Lycaon pictus
JF-Expert Member
- Jan 31, 2021
- 9,189
- 16,128
Baada ya vita kali toka mwaka 2013 hatimaye refinery ya Dangote imeanza kazi. Mwaka 2013 Dangote alitangaza kujenga kiwanda cha kusafisha mafuta. Gavana wa jimbo alilotaka kujenga akataka rushwa, ikabidi ahamishie kiwanda huko Lagos. Kimeanza kujengwa mwaka 2016 na kukamilika 2023-2024 kwa gharama ya jumla USD 20B. Refinery hiyo iliambatana na kujenga bomba la mafuta la zaidi ya kilomita elfu moja na bandari.
Refinery ya Dangote ni ya saba kwa ukubwa duniani. Inauwezo wa kuchakata mapipa laki sita na nusu kwa siku. Inauwezo wa kutosheleza mahitaji yote ya mafuta ya Nigeria na kuwa na ziada ya kuuza nje. Refinery hiyo itazalisha petrol, diesel, mafuta ya taa, mafuta ya ndege, lami na mali ghafi za kutengenezea plastics. Pia watapokea na gesi ambayo wataitumia kuzalisha mbolea na umeme wa kiwandani.
Kazi ya kujenga refinery hii imekuwa na vikwazo sana. Hasa kutoka kwa wanaijeria wenzake. Nigeria ni nchi ya kwanza kwa uzalishaji wa mafuta Africa. Lakini pamoja na hayo ilikuwa inaagiza kutoka nje mahitaji yake yote ya mafuta. Refineries nne za serikali zilikuwa hazifanyi kazi huku zikiwa zimekula pesa nyingi sana za matengenezo.
Kwenye hii dili ya kuagiza mafuta nje watu wengi sana walitajirika maana shirika la serikali ndilo lilikuwa linafanya hiyo kazi. Hawa ndiyo walikuwa kikwazo kikubwa kwa Dangote. Hawakujali kwamba nchi inatumia asiimia 40 ya fedha zake za kigeni kuagiza mafuta, walichojali ni wao kuwa matajiri wa kutupwa. Walianza kumuwekea kauzibe kwenye kumuuzia mafuta ghafi, mara wakaanza kumshutumu kutaka kuhodhi uchumi na karibuni walimshutumu kuwa mafuta yake si bora, jambo aliloonyesha hadharani kuwa mafuta yake ni bora kuliko hata yanayoagizwa.
Kikwazo kingine alichopata ni kutoka mashirika ya mafuta ya kimataifa. Hao ndiyo wenye visima Nigeria na ndiyo wamiliki wa refineries za Ulaya zilizokuwa zinawauzia Nigeria mafuta yaliyochakatwa. Hawa wamempiga vita kwa kujaribu kugoma kumuuzia mafuta ghafi. Kwenye mahojiano na Bloomberg Dangote alisema kuwa hakujua kuwa Cartel wa mafuta duniani wana nguvu kuliko wale wa dawa za kulevya.
Refinery ya Dangote itanunua mafuta kwa Naira na kuyauza kwa Naira. Jambo hili litapaisha sana litaipaisha sana Naira inayoporomoka kwa kasi.
Refinery ya Dangote imeanza kuingiza mafuta mtaani na inategemea mwishoni mwa mwaka kuwa at full capacity. Huu ni ushindi kwa waafrika, hasa dhidi ya waafrika wenzetu wajali matumbo yao tu.