Refa aliyeinyima bao Yanga aondolewa kwenye Ligi Kuu

Refa aliyeinyima bao Yanga aondolewa kwenye Ligi Kuu

John Haramba

JF-Expert Member
Joined
Feb 4, 2022
Posts
365
Reaction score
1,374
Refa aliyeinyima bao Yanga aondolewa kwenye Ligi Kuu

Yanga.jpg
 
Hawa waamuzi vilaza walitakiwa kushushwa kabisa madaraja ili iwe fundisho kwa waamuzi wote wasio na sifa.

Kitendo cha kuwafungia kuchezesha michezo mitatu na baadaye kuwarejesha, kuchangia kuharibu mwenendo mzima wa ligi.

Mfano ni huyu Ahmada Simba! hii ni mara ya pili anainufaisha simba kupitia maamuzi yake yenye utata! Anafungiwa, baadaye anarudishwa tena!!
 
Kuwe na faini za pesa, watu wametumia fedha kuweka kambi na kujiandaa, halafu anatokea mburura mmoja tu anafanya yake uwanjani...

Kama mwamuzi hawezi tafsiri sheria apigwe chini, sababu moja ya kazi ya mwamuzi ni kuhakikisha sheria zinatafsiriwa
 
Heading inaonyesha yanga kunyimwa goli.. maelezo ya chini yanahusu match ya simba.. aliekwambia uwe unandika uzi huku njaa inakufinya ni nani?
 
Kuna mmoja aliwahi kuua move ya Simba wakiwa kwenye box na wakiwa na uwezekano wa kufunga.Huyo hakuchukuliwa hatua eti tu kwa vile Simba hawakufanya press kulalamika.

Bodi ya ligi mnaendeshwaje na mihemko ya utopolo?
 
Kwani mayele alifunga ule mpira? Au unataka upewe goal wakati mpira haukuingia golini.
Ukiondoa ukolo kichwani mwako, ukaangalia vizuri ile move utagundua kuwa mayele aliuacha ule mpira sababu firimbi iliita na kwa kuwa hamna hata VAR bongo hakuona haja ya kuumalizia. Otherwise alishampiga chenga mpaka goalkeeper so it was obvious angefunga.
 
Swali la kujiuliza

Kwa nn waamuzi wana maamuzi ya namna hii...? Tukijiuliza kwa mapana yake tutatatua tatizo la waamuzi. Hapa kuna mambo mengi sana sana ya kujadili juu ya waamuzi wa nchi hii. Ikumbukwe hao ni waliochezesha Simba na Yanga ndio wanalaumiwa je huko championship hali ikoje? je mechi za timu za kawaida hua tunayaona hayo matokeo??

Turudi kwenye ishu ya goli la Mayele binafsi hata kama ningekua mwamuzi ningepuliza kipyenga kwa sababu moja; refa alidili na foul kwanza kabla ya mpira kumfikia Mayele tayari alipuliza kwa sababu mtoa pasi alikua ameenda chini wakati anaupiga mpira ule. Ni 50/50 ile hata ingekua advantage huenda angekosa au angepata watu wanakosa penalty sembuse kua marking na beki...? Ni vile tuna picha za marejeo ila matukio ya papo kwa papo mbona wengi tu tungefanya maamuzi ya utata na vituko endapo tungekua marefa kweli.

Ni vile tu hizi timu zinatupandisha presha game na Namungo watu wa Yanga mbona hamuongelei penati isiyokua halali au kwa sababu ilikua upande wenu na Namungo sio timu kubwa hawana wa kuwasemea??

Watu wa Simba mechi vs Mbeya kwanza goli lilikua offside hili nalo vipi??

Ni vile tu tuna usimba na uyanga uliopitiliza level za ushabiki wa mpira ule utani wa jadi.

Nachokiona Yanga pressure ipo juu na kinachofanyika ni kuomba huruma ya hadhira incase ikitokea ya kutokea watakua na sababu. Kama walivyofanya simba kwa mtibwa.


Ni vyema tujue kiini cha ubovu wa kimaamuzi wa marefa wetu na kuamua kuchukua hatua. Huko Afcon kulikua na maamuzi ya hovyo sana kuliko hata ya huku kwetu, EPL bahati kuna VAR vinginevyo tungejionea maajabu ya kimaamuzi.
 
Back
Top Bottom