Jerome Damon Refarii Mstaafu na Mkufunzi wa matumizi ya VAR wa FIFA, ameungana na maamuzi ya kulikataa goli la Yanga dhidi ya Mamelod sundown.
Damon amesema Kwa Sheria ya VAR kwanza kunakuwa na uamuzi wa awali ambao ni wa uwanjani (on-field decision) halafu VAR hutumika kuyakagua (check) maamuzi ya awali.
Damon ametolea mfano Wa Mechi kati ya Ujerumani na Japan ambapo vyombo vya habari vilionyesha kuwa kulikuwa na goli Lakini teknolojia ya mstari wa goli ilionesha mpira wote ulikuwa haujavuka mstari wa goli.
Damon anasema maamuzi yale huenda yalitokana na kutokuwepo na Camera Juu ya goli kuthibitisha kama ule mpira ulivuka mstari wa goli.