Rekodi ya Kibadeni kwenye derby ya Kariakoo ipo rehani

Gwele

JF-Expert Member
Joined
Jun 7, 2016
Posts
2,604
Reaction score
3,319
Ni ukweli usiopingika kuwa kufunga magoli matatu yaani Hat trick kwa mchezaji mmoja katika mechi ya watani wa jadi yaani Simba na Yanga ni jambo gumu sana na ni rekodi ya aina yake.

Hata hivyo rekodi hiyo mpaka sasa inashikiliwa na mchezaji mmoja pekee,Abdala King Kibadeni aliyefany hivyo mnamo Julai 19, mwaka 1977 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa Uwanja wa Uhuru, wakati Yanga ilipotandikwa 6-0 na Simba.

Siku hiyo, Kibadeni alitikisa nyavu za Yanga katika dakika za 10, 42 na 89, wakati mabao mengine ya Wekundu wa Msimbazi, yalitiwa kimiani na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 na jingine Selemani Sanga wa Yanga alijifunga mwenyewe dakika ya 20 katika harakati za kuokoa krosi ya Ezekiel Greyson 'Jujuman'.

Rekodi hii ya Kibadeni iliyodumu kwa miaka mingi sasa huenda ikafikia ukomo hapo tar 16 April 2023 kwa mshambuliaji Hatari zaidi kwa sasa ndani ya Ligi kuu Tanzania Bara,Jean Bakeke atakapotikisa nyavu za Yanga mara 3 na kuandika rekodi mpya ya kuwa mwanadamu wa pili kufanya hivyo baada ya mwanasimba mwengine kufanya hivyo mwaka 1977.

Rekodi hii si rahisi kuivunja ukizingatia kwa kipindi chote hicho toka 1977 Simba na Yanga wamepita washambuliaji wengi hatari lakini hawakuweza kuivunja rekodi hiyo na sasa ni wazi Jean Baleke (Jini) anaenda kuonyesha utofauti wake na washambuliaji waliowahi kupita kwenye vilabu hivyo vikongwe kwa kuitamatisha rekod ya King Kibadeni Mputa na nina imani hata yeye atafurahi hili jambo likitokea wakati huu akiwa hai
 
Hapa wala mihogo sasa ni vijampo tu na harufu za vinyesi kwenye vyupi vyao kama walivyofanya Kule Arusha dhidi ya costal .
 
Alishindwa Okwi itakuwa Baleke.
Simba akishinda 5 -0
Okwi mbili. 2
Kaseja.
Mafisango.
Sunzu.
 
Kipimo sahihi kwangu Binafsi ni MICHEZO mi nne ijayo.
Kwa Baleke.

Yanga.
Azam.
Wydad.
Whydad.

Katika hii MICHEZO akifunga MAGOLI 3 hapo ndipo nitasema ni mshambuliaji mwenye uwezo.

Kwa sasa nisiseme nikamaliza
Kwa hiyo kwa sasa hivi hana uwezo?
 
Tar 16 sio mbali mtayakataa maneno yenu mnadhani YANGA ni sawa na hizo team mdebwedo mnazofunga ee
 
Ohooo, mwamba unataka kumharibia kijana wa watu sasa! Ukimsifia kijana na mafanikio yake mbele ya wanga wa kitaa (Uto) wanaingia mzigoni mara moja kumroga. Naogopa yasije kutokea ya Phiri,Okrah,n.k. Witchcraft is real.
 
Ni Mayele again,what a goal. Hizi kelele mtazisikia sana
 
Wa kupimwa wewe..!!
 
Alishindwa Okwi itakuwa Baleke.
Simba akishinda 5 -0
Okwi mbili. 2
Kaseja.
Mafisango.
Sunzu.
Kwa nini wanaotajwa kushindana kuvunja hiyo rekodi ni wachezaji wa Simba tu, kwani Mayele wa Yanga hawezi kuivunja?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…