Refa wa Simba, Yanga ajadiliwa usiku mnene Dar

Refa wa Simba, Yanga ajadiliwa usiku mnene Dar

Joseverest

JF-Expert Member
Joined
Sep 25, 2013
Posts
52,812
Reaction score
71,392
JOTO la mpambano wa Ligi Kuu Bara baina ya Yanga na Simba utakaopigwa Jumamosi Aprili 30, 2022 saa 11 jioni wiki hii katika Uwanja wa Mkapa linazidi kupanda.

Hii sio tu kwa mabosi wa timu hizo, ila hata mashabiki wao.

Lakini kuna tukio kubwa lililojiri jijini Dar es Salaam jana usiku. Vigogo wa waamuzi na Bodi ya Ligi walikutana kuchekecha majina matano kupata moja la refa atakayesimama katikati Jumamosi.

Ni mchezo mgumu na wenye ushindani wa aina yake ambao tangu jana Simba na Yanga zimekuwa na hamu ya kujua nani atakuwa mwamuzi wa kati na hata wale wa pembeni.

Licha ya kwamba viongozi hao wa waamuzi wanafanya siri kubwa lakini habari za uhakika ambazo Mwanaspoti inazo ni kwamba mpaka wanaanza kikao jana mezani kulikuwa na majina matano.

Lakini kuna wawili wanaopewa nafasi kubwa, Elly Sasii na Abdalah Mwinyimkuu.

Sasii aliamuru kwenye mchezo wa mzunguko wa kwanza Desemba 11 wakati timu hizo zikitoka suluhu Simba akiwa mwenyeji.

Mwinyimkuu yeye anatoka Singida naye yupo kwenye orodha akipewa nafasi kubwa. Wengine ni Hance Mabena, Emmanuel Mwandembwa na Abel William ambae moja ya mchezo alioamua ni ule ya Namungo na Yanga kule Ilulu, Lindi.

Hata hivyo chanzo cha kuaminika kilieleza licha ya waamuzi hao kupewa asilimia kubwa ya mmoja wao kupewa nafasi ya kuchezesha kikao cha kamati ya waamuzi ndicho kitaamua lakini ni nadra kuwa na sapraizi nje ya hapo. “Kikao cha Kamati ya Waamuzi kitakutana na Jumatano (kesho) watangaze,”kilidokeza chanzo chetu cha kuaminika ndani ya waamuzi hao ingawa viongozi jana walikuwa wanarushiana mzigo juu ya nani atapewa hukumu hiyo.

“Safari hii kumekuwa na mvutano mkubwa wa nani atakayeamua mchezo huu kama unavyojua timu zetu na soka letu lilivyo ndani yake kuna mambo mengi.”

Hata hivyo katika michezo mitano iliyopita ya Ligi Kuu Bara zilipokutana timu hizo hakuna mwamuzi aliyechezesha dabi zote mbili za msimu au kujirudia, japo lolote linaweza kujitokeza msimu huu kutokana na changamoto za waamuzi na ushindani uliopo.

Chanzo: Mwananchi

SOMA PIA: Mwamuzi Ramadhani Kayoko kuwa 'Pilato' mechi ya Yanga vs Simba
 
Yule refa mwanamama huwaga yupo poa sana, jina nimemsahau
 
To be honesty mimi kama shabiki yani sina hata chembe ya wazo kuhusiana na Derby
Kusingekuwa na gap kubwa ya point usingeongea hivi. Mmeshakata tamaa ya ubingwa hivyo mechi derby haina faida tena
 
naona story yanga akimfunga simba na si simba akimfunga yanga kwasasa
 
naona story yanga akimfunga simba na si simba akimfunga yanga kwasasa
Kufungwa kwa Simba ni kawaida msimu huu kaishafungwa sana hivyo kufungwa kwa Simba haitokuwa ishu. Ila Yanga ndiye mwenye unbeaten run hivyo inasubiriwa kwa hamu kujua ni nani atakayekuwa wa kwanza kumfunga yanga kwenye ligi kuu msimu huu maana timu zilizotegemea kuiangusha zimeshindwa hadi sasa
 
Mashabiki wa simba hatuna presha yoyote na hakuna joto lilopanda.. wenye presha na huu mchezo ni uto..... Sisi pressure ilishia Kule kwa wazuru.. kwa wakubwa wenzetu..
 
Mashabiki wa simba hatuna presha yoyote na hakuna joto lilipanda.. wenye presha na huu mchezo ni uto..... Sisi pressure ilishia Kule kwa wazuru.. kwa wakubwa wenzetu..
Sasa huku mmefuata nini si mngebaki huko huko kwa wakubwa wenzenu
 
To be honesty mimi kama shabiki yani sina hata chembe ya wazo kuhusiana na Derby
Na mimi kama mshabiki wa Simba sina pressure ya match hii kwa sababu kuu 2.

1 tayari timu yangu tayari ina tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa (CAF).

2 Timu yangu ya Simba Sc tayari imeshaingiza kiwango cha pesa kinachozidi mshindi wa ligi kuu ya NBC.
 
Na mimi kama mshabiki wa Simba sina pressure ya match hii kwa sababu kuu 2.

1 tayari timu yangu tayari ina tiketi ya kushiriki mashindano ya kimataifa (CAF).

2 Timu yangu ya Simba Sc tayari imeshaingiza kiwango cha pesa kinachozidi mshindi wa ligi kuu ya NBC.
Unaongea hivyo kwavile timu zilizopo chini ya Simba kamavile Azam hazina muelekeo laasivyo nafasi ya pili mngeitafuta kwa tochi. Mfano Simba ikipoteza kwa Yanga na Azam akashinda mechi yake, kutakuwa na gap ya point 10 baina ya Simba na Azam
 
Back
Top Bottom