Sikuwahi kujua kama JF imebaki na low, poor poor profile thinker hivi.
Hivi wewe jamaa unajenga reli toka Dodoma to Arusha unataka kufanikisha kitu gani? Kuna mizigo mikubwa ya kusafirisha?
Unajenga sgr kwenda Kenye, man are you crazy.... Kenya wana banadari yao, unawapelekea nini?
Rwanda na Congo mashariki ni maeneo yanayoitegemea bandari ya Dar kwa mizigo yao yote. Pia wanaweza wakaitegemea Kenya.
Uganda wanaitegemea Tanzania na Kenya kwa mizigo. Je kati ya Kenya na Tanzania ni nani ana Miundo mbinu bora ya kuwezesha kupata hilo dili la kusafirisha mizigo ya Rwanda, Burundi, Uganda na Congo mashariki?
Ndio maana reli inaenda ziwa Victoria kwanza ili kuikamata mizigo ya Uganda na kuizimq Kenya. Pia kwendq Rwanda kuikamata Rwanda na Congo.
Yaani ulichoandika na upuuzi wa hali ya juu na nimetambua hautambui Micro na Macro economy.
Rudi darasani ndo utajua umuhimu wa huu mradi na uzembe wa JK kushindwa kujenga hii reli mpaka Kenya akataka kuijenga toka Mombasa hadi Kigali. Huu uzembe wa JK ungeua biashara ya bandari ya Dar.
Yaani mkuu nakusikitikia kwa ulichoandika.
Unaongelea macro na micro hapa wakati macro za kilimo kwanza tu mmeingiza siasa hakuna kitu. Reli zimeozeana hazipitiki barabara mbovu, viwanda mmeua kwa ulafi wenu. Mmeingia mikataba kihuni then inavunjwa kihuni tunalipa fidia ambazo watu wengine wana interest kwazo.
Hatujasoma uchumi lakini haihitaji kuwa na masters kutambua uhuni wa kagame na magu kwa sgr.
Kwanini msijenge kwa hela zenu wenyewe ili muwe na nguvu.
Kama ni ujenzi wa miundo mbinu anzeni kuimarisha reli hizi tulizonazo. Fufueni reli ya tanga. Acheni uhuni hizo macro economy na micro economy haziwezi kujioperate bila kutengenezwa.
Unatoka micro kwenda macro kama tu umeimarisha micro ambayo hasa ni uchumi wa ndani. Leo tukuyu mwakareli huko hakuna barabara viazi haviuziki ni km 50 tu hamsemi tunafanyeje huko kuna gesi imeanza kuchimbwa miaka nenda rudi, kuna utalii wa kila aina, kuna kilimo cha tija chai hakuna anayejali kuboresha barabara hata ya vumbi tu then mnakuja hapa macro micro sijui nini huko hv mnadhani elimu zenu za kukariri hizo hatuzijui.
Hamjui priorities mnajifanyia tu. Chunya hakuna barabara kuna migodi ya dhahabu, nenda Lindi kule barabara shida hakupitiki hamsemi tupeleke sgr mmekalia kwa kagame kwa kagame.
Hv kusini ikijengwa hakuna nchi tunapakana nazo zitafaidika na kutupa faida.
Mambo mepesi kabisa yanawashinda mtayaweza makubwa. Mnachojua ninyi ni kupiga wapinzani tu mabomu. Huo uchumi unaouongelea ni mfupa mgumu kwenu hamuuwezi.
Ask your self why to invest, to whom shall we invest, when to invest, which investment shall start, among a, b and c which is profitable to us.
Nakushauri wewe ndo urudi shule mie nimesoma uchumi wa wahenga wewe hunikamati hata chembe. Unachokijua ni minor sana ktk uchumi bado unaelea.
Hata tukizama kwenye calculations za kiuchumi bado wewe uko shallow. Usijibie mihemko ya mapenzi ktk vyama zama ktk ukweli.
Kwa akili yako unadhani magu uchumi anaujua hata chembe anachojua ni properties za compound tu. Angekuwa mtu anayeamini mawazo huru kweli tungefika mbali but not to this extent.
Asubuhi njema mkuu acha niwahi kutegua mitego yangu ya panya kujipatia kitoweo.