Reforms wanazozitaka Chadema ni ngumu kiasi gani mpaka zisifanyiwe kazi? Mbona Reforms ni sehemu ya "4R" za Rais Samia lakini CCM wanapinga?

Reforms wanazozitaka Chadema ni ngumu kiasi gani mpaka zisifanyiwe kazi? Mbona Reforms ni sehemu ya "4R" za Rais Samia lakini CCM wanapinga?

JokaKuu

Platinum Member
Joined
Jul 31, 2006
Posts
38,298
Reaction score
72,863
Hili ni swali ambalo najiuliza.

Kama 4R ni falsafa ya Raisi, kwanini chama chake kinapinga Reforms zinazopendekezwa na wapinzani?

Badala ya kuchangamsha bongo zao namna ya kuyachukua mapendekezo ya Chadema, nguvu kubwa zaidi imeelekezwa katika kuwabeza, kuwatukana, kuwatisha, na kuwakatisha tamaa.

Shida iko wapi katika Reforms wanazopendekeza Chadema?
 
Ungemueleza mwenye kifua kipana mtoto waukweni 4R alizotumia serilikali za mitaa kupitia TAMISEMI zilikuwa za Ukweni kizimkazi tuanze hapo.
 
Reforms za Chadema zinatishia maslahi yao na uhai wao kisiasa, Kwa kuwa wanajua tume ikifanyiwa mabadiliko na ukaja uchaguzi huru na hakika ndo mwisho wao na hawako tayari ndo maana wanaleta figisu figisu nyingi
 
Wakigomea Reforms kwenye mfumo wa Uchaguzi CHADEMA ianzishe Oparesheni PIGA MWIZI WA KURA ili hii Tume FEKI tuipopoe mawe kila tunapowaona na Maboksi ya kura zao FEKI.
 
CCM wanaitawala Tanzania kijeshi hawako tayari kutoka madarakani kwa style ya vikaratasi
Ndiyo maana drama ndiyo mtaji wao
 
Reforms za Chadema zinatishia maslahi yao na uhai wao kisiasa, Kwa kuwa wanajua tume ikifanyiwa mabadiliko na ukaja uchaguzi huru na hakika ndo mwisho wao na hawako tayari ndo maana wanaleta figisu figisu nyingi

..CCM ina mtaji mkubwa wa fedha na wanachama hivyo kitaendelea ku-dominate siasa za Tanzania kwa muda mrefu. Siamini kama wataporomoka kwasababu ya Reforms katika mifumo yetu ya uchaguzi.
 
KANU pia walikuwa wakisema hivyo na UNIP.

..siasa za Kenya ni tofauti sana na Tanzania.

..Kenya unacheza na namba za kura za makabila makubwa mchezo unakuwa umekwisha.

..siasa za Tanzania zinahitaji upate kura kila mahali, ukabila hauna nguvu.
 
..hili ni swali ambalo najiuliza.

..Kama 4R ni falsafa ya Raisi, kwanini chama chake kinapinga Reforms zinazopendekezwa na wapinzani?

..badala ya kuchangamsha bongo zao namna ya kuyachukua mapendekezo ya Chadema, nguvu kubwa zaidi imeelekezwa katika kuwabeza, kuwatukana, kuwatisha, na kuwakatisha tamaa.

..Shinda iko wapi katika Reforms wanazopendekeza Chadema?
CCM hawawezi kukubali maana wanajua CCM igaanguka chap
 
..siasa za Kenya ni tofauti sana na Tanzania.

..Kenya unacheza na namba za kura za makabila makubwa mchezo unakuwa umekwisha.

..siasa za Tanzania zinahitaji upate kura kila mahali, ukabila hauna nguvu.
Chiluba na Kaunda?
 
Chiluba na Kaunda?

..Zambia walikuwa na strong labour movement katika ukanda wa shaba.

..bahati mbaya uchaguzi wa vyama vingi Zambia ulifanyika kipindi ukanda wa shaba una matatizo makubwa ktk mauzo na uzalishaji.

..mazingira hayo ndio yaliyopelekea Chiluba mtu aliyekuwa katika Labour movement kushinda uchaguzi.
 
..CCM ina mtaji mkubwa wa fedha na wanachama hivyo kitaendelea ku-dominate siasa za Tanzania kwa muda mrefu. Siamini kama wataporomoka kwasababu ya Reforms katika mifumo yetu ya uchaguzi.
Nje ya madaraka , CCM itayumba , ndo maana hawako tayari kuachia, wanajua wakiachia madaraka ndo mwisho wa era yao
 
Back
Top Bottom