Rejea kifo cha wazazi wa Anna: Maisha hayana maana kama hakuna kifo

Rejea kifo cha wazazi wa Anna: Maisha hayana maana kama hakuna kifo

Da'Vinci

JF-Expert Member
Joined
Dec 1, 2016
Posts
36,444
Reaction score
110,233
Salute:
pexels-photo-551590.jpeg


Siku ya jana ilikua majonzi kwa binti Anna Zambi na watanzania wote wenye mioyo ya huruma
na utu, kwake Anna ilikua ndio siku mbaya zaidi kuliko zote alizowahi ishi hapa duniani.

Wapo walionguna nae kwa kilio, wapo walioungana kwa maombi na kumtakia heri katika safari yake mpya hiyo ya maisha pasipo wazazi.

Wengine walienda mbali zaidi kwa kutoa maneno makali, kufuru kwa Mungu kutokana na tukio hilo lililomtokeaa binti huyu mdogo "Kwanini huyu Mungu hajaziwia vifo hivyo hadi anamuacha mtoto mdogo pekee katika dunia hii yenye taabu"

Wengine wamemchukulia labda huyo Mungu ni kitu kisichokuwa na huruma kwa viumbe wake.

Ni baadhi tu ya maneno watu waliyokuwa wanasema hata humu jamvini. Sio kosa lao maana hicho ndicho kinachotokea kwa binaaadamu pale jambo kama hili linapotokea "Hisia zikiteka kichwa kufikiria hua hakupo" ila kwa upande wangu katika familia ile kifo ilikuwa ni halali yao kabisa, msinielewe vibaya hata mimi nina soft heart made up with tissues. Inaniuma pia.

Baadhi ya watu wanamlaumu baba wa familia ambae alikua ndio kiongozi wa safari ile kuruhusu kuendelea na safari wakati wanaona kabisa hali sio mbaya, ukweli kabisa baba huyo hana makosa kabisa katika hilo. Kwanza kabisa tuelewe kuwa kila kitu kimeumbwa katika hili ya msawazo, kila kitu kina kinyume chake duniani hapa.

Uhai una kifo, Mungu ana shetani, Moto
una maji, kushoto kuna kulia, Kuna mbingu na ardhi, afya na magonjwa mwanaume na
mwanamke nk.

Kwenye kuishi kuna kifo those things goes paralell ili ufe lazima uishi na ili uishi lazima ufe kifo ni hatma na haki ya binaadamu yoyote yule anayeishi and nobody can escape his/her Destiny labda itokee neema tu.

Thats is the law of nature and you cant change the law of nature if you do that expect Great Concequences to haunt you. Kwa mantiki hiyo ile siku ilipotokea ajali katika famlia hiyo ndio ilikua siku ya hatima yao ya mwisho (Final Destination) hata
wangefanyaje siku ile ilikua tu ni lazima watu wale tamati yao ifikie.

Kama sku ile isingewatokea pale kwenye mafuriko basi hata sehemu nyingine ingewakuta! Kibinaadamu ni ngumu kidogo
kuelewa haya mambo yanavyo operate.

Kama siku yako imefika huwezi kimbia kifo na kama haijafika unaweza ukaokoka kifo katika njia ya ajabu hadi ukabaki huamini mfano..m

Mwaka 2017 mwezi wa 4 Zanzibar kunatukio lilitokea na mwenyewe nililishuhudia.Kuna sehemu kunaitwa fuoni ukinyosha barabara ya kwenda huko fuoni inaelekea mpaka mkoa wa mjini magharibi kisha inakunja kueleka maeneo ya Kizimkaazi,paje,jambiani,makunduchi nk nk
sasa huko fuoni kuna sehemu kuna kama bonde hivi barabarani mvua ikinyesha panakua na mafuriko. Siku hiyo pakawa na mafuriko dereva wa vespa kapita pale kasombwa na maji, kulikua na gari la chuo cha kiislamu limebeba wanafunzi wakati limevuka pale dereva akamuona yule mtu akiwa anasombwa na maji anajishikiza kwenye majani, dereva wa gari
akasimamaakaenda kumsaidia yule mtu..alifanikisha kumtoa lakini maji yalemchukua yule
dereva wa basi akafariki! sasa umeona kama siku yako haijafika kamwe huwezi kufa.

Kwanini Mungu hakuwalinda wasife?
Kwanza Mungu hahusiki na kifo chako, As i always say Time ndio sababu tunakufa.

Mungu alishafanya uumbaji wa kila kitu, kila kitu kakiwekea jinsi kitakavyo jiendesha chenyewe yeye kazi yake ni kusimamia yale aliyoyaumba yaende kama yanavyotakiwa kwenda, unajua Mungu haamui jinsi ya wewe utakavyo kufa!

Mungu kaupa Muda na Nature kuamua kifo chako. Ipo hivi Time yenyewe inakua inajua muda fulani Mtu fulani Inatikiwa afariki so ule muda ukishawadia.

Time inawasiliana na nature, Nature yenyewe ndio inaamua baada ya muda wako kufika ufariki either kwa
magonjwa, ajali, kuuwawa nk.

Mungu hawezi kuingilia hizo shughuli maana kashawaachia Control, labda itokee akuongezee muda tu au aamue yeye vyovyote yeye anavyoona inafaa.

So kwa familia ya Anna inaonekana muda wao ndio ulikua umewadia, ilikuwa lazima siku ile waondoke na hata kama pale wangepona basi lingetokea lolote lile ili mradi tu hatima yao ifike.

Kwanini Mungu kaichukua familia ya Anna wakati bado ni mdogo na anahitaji wazazi wake?
Kama nilivyosema muda wako ukifika umefika tu! haijalishi akina nani wako nyuma yako
wanakutegemea.

Wazazi wa Anna wameondoka wamemwacha pekee hana msaada wa kutosha kama ilivyokua mwanzo.

Kwenye mambo ya kiroho tunaamini hakuna Hasara isiyo na faida. Ili upate faida kubwa lazima upoteze vitu vya thamani kwako.

Hata wewe binafsi ukijiangalia ulipotoka na ulipo hali yako kuna vitu ulipoteza vya muhimu ndio ukafikia mafanikio haya uliyonayo leo. nitoe mifano kidogo. Yusufu alipoteza familia yake akauzwa misri lakini huko alitokea akawa mtu mkubwa na kusaidia familia yake.

Naomi alipoteza watoto na mumewe lakini
kwa kupitia mkwewe Ruthu aliweza kupa mjukuu aliyekuja kuwa kipenzi cha Mungu (Daudi), Ayubu alipoteza Familia na mali zake zote bila kusahau afya yake lakini baadae alikuja kuwa mtu mkubwa na tajiri katika familia yake, ili kueneza imani ya uislamu ilibidi Mohamad apoteze meno na alikuja fanikiwa.

Mitume na maswahaba walipoteza Uhai ili kuleta faida kwetu, Yesu ilibidi apoteze uhai ili kutuleta uzima, ilimghalimu uhai Socrates na Galileo ili kubakiza ideas zao
duniani nk nk.

Newton's 3rd Law of motion inasema "For every action there is an equal and opposite Reaction" Akimaanisha kwamba kwa kila kitendo tunachofanya basi kutatokea Muitikio kama huo au ukatokea muitikio (MATOKEO) ulio kinyume na tendo hilo.

Kama wazazi wa Anna wamemuacha hana masaada wa kutosha basi tutegemee Mambo mazuri mengi katika maisha ya binti huyo siku za baadae.

Kupitia tukio hili Binti huyu anaweza kupata mambo mengi ya mafanikio katika maisha yake. kila kitu kinachotokea kwenye maisha yetu kinatokea kwa sababu na kinakuja na faida zake. Ili upate ngano inabidi ipigwe pigwe, ili dhahabu ipatikane inabidi ipaite motoni, ili upate mafanikio lazima upate mateso ya kimwili na kiroho.

Kwa upande wake Anna ya kutokea yametokea na yalitakiwa yatokee, cha msingi walio karibu nae wamliwaze na kumpatia tiba ya akili (Psychotherapy) ili Post-Traumatic Stress Disorder isije
kumkumba nae tukampoteza kimwili au kiakili.

Yaliyotokea yametokea, Kifo ilikua ni halali yao nasi pia na halali yetu. Maisha hayana maana pasipokua na Kifo. ili tuishi lazima tufe. Mungu yupo nawe Na naamini Mambo mengi mazuri yanakujia muda sio mrefu.

Be Blessed Anne. Good things are coming
Rest in Heaven Survivors and other little angels.
~Vers.
Mshana Jr mchango wako muhimu.
The End.
Ciao.

#UPDATES
Kwa amabao hamjaelewa paragraph ya mwisho.."Rest in Heaven Survivors"
Survivors ni wahanga wa tukio fulani..
So nimewaita hao wazazi wa Anne survivors kwakua Duniani humu wote tunapambana ili tu survive to the fittest, So wote hao ni wahanga wa kupambana katika maisha
 
Umelezezea kiufasaha na kiswahili safi sana.Tuliokuwa tukitoka machozi,kuhusu hili tukio,umetufuta machozi na umetuliwaza kiasi kikubwa.Ujumbe umefika kwa sisi walengwa,sijui mlengwa mkuu,kama umemfikia.Shukrani sana.
Pamoja sana ndio ilikua lengo langu
 
Nje ya mada kidogo.

Hivi huyu Ni ndugu wa Godfrey Zambi alikua mbunge au waziri kama kumbukumbu zangu ziko sawa
 
Hakika binti huyu atapata mengi sana kama misaada ya kifedha malazi na chakula, lakini ndugu mwandishi hawezi tena pata upendo ule wa wazazi na ndugu zake ambao ni muhimu sana, alikua anatamani wazazi wake waone mafanikio yake na aje awafanyie suprise wazazi na wadogo zake, msaada wa kifedha ni muhimu sana kwake lakini hauwezi replace hata robo ya kilichopotea.hivo hakika anapigo kubwa sana. Mungu amtie nguvu
 
Back
Top Bottom