Elections 2010 REDET walituambia, tukawakejeli

Elections 2010 REDET walituambia, tukawakejeli

JF tulisema mapema kabla ya REDET kushindwa kwa wabunge wa CCM tena basi JF ilisema hata mbinu za kuwamwaga wapiganaji REDET hawakufika huko. Tatizo kubwa la REDET ni jinsi gani walitumia ukusanyaji wa data zao kuhusiana na imani ya wananchi kwa viongozi hasa kiti cha Ikulu.

Binafsi unapoanza na kuonyesha uwezekano wa makosa kuwa ni ya mbunge na sio ya rais kisaikologia unamjengea mtu majibu ya mkosa. Kama mtu akimlaumu mbunge wake mara nyingi hushindwa kuunganisha lawama hizo na uongozi wa juu yaani rais..

Pia unaposhindwa kuweka upinzani badala yake ukaweka Ukuta ni upotoshaji wa makusudi ikiwa maswali yenyewe hatayahusiana na utendaji kazi wa kiongozi aliyepo haswa ikiwa hakuna kipimo halisi cha mafanikio yanayohusu particular areas. REDET walipanga matokeo kama yale ya refa wa mpira baina ya Ivory Coast na Brazil kuachia goli akijua wazi mkono ulitumika mara mbili kusogeza mpira mbele..
Na hakika Ushindi utapatikana, hakuna utabiri unaopangwa.
 
uchaguzi hauko mbali, akina CHADEMA mtaona ukweli wa REDET mwaka huu ni wa kikwete tu, sio mwengine
 
Ninapozungumzia objectivity katika utafiti, ni tafiti zote ziwe za REDET, JF au SYNOVATE. Ili kupata majibu yaliyo sahihi utafiti unatakiwa uwe na sample kubwa ambayo pia ni representative, mfano mzuri ni huu utafiti wa JF unauliza kama wanajanvi wanaipenda serikali ya Jakaya au La. Sample ya watu wanaoulizwa ni biased kwasababu wengi wa wanajanvi naweza kusema hawaipendi ccm na ni wachache sana ukilinganisha na population ya million 40 ya waTanzania, kwahiyo basi ni dhahili kuwa matokeo yake yataiponda CCM na hayatakuwa representative ya maoni ya majority ya WaTanzania!! Hivyo hivyo kwa taasisi za REDET na SYNOVATE!! Synovate kwa mfano tafiti zake hazitiliwi maanani sana kule Kenya kwa sababau hizi hizi za kuwa biased for the establishment.

Umesomeka mkuu 100%! Hata hivyo, tatizo la wengi kwa REDET sio kutokuwa technical, tatizo la wengi ni kwamba REDET wanamtabiria JK kutokana na utafiti wao! Hata kama wangezingatia yote hayo, bado wasiokubali ukweli wangepinga tu tafiti hizo za REDET kv kilichomo humu ndani ni ushabiki zaidi kuliko kuangalia fact! Mathalani, binafsi si mwanachama wala shabiki wa CCM lakini hata hivyo nitakuwa najidanganya nikisema kwamba Slaa atamshinda JK kv sitakuwa nimeangalia hali halisi ilivyo! Suala la sample ni muhimu kwa 100% na ndio maana "sample" ya uhakika imakuja october 31, 2010
 
Mwelekeo wa matokeo ta tafiti za REDET hata wakifanya sasa baada ya DR. Slaa kuingia ulingoni hayatakuwa tofauti na matokeo yao ya awali kwasababu nilizoziainisha hapo awali. Tafiti zao zina malengo mahususi!!

Mkuu Bulesi, mi nahisi nimekusoma ile mbaya! Unajuwa nimekusoma nini, inawezekana kabisa kwamba utafiti wa REDET una malengo maalumu na kubwa zaidi la kumng'alisha mkulu; au sio mkuu Bulesi?! Sasa tuachane na hayo mapungufu ya REDET ambayo hata hivyo ni ngumu kuyathibitisha! Assume utafiti ule unafanywa na taasisi isiyo na mafungamano yoyote na JK au CCM, hivi ni kweli matokeo yake yatakuwa tofauti na yale ya REDET?!
 
REDET walishazungumza mapema! Watu wakawakejeli kwamba eti wanatumiwa!! Gazeti la Tanzania Daima likadai eti REDET inatumiwa na Kikwete; kwamba REDET wanapotoa utafiti kuonesha kukubalika kwa Kikwete kunajenga saikolojia ya wapiga kura wamchague Kikwete!! Aibu zaidi, Tanzania Daima waliibuka na tahariri iliyoikandia REDET; kwavile tu ripoti hiyo ya REDET ilionesha Kikwete angeshinda kwa asilimia nyingi endapo uchaguzi mkuu ungefanyika wakati wa utafiti uliokuwa umefanyika na REDET!

Bila shaka Tanzania Daima wangekubaliana na utafiti wa REDET endapo ungesema CHADEMA kingeshinda!! Wakati Tanzania Daima walipotoka na tahariri ya kukejeli utafiti wa REDET, walisahau kwamba siku chache tu kabla ya hapo wao walikuwa wameibuka na kura za maoni zilikuwa zimeendeshwa humu JF!

Hata wana CCM nao wakaupinga utafiti wa REDET, kisa tu kilitabiri mabaya kwa wabunge kadhaa kwamba wangepigwa chini!! KIKO WAPI? Nyota njema imeonekana asubuhi! Asubuhi asubuhi, tayari wabunge kadhaa wa CCM wamegalagazwa hata kabla ya uchaguzi mkuu wenyewe bado! Nasikia karibi wabunge 50 chali na game bado linaendelea! Hao ni wale waliopteza mikononi mwa wana-CCM wenzao! Je, ni wangapi kwa waliosalia watakaopoteza viti vyao kwa upinzani?!


Mimi si Mwana CCM, CHADEMA wala REDET; ila ningependa kuwashauri Watanzania kujenga utaratibu wa kuamini tafiti zetu! Sina hakika, lakini naamini REDET imeundwa na wasomi hivyo kubeza tafiti zao ni kubeza umuhimu wa wasomi wetu.
Kama unashawishika na UTAFITI wa REDET basi naamini kuwa wewe ni another custodian wa brainwashed wa hilo dubwasha.
Pamoja na kuundwa na wasomi kedekede tena mahiri, ukisoma dots na dotis utagundua kwamba wanachikisema sich cha kweli. Wao tafiti zao zipo ktk MYTH na sanasana wanajaribu kubalansisha wasionekane kuwa wanaelemea upande wa JK.
Siwakandyi REDET lakini nawaouts kwa kutokuwa wazi na wakeli ktk tafiti zao.

Hebu fikiria wanakwamba UCHUMI umepanda kwa asilimia kadhaa while at the same time kuna backfall ya shilingi zaidi ya asilimia 50. Unadhani inahitaji USOMI kugundua mwangaza wa JUA?

REDET na SYNOVATE go TO HELL
 
Mkuu Bulesi, mi nahisi nimekusoma ile mbaya! Unajuwa nimekusoma nini, inawezekana kabisa kwamba utafiti wa REDET una malengo maalumu na kubwa zaidi la kumng'alisha mkulu; au sio mkuu Bulesi?! Sasa tuachane na hayo mapungufu ya REDET ambayo hata hivyo ni ngumu kuyathibitisha! Assume utafiti ule unafanywa na taasisi isiyo na mafungamano yoyote na JK au CCM, hivi ni kweli matokeo yake yatakuwa tofauti na yale ya REDET?!

NasDaz Mkuu, let us assume kama unavyoshauri kuwa independent researcher aje leo afanye utafiti juu wagombea wetu wa urais; mimi ninahakika kabisa matokeo yake kama sample yake itakuwa representative yatakuwa tofauti na yale ya REDET!!Hali ya maisha ya waTanzania ni mbaya sana kiasi kwamba sioni jinsi ambavyo mgombea wa urais wa ccm ataweza kuibuka mshindi kwenye utafiti huo; ingawa anaweza kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa October kwa vile wataiba kura [absence of level playing field]!! Kumbuka tu kwamba malengo makubwa ya hizi opinion polls ni kushawishi mwelekeo wa wapiga kura.
 
NasDaz Mkuu, let us assume kama unavyoshauri kuwa independent researcher aje leo afanye utafiti juu wagombea wetu wa urais; mimi ninahakika kabisa matokeo yake kama sample yake itakuwa representative yatakuwa tofauti na yale ya REDET!!Hali ya maisha ya waTanzania ni mbaya sana kiasi kwamba sioni jinsi ambavyo mgombea wa urais wa ccm ataweza kuibuka mshindi kwenye utafiti huo; ingawa anaweza kuibuka mshindi kwenye uchaguzi wa October kwa vile wataiba kura [absence of level playing field]!! Kumbuka tu kwamba malengo makubwa ya hizi opinion polls ni kushawishi mwelekeo wa wapiga kura.

Nikuambie kitu kimoja mkuu Bulesi, inawezekana kabisa kwamba tradition ya tafiti kama hizi zinalenga kushawishi watu kufuata uelekeo fulani! Lakini hata hivyo, it can hold true kwa nchi kama america na ulaya ambako watu wapo sensitive sana na issue kama hizi lakini sio hapa TZ! Endapo watanzania wengi wangekuwa ni kama waliopo Dar hususani wale wenyewe uelewa kidogo labda madai yako yangekuwa perfect! Lakini kusema kwamba utafiti wa REDET au SYNOVATE una impact kwa wapiga kura walio wengi (ambao wapo vijijini), tutakuwa tunajidanganya! Watanzania, hususani tuliopo mijini tunasahau kabisa kwamba Watanzania wengi wapo vijijini na ndio hawa walio tayari kuacha kazi zao na kwenda kupiga kura. Kwa bahati mbaya, wengi wa watanzania wa vijijini wana misimamo( nieleweke kwamba mtu mwenye msimamo ni yule asiyetaka kubadilika hata kama ukweli anauona) yao. Wakiiona Helikopta ya Slaa,wataikimbilia na kufurahia, lakini akitoka anatoka yeye na kuwaacha na msimamo wao! Wala haiitaji shahada kulifahamu jambo hili! Kwani, tuseme Slaa ameenda kijiji fulani na kupokewa na umati mkubwa wa watu! Akishaondoka, anakuwa ameacha wanachama wangapi wa CHADEMA nyuma yake? atakuwa ameacha ofisi yoyote ya CHADEMA nyuma yake? Tutake tusitake, CCM wataendelea kusurubu hadi pale vyama vya upinzani vitakapokuwa na misingi vijijini! Wala sisemi haya kwa kuyafurahia, bali ni kwa uchungu kv ningependa kuona upinzani wenye nguvu! Mimi ni mtu wa Lindi, among of the poorest regions in TZ, lakini mara zote CCM wanashinda kwa kishindo coz' upinzani umeshindwa ku-take advantage na kujichimbia kule tu ambako waasisi wa vyama vya upinzani wana asili nako! Yaani upinzani unasubiri hadi atokee mtu kwenye mkoa fulani na yeye afanye jitihada binafsi kama ambavyo alifanya Dr. Kaborou (na sasa Zitto) na CHADEMA kule Kigoma! Mkuu Belesi unataraji vipi chama kilichojikita kwenye baadhi tu ya maeneo kiweze kushindana na chama kilicho na mizizi hadi kwenye vyoo vya wafungwa
 
Back
Top Bottom