Rekodi yangu bora kimasomo haijaniwezesha kupata ajira. Naathirika Kisaikolojia

Muangalie na course za kusoma. Kuna course za watu wa kishua wenye connection na za watoto wa maskini wasio na connection.

Ungesoma education au afya I hope ungekuwa umeajiriwa au uko kwenye nafasi nzuri ya kuajiriwa. Tena na hiyo pcm huko kwenye education ingekuwa zamani sana.
Mie kwa wtt wangu najikita kwenye education, afya na business
Km akiwa smart hukohuko atajitengenezea connection za maana zaidi.
Tena ualim ndio daraja zuri la kupitia unapoanza maisha
 
Kama ulianza form1 wakati shule za kata zinaanzishwa na ukasoma Enginnering geology chuo, basi itakuwa uligraduate 2014.
You are my classmate. 2014 hadi leo ni miaka 10. Bado unahaha kutafuta kazi. Utafutaji wa kazi ukiuendekeza sana utashtukia uzee huu. Hamna cha maana ulichofanya.

Ushauri wangu. Ni wakati sasa wa kupunguza au kuacha kabisa kutia effort kwenye kutafuta kazi. Anza kujitafuta wewe. Japo hata kwenye kujitafuta bado ni kwamoto lakini niamini ukitia nia, ipo siku utajipata. Nilikuwa kama wewe zamani. Mimi nimesoma mining Engineering. Zoezi la kutafuta kazi nimeabolish rasmi mwaka 2020. Saivi nashukuru am good the other way.
KILA LA KHERI MPAMBANAJI.
 
Ndiyo maana mi mtoto wangu nimempangia asome mwisho form 4 then peleka SUA akasomee KILIMO NA UFUGAJI then akiwa anaingia Degree namuanzishia duka la pembejeo akimaliza nauza viwanja viwili namfundisha kufuata madawa ya mifugo na shambani KENYA NA CHINA likiwa pumbafu shauri lake nahamia kwa mdogo ake.
KAMA UMEPENDA HUU MPANGO WANGU GONGA LIKE TWENDE WOTE
Mpango wa kipumbavu. Angalia kwanza mwelekeo wa mtoto wako na sio kumlazimisha afanye unachotaka wewe. Wazazi kama wewe ni wabinafsi wanaojijali wao tu.
 
Habari wana jukwaa. Kwa kweli hivi sasa bila connection ni ngumu kupata kazi, vinginevyo Mungu aingilie kati. Binafsi kwa neema ya M/Mungu nimefanikiwa kuwa nahistoria ya kufanya vizuri darasani, na kuwa mwanafunzi bora kuanzia nilipokuwa shule ya msingi mpaka chuo kikuu. Historia yangu kwa ufupi ipo hivi.

Primary

Ufaulu mzuri nikapangiwa kwenda sekondari, japo ni ya kata, wakati huu ndo shule za kata zimeanzishwa kwa wingi, hivyo hata wenye ufaulu mzuri walipelekwa shule hizi ili kufidia gap la wanafunzi

Sekondari

Nilifanya vizuri sana. Nimekuwa mwanafunzi namba moja darasani tangu kidato cha kwanza mpaka cha nne na nikafanikiwa kuzawadia cheti cha mwanafunzi bora na uongozi baada ya kufanya vizuri kwa miaka yote minne ya sekondari.

Nikafaulu kwa ufaulu wa daraja la kwanza, nikiwa mwanafunzi pekee darasa nzima la wanafunzi 138 mwenye daraja la kwanza na nikapangiwa kwenda Advance kwa mchepuo wa PCM (Physics, Chemistry, Advance Math)

Advance

Hapa napo sikukaa kizembe, katika darasa la wanafunzi 38, kidato cha tano na cha sita vyote nilikuwa mwanafunzi namba moja ama namba mbili kwenye mitihani ya terms na kikanda. Katika wanafunzi 38 wa PCM, wanafunzi 2 pekee tukafanikiwa kupata Div I. Hivyo moja kwa moja tukapangiwa chuo kikuu, na wote tulikwenda chuo kimoja, UDSM (University of Dar Es Salaam)

Chuo Kikuu.

Nikasomea program ya engineering (Engieering Geology), ni program ya miaka minne. Kwa ufupi hapa shule ilikuwa ngumu sana, ukijumlisha na changamoto za kifedha, lakini historia ya nyuma ya shule ilinibeba nikapata mkopo wa serikali 100%. Chuoni tulianza wanafunzi 14, lakini tuliobahatika kumaliza mpaka mwaka wa mwisho ni wanafunzi 6, na katika hao sita, ni mimi pekee nilifanikiwa kufaulu kwa kiwango cha juu kidogo ukilinganisha na wenzangu cha Second class honors, Upper division ambacho na hakika si kiwango haba kutokana na ugumu wa program husika.

Hio ndo historia yangu ya shule kwa ufupi sana, nimeelezea matokeo tuu, sijaelezea matukio. Lakini nasikitika kuona kwamba rekodi hio haijawa na mchango chanya kuniwezesha kupata kazi. Mpaka sasa kijana natangatanga, hapa na pale. Nipo wazi kufanya kazi kwenye migodi ya uchimbaji, kampuni za ujenzi wa majengo na barabara. Na kwa sasa nina leseni ya ulipuaji (blasting licence for both Open pit & Underground mining)
Hahah! Ama hakika kupata kazi zama hizi connection... Wakuu nipeni CONNECTION!! Umri ni miaka 27.
Yaani wewe jamaa umenikera sana .
Mkopo asilimia 100% ukahindwa kujiajri.

Kweli usilaumu elimu ,jilaumu wewe hapo
 
Siku Ukiingia kwenye system ya ajira ama biashara ya fani yako utasahau kama ushaandika uzi kama huu wa kulaumu. Hatima yako ni njema, endelea kukaza
 
Mpango wa kipumbavu. Angalia kwanza mwelekeo wa mtoto wako na sio kumlazimisha afanye unachotaka wewe. Wazazi kama wewe ni wabinafsi wanaojijali wao tu.
Vijana wa sasa ndio wamechanhanyikiwa hawajui hata nini wanataka
Wao wanataka maisha ya short cut na kubeti tu
Wakati mwengine mzazi inabidi uwe kabaji ndio mtt akuelewe
 
Sio vijana wote wamechanganyikiwa. Mzazi kulazimisha kutimiza ndoto zake kupitia mtoto sio sawa.
 
Mkuu kama ulivyosema kwenye haya maisha mara nyingine unaamua tu kusoma kitu flani ili mradi usije ukateseka kwenye maisha... Back in 2009 nilikua na one but niliamua tu kusoma education pale udsm ilimradi tu nisije hangaika baadae nibaki kujilaumu kwamba nilikua vizuri darasani but Leo Sina KAZI.... Sasa mtu akisikia jamaa ni teacher basi anajua huyu ni kilaza alifeli kumbe ni kuchekecha maisha...
Mkuu kwenye haya maisha sisi tunapanga na Mungu naye anapanga.

Cha msingi kwenye maisha ni kuridhika na pale ulipo, hilo ndo la msingi.

Ridhika na kile ulichojaaliwa meanwhile unaendelea kupambana, ila usiridhika unaweza kujikuta unajikatia tamaa na uharibu kila kitu.
 
Mpango wako umekaa vizuri lakini je huyo mtoto wako ana ndoto kama za kwako au unalazimisha afate ndoto zako.
Watoto wengi wa kizazi hiki hawataki kuamuliwa cha kufanya unakuta tayari ana plans zake...na kama anajitambua basi plans zake zinaeleweka.
Nimempeleka shule ina interest hizo na pia anaonesha yupo interest na pia na mimi nalima na pia nafuga so naamini atapokea ushauri
 
Kama ni hivyo kila la kheri.
 
Ndiyo maana mi mtoto wangu nimempangia asome mwisho form 4 then peleka SUA akasomee KILIMO NA UFUGAJI then akiwa anaingia Degree namuanzishia duka la pembejeo akimaliza nauza viwanja viwili namfundisha kufuata madawa ya mifugo na shambani KENYA NA CHINA likiwa pumbafu shauri lake nahamia kwa mdogo ake.
KAMA UMEPENDA HUU MPANGO WANGU GONGA LIKE TWENDE WOTE
afanye na ufugaji wa ng'ombe wa maziwa na kuku pia, akiwa maeneo ya chuga wallah hawez lala njaa
 
Back
Top Bottom