WATU WANAOFAA UWAWEKE KAMA REFEREES KWENYE CV YAKO WAKATI WA MAOMBI YA KAZI
Uchaguaji wa referee hutegemea na kiwango chako cha uzoefu, yaani kama umewahi fanya kazi sehemu nyengine ama hujawahi bali umetoka tu chuo.
MAMBO YA JUMLA YA KUZINGATIA:
1. Unaemuweka lazima awe anakufahamu vizuri
2. Referee wa kazi huwa ni mtu wa kiofisi ama kijamii na sio kindugu kwa maana kuwa hushauriwi kuweka ndugu yako.
A. IWAPO NDIO UMEMALIZA TU CHUO REFEREE WEKA HAWA WAFUATAO:
1. Mmoja kutoka uliposoma
2. Mmoja kutoka ulipofanya field
3. Mmoja kutoka katika nafasi za kijamii ama kiserekali anaekufahamu vizuri.
B. IWAPO UMEWAHI FANYA KAZI SEHEMU BASI WEKA REFEREE WAFUATAO:
1. Mmoja kutoka kazi yako ya mwisho
2. Mmoja kutoka kazi ya kabla yake kama hakuna basi weka wa field
3. Mmoja kutoka ulipofanya field kama namba mbili hapo juu umeweka wa kazi ya kabla ama mtu wa nafasi ya kijamii anaekufahamu vizuri kama namba mbili hapo juu umeweka wa field.
TANBIHI
Ila kwa soko la ajira lilivyo gumu wengi nafasi za referees hawana hivyo inashauriwa kujijengea mazingira tu ya mtu ataekuwa tayari kutoa comment nzuri kwako.
KWA UZOEFU WANGU:
Cha kushangaza 90% ya kazi nilizowahi ajiriwa nazo referees wangu hawakuwahi kupigiwa simu so sijui kama wengi wa referees hupigiwa ama la ila ukiwa unajuana na watu wakubwa wakubwa na ukawaweka kwa CV inakujengea mazingira ya kupata nafasi kwa haraka.
Huo ndio mchango wangu wengine wataongezea.