Rekodi kabambe alizoweka Rais Samia kwa watumishi wa umma Tanzania

Rekodi kabambe alizoweka Rais Samia kwa watumishi wa umma Tanzania

Zack Abdul

JF-Expert Member
Joined
Mar 9, 2026
Posts
1,194
Reaction score
911
Nyongeza ya mishahara iliyovunja rekodi ya 35.1% na 23.3% baada ya kuondolewa miaka 6 na ajira mpya 96,000, kupunguza kodi ya mshahara (PAYE), kupandisha vyeo watumishi 631,000, kulipa madeni, malimbikizo zaidi ya Trilioni 1.

Na Bwanku M Bwanku.

Leo Jumanne kwenye Gazeti la Uhuru ukurasa wa 12, Ndugu Bwanku M Bwanku amechambua mageuzi makubwa yaliyofanywa na Serikali ya Rais Samia kwenye Utumishi wa umma ili Watanzania wapate huduma bora ikiwemo nyongeza ya mishahara iliyoweka rekodi ya 35.1%, 23.3%, ajira mpya zaidi ya 96,000, kupunguza kodi kwenye mishahara ya watumishi (PAYE) na kupandisha madaraja watumishi zaidi ya 631,000, kulipa malimbikizo ya mishahara, madeni na mengine mengi.

Licha ya majanga makubwa ya Dunia kama Corona, vita zilizovuruga uchumi kama ile ya Urusi na Ukraine, Marekani na Israel dhidi ya Iran na kusababisha uchumi sehemu kubwa ya Dunia kushuka hadi Mataifa mengine kushindwa kulipa mishahara, Tanzania imeendelea kulipa na kuboresha maslahi ya watumishi na wafanyakazi ili Watanzania waendelee kupata huduma bora kila mahali. Soma makala hii kwenye Gazeti la Uhuru uone mageuzi haya.
IMG-20261013-WA0066.jpg
 
Back
Top Bottom