Refa na Mkufunzi wa FIFA akataa goli la Yanga

Refa na Mkufunzi wa FIFA akataa goli la Yanga

mbona jamaa kama haelewi anaongea nini? Kama kamera ya juu ilikuwa haipo haimaanishi ndio sio goli.
 
Jerome Damon Refarii Mstaafu na Mkufunzi wa matumizi ya VAR wa FIFA, ameungana na maamuzi ya kulikataa goli la Yanga dhidi ya Mamelod sundown...
Kama halikuwa goli basi ilikuwa kona, swali fikirishi baadae ya kulikataa goli kwanini hawakupewa kona, njia za muongo ni fupi
 
Kwanini refa hakwemda kujiridhisha kama alivyofanya kwa faulo ya Lomalisa?!
 
Kasema ni mpaka kuwe na ushahidi Wa zaidi ya kamera Moja kuthibitisha goli
Sasa yeye kaconcludije kama sio goli wakati hakuna huo ushahidi? Pia kama sio goli ilikuwa ni nini? Je kwanini refa alidundisha mpira na kumpa kipa wa Mamelodi aanzishe wakati beki wa Mamelodi aliutoa nje na kipa kuudakia nje?
FB_IMG_1712610676296.jpg

Mzee kakazia kauli yake.
 
VAR kimsingi hapo haina msaada sana zaidi ya ingekuwepo Goal line technology
VAR ililetwa kwa gharama zote zile ili kusaidia kuondoa makosa ya kibindamu yanayoweza kufanywa na refa kwa kuruhusu replay ya mchezo na kuuanglia kutoka pande tofauti. Refa kukataa kutumia VAR ni sawa na kulazimasha maklosa makosa yake ya kibindamu yakubalike, jambo ambalo siyo sahihi.
 
Anaetakiwa kusema ni goli au sio goli ni kipa wa Mamelodi ambae shuti kali la Aziz Ki lilimshinda!

Wanayanga sasa tuanze kumsakama kipa Williams instagram yake na Instagram ya Mamelodi hadi kipa afunguke, ye ndo mtu pekee aneujua ukweli maana ni mtu pekee aliekuwa karibu na goli na mpira uliopigwa na kumshinda, mwenye akaunti yake ya instagram aweke hapa, hatuhitaji VAR kwasasa wamefanya ni kichaka cha kuhalalisha haramu kwenye soka!

hao sijui wakufunzi Mara sijui marefa lazima wamtetee refa mwenzao, lile ni goli halali zingine stori tu
Kipa nae nadhani hakuona kitu aliona nyota nyota tu .Lile shuti lilikuwa Kali sana la spidi ya ndege za kivita za urusi.Kipa aliona tu mpira umerudi kwa kuwa baada ya shuti kumshinda alibaki anagaragara tu golini.
 
Jerome Damon Refarii Mstaafu na Mkufunzi wa matumizi ya VAR wa FIFA, ameungana na maamuzi ya kulikataa goli la Yanga dhidi ya Mamelod sundown.

Damon amesema Kwa Sheria ya VAR kwanza kunakuwa na uamuzi wa awali ambao ni wa uwanjani (on-field decision) halafu VAR hutumika kuyakagua (check) maamuzi ya awali.

Damon ametolea mfano Wa Mechi kati ya Ujerumani na Japan ambapo vyombo vya habari vilionyesha kuwa kulikuwa na goli Lakini teknolojia ya mstari wa goli ilionesha mpira wote ulikuwa haujavuka mstari wa goli.

Damon anasema maamuzi yale huenda yalitokana na kutokuwepo na Camera Juu ya goli kuthibitisha kama ule mpira ulivuka mstari wa goli.
Ok, huyo refa mstaafu amezungumza lolote kuhusu kwanini haikuwa kona?
 
Anaetakiwa kusema ni goli au sio goli ni kipa wa Mamelodi ambae shuti kali la Aziz Ki lilimshinda!

Wanayanga sasa tuanze kumsakama kipa Williams instagram yake na Instagram ya Mamelodi hadi kipa afunguke, ye ndo mtu pekee aneujua ukweli maana ni mtu pekee aliekuwa karibu na goli na mpira uliopigwa na kumshinda, mwenye akaunti yake ya instagram aweke hapa, hatuhitaji VAR kwasasa wamefanya ni kichaka cha kuhalalisha haramu kwenye soka!

hao sijui wakufunzi Mara sijui marefa lazima wamtetee refa mwenzao, lile ni goli halali zingine stori tu
Kwahiyo, unataka mshitakiwa ajihukumu..!!
 
Back
Top Bottom