Rekodi ya Kibadeni kwenye derby ya Kariakoo ipo rehani

Rekodi ya Kibadeni kwenye derby ya Kariakoo ipo rehani

Kinacho muhusisha Baleke hapo ni uwezo wake mkubwa wa kufunga Hat trick na kulifanya lionekane jambo rahisi tu na ndio maana kwenye mechi 06 za mwisho huyo mwamba ana Hat trick mbili
vs timu gani
 
Mimi Ni mwananchi lkn Kuna wachezaji wa Simba nilikua nawakubali Kama King Kibaden, Tanzania one na Golden boy Zamoyoni.
 
Ni ukweli usiopingika kuwa kufunga magoli matatu yaani Hat trick kwa mchezaji mmoja katika mechi ya watani wa jadi yaani Simba na Yanga ni jambo gumu sana na ni rekodi ya aina yake.

Hata hivyo rekodi hiyo mpaka sasa inashikiliwa na mchezaji mmoja pekee,Abdala King Kibadeni aliyefany hivyo mnamo Julai 19, mwaka 1977 katika Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam, sasa Uwanja wa Uhuru, wakati Yanga ilipotandikwa 6-0 na Simba.

Siku hiyo, Kibadeni alitikisa nyavu za Yanga katika dakika za 10, 42 na 89, wakati mabao mengine ya Wekundu wa Msimbazi, yalitiwa kimiani na Jumanne Hassan 'Masimenti' dakika ya 60 na 73 na jingine Selemani Sanga wa Yanga alijifunga mwenyewe dakika ya 20 katika harakati za kuokoa krosi ya Ezekiel Greyson 'Jujuman'.

Rekodi hii ya Kibadeni iliyodumu kwa miaka mingi sasa huenda ikafikia ukomo hapo tar 16 April 2023 kwa mshambuliaji Hatari zaidi kwa sasa ndani ya Ligi kuu Tanzania Bara,Jean Bakeke atakapotikisa nyavu za Yanga mara 3 na kuandika rekodi mpya ya kuwa mwanadamu wa pili kufanya hivyo baada ya mwanasimba mwengine kufanya hivyo mwaka 1977.

Rekodi hii si rahisi kuivunja ukizingatia kwa kipindi chote hicho toka 1977 Simba na Yanga wamepita washambuliaji wengi hatari lakini hawakuweza kuivunja rekodi hiyo na sasa ni wazi Jean Baleke (Jini) anaenda kuonyesha utofauti wake na washambuliaji waliowahi kupita kwenye vilabu hivyo vikongwe kwa kuitamatisha rekod ya King Kibadeni Mputa na nina imani hata yeye atafurahi hili jambo likitokea wakati huu akiwa hai
Akishinda kwenye mechi hiyo moderators naombeni ban tafadhali
 
sasa tukianzia hapo hapo ulipoandika mayele aliyewahi funga goli mbili dhidi ya simba na beleke ambaye hakuwahi kucheza kabisa hiyo mechi nani wa kumpa credit iyo...yani uhusiao wa beleke kufunga hatrik unatokea wapi kama yule aliyewahi kufunga goli mbili ktk iyo mechi hawezi kuhusiana na goli tatu
Kibadeni alipoipata ilikuwa ni mechi yake ya kwanza, hakuwahi kucheza kabla.
 
Mimi Ni mwananchi lkn Kuna wachezaji wa Simba nilikua nawakubali Kama King Kibaden, Tanzania one na Golden boy Zamoyoni.
Na sasa hivi Mwamba Jean Baleke nae lazima ukiri tu kuwa unamkubali au nakosea mkuu?
 
Kibadeni alipoipata ilikuwa ni mechi yake ya kwanza, hakuwahi kucheza kabla.
Ni bora umemuweka sawa mkuu huyu jamaa anafikiri kwakuwa Mayele aliwahi funga mawili kwenye mechi ya derby huko nyuma basi amebakisha kufunga moja kuipata Hattrick hajui kuwa hii mechi inaanza kivingne na Baleke anaweka rekodi yake mpya
 
Haya sasa leo ndio leo masaa mawili tu yamebaki Baleke kuweka Hat Trick yake ya kwanza kwenye Derby ya Kariakoo
 
Back
Top Bottom