Rekodi za ukoo za kwako ni zipi?

Rekodi za ukoo za kwako ni zipi?

The Boss

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2009
Posts
49,282
Reaction score
117,244
Inachekesha lakini hii kitu ipo sana....

Unakuta kuna mtu anaheshimika mno kwenye ukoo wao...
Ukiuliza unapata majibu very interesting....

Mimi huwa naaita kuweka rekodi kwenye ukoo..lol

utakuta mtu anaheshimika kwa kuwa kwenye ukoo yeye alikuwa

1.wa kwanza kufika daresalaam.
2.kufika chuo kikuu
3.kwenda ulaya...
4kupanda ndege na kadhalika .......

Swali ni hili je wewe mwana jf kwenye ukoo wenu una rekodi gani unashikilia???????????????????lol

msione aibu hebu mje share na sisi hapa???????
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hahhaahahh....mimi kwenye zote ulizotaja siwezi kua wa kwanza!

Labda ntakua wa kwanza kusomea nlichosemea...
Kaka yangu wa kwanza kula konokono.....
 
Hahhaahahh....mimi kwenye zote ulizotaja siwezi kua wa kwanza!

Labda ntakua wa kwanza kusomea nlichosemea...

KUNA REKODI NYINGI SANA

labda we ndo wa kwanza kwenye ukoo kuwa na line tatu za simu lol

au kumiliki lap top lol

jichunguze...lol
 
babangu alikuwa mtu wa kwanza kujenga nyumba na kuezeka kwa bati kijijini kwao,mpaka leo kijiji kinaitwa kijiji cha bati
 
Hahahhahah hivyo vyote wakubwa wangu wamenipiku....Ohhhhh nimekumbuka nadhani ntakua wa kwanza kutumia hii simu yangu....
 
hongereni sana.........kwa kweli lol
 
babangu alikuwa mtu wa kwanza kujenga nyumba na kuezeka kwa bati kijijini kwao,mpaka leo kijiji kinaitwa kijiji cha bati
Mimi babu yangu alikua wa kwanza kwenye ukoo wao kuoa muislamu...
 
Hahahhahah hivyo vyote wakubwa wangu wamenipiku....Ohhhhh nimekumbuka nadhani ntakua wa kwanza kutumia hii simu yangu....

ha ha haa haaa blacberry sio???hongera saana....
 
Mimi babu yangu alikua wa kwanza kwenye ukoo wao kuoa muislamu...

umeona sasa rekodi tunazo nyingi sana...

mimi nataka niweke rekodi ya kuwa na wake watatu kwa mpigo,kwetu hakuna aliye wahi..
wengi wameishia wawili tu lol
 
Swali ni hili je wewe mwana jf kwenye ukoo wenu una rekodi gani unashikilia???????????????????lol

msione aibu hebu mje share na sisi hapa???????

Mimi nashikilia rekodi ya kufeli darasa la saba, kufeli fom foo, kufeli fom siksi na hatimaye kupata bahati ya kuja ughaibuni (kwa kutumia bank statements za Salamander) na kuwa wa kwanza katika familia kuwa mbeba maboksi.
 
si jambo dogo hilo hongera sana..
umewaonyesha na kuwapa nguvu nguvu wengine waliofeli na wataofeli kuwa
there is more to life than kufaulu shule....
 
mimi wenye rekodi ya kuwa wa kwanza kufika daresalaam
wananifurasha sana....
wanakuwaga na mbwembwe saana..lol

vikao vyote vya ndugu wanataka vifanyike kwao ha ha ha lol
 
Back
Top Bottom