Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Wengi wetu tumefaulu Sana Ila katika maisha network na social intelligence ndio muhimu zaidi.

Kuusoma Mtaa na kujua unahitaji na ni vipi ujamiane na watu Kwa ajili ya kupata pesa.

Mimi na marafiki zangu wengi tuliokuwa tunafanya vizuri darasani .

Tupo hatua Fulani ya maisha Ila kuna jamaa yeye alikuwa darasani hayupo vizuri Sana Ila Leo hii yeye safari za ulaya German ,France anaend Kama unavyoenda kariakoo.

So mambo mengi ni swala la chance and opportunity, efforts plus GOD and nothing else.

Naamini connection utapata na mambo yatabadilika kuanzia sasa
 
Miaka 27 bado mkuu! Wengine tumepata kazi serikalini tukiwa above 30 yrs! Wengi wanajichanganya kwenye kuchagua course mavyuoni, kwa ufaulu wako ungekuwa umesomea course zingine mfano civil, mechanical, Electrical, IT hizo course hata usipoajiriwa na serikali huwezi kulala na njaa!!

Note: mimi sio muumini wa connection toka nafanya usaili pale utumishi nimepiga saili nyingi sana mpaka nakuja kupata kazi ilikuwa nafasi moja na nikaenda nikapiga nikachukuliwa kwa hiyo usiamini kwenye connection pambana sema wewe ulichagua course zenye nafasi za ajira chache ndo maana unaangaika mkuu! Ila kuwa na subira siku yako ikifika utafidia miaka yote uliokaa mtaani
 
ELIMU sio vyeti (makaratasi) ELIMU ni maarifa /nyezo muhimu kukuwezesha kupambana na your environment na kupata matokeo chanya.

Mimi kwangu ELIMU inabakia kua confidence/ Sina excuse kulaumu kujilaumu au kulaumu nimesoma au sijasoma.

Leo hii nikiamua kuuza genge ntauza kwa utalaam wa Hali ya juu/ nikiamua kuuza maandazi na vitafunio ntajibrand na kuuza kwa kiwango cha juu.

Ukingojea ajira za serikali kwa wakati huu OMBA uwe na bahati sanaaa ama connection pesa ipo mtaani ingia street anza harakati mdogo mdogo kua guru kwenye industry utakayo amua jipe muda fanya mambo with time utakua somewhere na huto taka hizi ajira Tena .

NB.
ELIMU ni kile KINACHO BAKIA KICHWANI BAADA YA KUMALIZA KUJIFUNZA 🎓
 
Ni ushauri nzuri sana
 
Bado una Mentality ya kishule shule...ondoa kwanza iyo mentality
 
Uliwekeza kwenye kukariri mambo ya vitabu yasiyo na Tija ukasahau kuwekeza kwenye maarifa ya Maisha na connection
 
Jiajiri Mkuu kuwa na historia ya taaluma sio kigezo ufosi ajira vipi kama huna tabia nzuri pengine mlevi unakula wake za watu shisha km Aziz Stephen
 
Kwanza ondoa mentality ya ukipanga kichwani mwako, vipanga mko wengi, kila shule na kila darasa kuna vipanga, mimi mwenyewe nilikuwa A-List student enzi zangu.

Ila kwenye kufanya maamuzi ya nini nikakisomee from form 4 niliangalia zaidi kitu chenye tija mbeleni. Ushauri kutoka kwa ndugu zangu walionitangulia ilikuwa nichague arts ila nikawakacha nikachagua science. Kwenda chuo nikaikacha SUA japokuwa nilisomea kilimo advance, nikachagua afya.

Hata ww bado una nafasi ya kufanya maamuzi sahihi.

Cha kwanza ondoa mentality ya kwamba ulikuwa kipanga hivyo unapaswa "Upewe Priority". Kisha tafuta cha kufanya wakati unaendelea kutafuta ajira rasmi, na kifanye kwa bidii, utafanikiwa tu.
 
Gentleman,
fanya biashara.
kilimo biashara na ufugaji biashara ndiyo kila kitu gentleman.

ni muhimu ujuzi na maarifa yako ya elimu kubwa uliyonayo ukatumia vyema kwenye maeneo hayo ya wazi kabisa kujikwamua kwenye fedheha, unyonge na kuchakaza viatu mtaani kwa kurandaranda bila mipango 🐒
 
Ushaur dume huu hongera mkuu
 
Nikwambie tangu mwaka 2015-2024 hapo ndipo mambo yalipoanza kubadilika
Kwa uzoefu wangu

Kama unataka kazi za serikalini
Kuna makundi ya Aina Tatu mkuu haya probability
1.kuna watakao maliza Chuo na kupata kazi au Baada ya Mwaka 1 (2%)ni wachache sana
👉Vigezo wanashikiwa nafasi


👉Wanahonga aidha pesa au kwa wanawake wanahonga ngono
👉Kampuni /serikali imegundua wewe ni expert katika angle fulani sio kwamba unaenda Tena kujifunzia kazini

2.kumaliza Chuo na kupata kazi baada ya Miaka 2,3, 4, 5(70%)wapo wengi sana hili kundi kigezo ni
👉experience two years and above ndo inawabeba kutoka zile short term strategy
👉Na mengine kama twaja hapo juu

3.kumaliza Chuo na kupata kazi au kutokupata kazi kabisa baada ya miaka 6,7,8,9n.k(28% iliyobaki)
Hapa unakuta mtu Alishasahau kabisa na hana mpango wa kutembeza bahasha Ana deal na kipaji, na biashara ndogo ndogo

👉Ushauri Mtaa hautaki watu wenye moyo legelege (Simama imara) toa hiyo degree iweke pembeni
Asilimia kubwa ya watu ambao hawana ajira wanaendesha maisha yao kwa biashara usiogope kuanzia chini, usiogope kuchekwa, kama upo home hama kwenu kafanye vibarua mbali

Inakuathiri kisaikolojia sababu unalifikiria sana toka Maghetoni kajichanganye mzee (chukua Ata bajaji ya mkataba babu jifunze)
Kwa wiki hesabu unapelekea (120k kwa boss) mkataba miezi 24,26,28

Hii itakua njia rahisi ya wewe kupata mtaji! Keep it up





3.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…