OKW BOBAN SUNZU
Platinum Member
- Aug 24, 2011
- 53,868
- 121,001
Florentina Zabron nje miezi 6
Mwamuzi Florentina Zabron ameondoshwa kwenye ratiba za michezo ya Ligi Kuu kwa kipindi cha miezi 6 ijayo kutokana na kuionea Klabu ya Geita Gold ilipocheza na Yanga SC pale CCM Kirumba Mwanza.
My Take
Kumekuwa na tetesi za Utopolo kuwawezesha marefa wanaofungiwa kwa ajili yao. PCCB fanyieni kazi.
=======
Mwamuzi Florentina Zabron amesimamishwa kwenye ratiba ya kuchezesha michezo ya Ligi kuu kwa kipindi cha miezi 6 ijayo na TFF kutokana na kushindwa kumudu mechi kati ya Geita Gold dhidi ya Yanga.
Mechi hiyo ambayo ilipigwa katika uwanja wa CCM Kirumba Mwanza huku Geita wakiwa ni wenyeji wa mchezo huo ambapo Florentina aliionea timu hiyo ya Geita kwa kuwapa penati klabu ya Yanga kwa kutafsiri kuwa mchezaji wa timu pinzani alishika mpira kwa mkono.
Lakini baada ya Bodi kukaa na kujidhihirisha na kuona kuwa mchezaji huyo wa Wachimba madini alikuwa nje ya boksi hivyo haikustahili kuwa penati, na baada ya hapo mwamuzi huyo atakuwa nje miezi sita.
Tukio hilo lilizua taharuki kwa mashabiki na wapenzi wa mpira kwa kuona kuwa Florentina hakuwa sahihi na maamuzi yake na penati hiyo ilipelekea Yanga kupata pointi 3 baada ya kushinda kwa bao 1-0.
Matukio haya yanajirudia sana hapa Tanzania hasa timu ndogo zinapocheza dhidi ya kubwa huwa waamuzi wanakosa umakini kitu ambacho mechi huisha kwa timu ndogo kuonewa kutokana na matokeo hayo
Tanzaniaweb.