Refa na Mkufunzi wa FIFA akataa goli la Yanga

Refa na Mkufunzi wa FIFA akataa goli la Yanga

Allen Kilewella

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2011
Posts
21,470
Reaction score
40,593
Jerome Damon Refarii Mstaafu na Mkufunzi wa matumizi ya VAR wa FIFA, ameungana na maamuzi ya kulikataa goli la Yanga dhidi ya Mamelod sundown.

Damon amesema Kwa Sheria ya VAR kwanza kunakuwa na uamuzi wa awali ambao ni wa uwanjani (on-field decision) halafu VAR hutumika kuyakagua (check) maamuzi ya awali.

Damon ametolea mfano Wa Mechi kati ya Ujerumani na Japan ambapo vyombo vya habari vilionyesha kuwa kulikuwa na goli Lakini teknolojia ya mstari wa goli ilionesha mpira wote ulikuwa haujavuka mstari wa goli.

Damon anasema maamuzi yale huenda yalitokana na kutokuwepo na Camera Juu ya goli kuthibitisha kama ule mpira ulivuka mstari wa goli.
 
Anaetakiwa kusema ni goli au sio goli ni kipa wa Mamelodi ambae shuti kali la Aziz Ki lilimshinda!

Wanayanga sasa tuanze kumsakama kipa Williams instagram yake na Instagram ya Mamelodi hadi kipa afunguke, ye ndo mtu pekee aneujua ukweli maana ni mtu pekee aliekuwa karibu na goli na mpira uliopigwa na kumshinda, mwenye akaunti yake ya instagram aweke hapa, hatuhitaji VAR kwasasa wamefanya ni kichaka cha kuhalalisha haramu kwenye soka!

hao sijui wakufunzi Mara sijui marefa lazima wamtetee refa mwenzao, lile ni goli halali zingine stori tu
 
Ya Japan

FB_IMG_17125893789508054.jpg
 
Back
Top Bottom