Just Distinctions
JF-Expert Member
- May 5, 2016
- 3,230
- 6,742
hahahah siku hizi ni Kabumbu tu na uchambuzi wa kijanja kijanja mixer kugoogle kwingi. Media imeona fursa kwenye michezo hasa mpira wa miguu maana hata hivyo vipindi vya michezo unavyosema zaidi ya asilimia 90% ni mpira wa miguu, chache inayobaki ndio michezo mingine ila kupata hata mchambuzi wa masumbwi, mpira wa kikapu, mpira wa pete au wa wavu aisee ni ngumu sana.
karibia wote ni mpira wa miguu tu, unaweza kukuta kipindi cha michezo kimesheheni wachambuzi wanaojiita ‘manguli' ila hamisha swali toa kwenye mpira wa miguu peleka kwenye mchezo wowote ule hata mpira wa kikapu uone jinsi wanavyopoteana hamna wanachojua wote wamemeza mipira tu, na u-Simba na U-Yanga mwingi.
Itoshe kusema kuwa hapa Tanzania tuna vipindi vingi sana vya mpira wa miguu ila tuna vipindi vichache sana vya michezo.