zifuatazo, mojawapo ya hizo taasisi ni TUCTA, gimme a break TUCTA inaingiaje hapa kwa nini isiwe TAMICO, au kile chama cha wahadhiri. TUCTA haiwahusu wafanyakazi wote let alone watanzania wote. Tunachofahamu ni kwamba TUCTA imekuwa na msuguano na serikali kwa muda kiasi kuhusu maslahi ya wafanyakazi na wanaotakiwa kuiamini au kutoiamini ni wanachama wake sasa mtanzania mkulima aliyeko Maneromango, Tandahimba au Nkasi TUCTA inamuhusu nini?

My Take:
Kama hii ndiyo ripoti rasmi basi ingekuwa ni mchezo tungeomba turudishiwe kiingilio. Hawa jamaa wanaonyesha hawako serious kabisa na kuna kila dalili hii ripoti yao imepikwa.
 
Mods pls mnaweza kunirekebishia hiyo heading, bdala ya syovate isomeke synovate!
 
Utoto mtupu kamanda, Synovate wameshurutishwa kutoa matokeo yao haraka na mteja wao ili kuzidi kuangamiza saikolojia za wapiga kura ionekane kwamba mkulu ndiye chaguo.
Sisi tafiti yetu tutaifanya kwenye sanduku la kura walah!
 
Utoto mtupu kamanda, Synovate wameshurutishwa kutoa matokeo yao haraka na mteja wao ili kuzidi kuangamiza saikolojia za wapiga kura ionekane kwamba mkulu ndiye chaguo.
Sisi tafiti yetu tutaifanya kwenye sanduku la kura walah!

Yea yaani it's so funny!!!!!!!!
 
REDET walisema JK ana-drop na Kinana kukubaliana nao ila si kwa asilimia 100 na Dr. Slaa anapanda (Mwananchi 9/10/2010). Sijui REDET walifanya lini na Synovate lini, lakini kama REDET walianza, wakafuata Synovate basi ni kweli JK ana-drop tena kwa kasi, na kufikia 31 October 2010 atakuwa kwenye 40% na Dr. Slaa 45%!!!!!!!!!!!!!!
 

ahsante
 
Tatizo ccm na vibaraka REDET & SYNOVATE wako busy kuzuia maji ya mto kwa wavu wa kuvulia samaki! Shida ndiyo iko hapo.
 


Who could be the Synovate's client in this case? CCM, I presume Angalia rangi nyekundu na ni wazi wapo kibiashara zaidi na wanajenga mazingira ya kibiashara
 
Wana JF, salamu kwenu nyote.

Kama tulivyoona tarifa ya utafiti wa REDET, hayo yaho yamejitokeza kwa SYNOVATE
"STUDY zao sio representative enough". HAitoshi kutuambia uliwahoja wanawake na wanaume achilia mbali uchache wao...lazima watuambia NYUMRI na ELIMU ZAO na ikiwezekana UKEREKETWA WAO maana kuhoji watu kwenye mkutaano wa kampeni wa ccm lazima majibu waliyoyatoa yatajidhihirisha.

Baada ya kusoma ripoti ya SYNOVATE nashindwa kuelwewa vitu vichache...nitanukuuu gazeti la daily news kama walivyomnukuu bossi wa synoivate, shangaaaa....

1. It was conducted from September 5 to 16, this year. Leo ni 1 month tangu wamalize kukusanya data....majobu wanayatoa 1 month later kwamba ndio hali ilivyo sasa.

2. the study involved 2,000 respondents from 63 districts in 26 maana yake watu 2000/wilaya 63 = watu 31 hii ni adadi ndogo sana, less than idadi ya watu kwa kijiji kimoja ( maana yake ni watu wa mabalozi 2 maana ile dhana ya balozi 1 watu kumi ilishakufa...leo ni zaidi ya hiyo...

KAMA DATA ZAO NDIZO HIZI wanapata wapi kiburi cha kutuambia kuwa hii ndio hali halisi na kwamba kama uchaguzi ungefanyika leo basi CCM ingepata 90%?

NAsikitika taaluma ya utafiti imeingiliwa....
 
Great Thinkers aka Great Fans wa Chadema wamecharuka humu!!!!
 
Mwakani tunatimiza miak 50 tangu tupate UHURU. Tumetawaliwa na watu wale wale kipindi chote hicho, na sasa tuko hoi. Hakuna Mtanzania asiyejua hilio.

Sidhani kama kuna Mtanzania wa kawaida anayependa tuanze miak 50 mingine na chama tawala kile kile kilichotudidimiza kasi hiki. Lazima tubadilishe, kwani tukichagua watu wale wale hali itaendelea kuwa ile ile ya UFISADI, USANII mtupu!

Sasa kama hivyo ndivyo, hao Watanzania wa ajabu ambao wameonwa na REDET na Synovate kwamba wanataka tusibadili chochote wako wapi?

Opinion poll zote ambazo ni huru (kwa maana ya kuwa hazipitii mkononi kwa mtu - ya JF, ya Daily News, ya Majira) zinaonyesha Slaa anapata kwenye 70%.

Bila shaka basi huu upuzi wa Redet na Synovate ni maandalizi ya wizi wa kura. Tuwe macho wananchi. Tumetawaliwa na CCM bila maendeleo kiasi cha kutosha. Sasa tunataka kuwangoa.

Itabidi CHADEMA, na sisi wananchi tutafute mbinu za kuzuia kuibiwa kura zetu. Kama hesabu za kura mahali zinaonyesha Slaa kapata 91, 100 basi na huko kwenye majumuisho ya mwisho ifike hiyo 91,100, na sio ifike 9,100 badala yake.
 
Hawa ndo pweza wetu, kama yule wa Kombe la Dunia.

Hata kama ni utafiti wa kubuni wangejitahidi kutumia usomi wao. Unatafiti, sample size yao haifikii hata 40% halafu wanatoa matokeo na kuyabariki. Wanajiita wasomi!.

Hapo UD jamani, hicho chuo kweli ndo kile kilichowatoa akina Museveni, Garang, nk. Hapo ndo walipokuwa akina Rodney? UD yenye patriotism imekuwa ni ya hypocrisy.

Kumbe ndo umuhimu wa kuwa na vyuo zaidi ya 30 nchini. UD mumetuangusha kabisa!

Niliwahi kuandika hapa kwamba Dr Benson wa REDET sioni kama ana qualities zozote za kuwa 'msomi.' Au hiyo PhD? No! Hata ukimuangalia usoni haonyeshi dalili za intelligence, na huyo ndo brain engine ya REDET. Anao ufahamu wa kawaida tu lakini si kwa kiasi cha kutushawishi kwamba kasema tusiyoyajua. Au alipewa favour kwa ukabila maana nasikia nalo ni tatizo.

Angalia hata arguments zake anapohojiwa kwenye TV. Jamani!

Poleni wanafunzi wake.
 
Matokeo ya utafiti yanatoa muongozo wa nani anaweza kushinda, na hayo yanaweza kubaki hivyo endapo upepo utabaki kuwa kama ulivyokuwa wakati utafiti unafanyika.Ikumbukwe kuwa katika ulingo wa siasa muda ni kitu muhimu sana kwani ndani ya wiki moja upepo wa siasa unaweza kutoa ishara tofauti na mwanzo.

Hebu tujikumbushe yaliyotokea wakati ule George Bush alipopambana na John Kerry wa Democratic huko Marekani.Mtakumbuka John Kerry aliendelea kuongoza tangu mwanzo wa kampeni hadi wiki ya mwisho ya kampeni.Lakini mambo yalibadilika zikiwa zimebaki siku saba kupiga kura,Pale ulipofanyika mdahalo wa mwisho, ambapo John nkerry aliulizwa swali moja la msingi kuhusu msimamo wake juu ya NDOA ZA JINSIA MOJA.

John kerry alijibu kuwa ndoa za jinsia moja ni uhuru na haki ya mwanadamu kuamua.Ikumbukwe kwamba John Kerry ni mkristu Mkatoliki kanisa ambalo linapinga kwa nguvu zote ndoa za jinsia moja. Kwa upande wake George W.Bush alipoona mwenzake kachemsha alipinga huku kionyeshwa kukerwa sana na swali lile kwa maaana kwamba halikupaswa kuulizwa kwani HAIKUBALIKI katika dini ya kikristu na kumbuka Bush ni muumini wa madhehebu ya Mashahidi wa yehova nayo yanapinga vikali.

Baada ya majibu hayo John KERRY upepo ulimwendea vibaya kuliko kawaida yake kwani wakatoliki wote walimhama kwa kuwadhalilisha kukubali kutoa uhuru wa watu kuamua badala ya kuzuia kwa nguvu zote.
NA HAPO KERRY ALIANGUKA NA KUMUACHA BUSH AKIPETA.

Ninachotaka kusema kwa upande wa Tanzania ni kwamba, kura za utafiti zilizotolewa kwa mfululizo kwa makampuni mawili tofauti, REDET NA SYNOVATE ndani ya masaa 72, haziwezi kutushawishi moja kwa moja kuwa JK ndiyo atakuwa mshindi, la hasha hizi zinawakilisha muda Fulani tu, zinaweza kubadilika kuendana na kampeni zinavyobadilisha upepo na pia wapiga kura kuendelea kuelimika kwa kusikiliza sera.
Kwa mfano:utafiti umefanyika septemba muda ambao JK alikuwa hajamnadi.Rostam, Mramba, Lowasa, chenge na wengine Mafisadi, tukumbuke sasa hivi watu wanalalamika kwa nini afanye hivyo hata wana CCM wenyewe.Rejea jana hotuba ya Sumaye pale AR-KKKT

Mazingira ya kura hizi pia yanaonyesha kupikwa kwa mtindo wa PROPAGANDA ILI KUWAKATISHA TAMAA WAPIGA KURA.
Tukumbuke JK nimtaalam wa PROPAGANDA na kwamba kaisomea anajua fika namna ya kuitumia na ndiyo maana yawezekana matokeao HAYA YAMEMSAIDIA KUMUINUA kwa kiwango Fulani.Lakini baada ya muda watu watasahau.

NINI KIFANYIKE
Wadau/chadema waendelee kuwaelimisha wapiga kura na kuyakataa kwa nguvu zote matokeo kwa kutumia PROPAGANDA PIA, maana dawa ya moto ni moto.Kwa kufuatilia kwangu nimendua matokea hayana IMPACT kwa wapiga kura ila faida ya haya matokeo kwa JK ni kwamba sasa anao uwanja uliobarikiwa kumuwezesha kuiba kura kwani atajitetea hata tifiti zimeonyesha ndiyo maana kafanya tafiti zaidi ya mbili ili kutoa uwanja mpana wa kujitetea.CHADEMA wajizatiti kuimarisha ulinzi wa kura na kuziba mianya yote .YOTE YANAWEZEKANA KWA KUMTUMAINI MUNGU
 
Imetangazwa na Synovate mchana huu

KIkwete - 61%
Dk Slaa - 16%
Prof Lipumba - 5%

Less 18%. Kumbe ni rahisi kuitwa profesa. Kwa miaka mitani iliyopita lazima ripoti hizi zimpandishe mtu kuwa Prof.
 
We must ask themselves, Who pays for the research and for whose interests! After knowing that, everything will be vivid! Kwa nini REDET, na Synovate watoe matokeo kama hayo. All I know ni kwamba wanatumikia kafiri mwanharamu apite ila wanajua ukweli ni upi! Aluta Continua
 
Yes kwa hiyo inamaaana mpaka 31 atakuwa negative! wanahaha hao kutafuta njia za kuiba duuu!
 
Hawa jaama REDET na synovate ni wapuuzi sana na wanatangaza upuuzi wao kwa kuwasaliti watanzania na mijitu kama hii ndio chanzo cha fujo kutokana na tamaa ya kula hela za mafisadi
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…