Reli ya standard gauge ya Rwanda na Tanzania ni kaburi la uchumi wa Tanzania

Sante!

Yote kwa yote...pia mista slimu hajawahi kuwa na mapenzi na kitu kingine chochote ukiacha yeye mwenyewe, familia yake na kabila lake. Nchi yake tu sina uhakika kama amewahi kuipenda.

Jamaa mjanja mjanja sana. Inatakiwa uwe smart kimuelewa vinginevyo unaweza ingia mkenge.

Makofia alizugwa sema slim hakuwa na interest nae ndio maana akampotezea lkn aliishajaa kwy 18 zake.
 
Mie ninaetoka KANDA YA ZIWA ... ninajua fika CHALLENGES nyingi tulizonazo katika CENTRAL LINE ikiwemo na muda utumikao kusafiri ama kusafirisha bidhaa especially from Dar - Mwanza (It's like a nightmare) .. wanasema wahenga AISIFUYE MVUA IMEMNYEA ... I exactly know what I'm saying ... katika issue moja tu ya TIME CONSUMING ... SGR itakuwa mkombozi tena sana ... watanielewa wenye ku-reason na si wabishi tu wasio na hoja ... Tunaoguswa na MRADI huu twapongeza na tutaendelea kupongeza na tukisubiria kukamilika kwake ...

By the way faida kiuchumi na kijamii kwa SGR NATIONWISE ziko nyingi sana ... tatizo mmeshajiapiza katu kutopongeza jitihada zozote zifanywazo na serikali ... yenu ni kupinga tu ... and the same time pretending to be TOTALLY BLIND ..
 
Hatujakataa reli za ndani kujengwa.Hivi Rwanda unaijua vema kweli wewe.Tunahitaji reli za ndani zijengwe ndiyo kilio chetu maana zinaozeana tu.Elewa hoja yangu.
 
Mimi nahisi bora tungejenga cc wenyewe, ili tuoparete cc, na sio kushare nchi mbili ktk ujenzi.

Maana hii ingetusaidia hata kutep another root on the way to other countries kama Burundi , Uganda and even Congo, lkn tukisema tujenge na Rwanda ,hasara ni kwamba pale tutakapotaka kutep other roots kutoka kwenye hiyo ya Tz to Rwanda ,kagame nae atahitaji kunufaika maana aliweka hela yake ktk kuestablish hii kama main root.
Kagame angetakiwa asiingie kabisa kwenye operation.

Kujenga hatujakosea still kuna manufaa, kwa kumubana zaidi huyu kiwembe ni bola tufanye kujenga cc kama cc afu yy alipie kila kitu, ili akizingua tu tunaminya na hatoweza kukoroma maana atajua kuwa hakuweka chochote kwenye ujenzi isipokuwa ni kusafrishia bidhaa zake tu.
 
Hii reli inahitajika ikiwa Tanzania inataka kufaidika kwa kujijenga kama logistic hub kwa Afrika mashariki na ya kati. Reli hii itahudumia Tanzania magharibi, na nchi nyingine za karibu ikiwa na uwezekano wa kuunganisha Burundi, Zaire, na hata Uganda. Mipango mingi ya maendeleo na ufanisi ina athiriwa na miundombinu mibovu ya usafiri iliopo sasa
 
Mkuu pamoja na madhaifu yaliyopo, ukweli ni kuwa kusafirisha mizigo mwa malori ni uchumi mfu na ndio maana nchi ilikuwa imelala. Nchi zote zinazoendelea matumizi ya reli za kisasa hayaepukiki, kusadirisha mamontena kwa malori haitakiwi kabisa. Nikisoma sababu za maana za uchumi kufa kutokana na reli hii hujazitaja, kama ni kwanini reli ya kati ndiyo inajengwa kwanza, tuombe tupate hela na njia nyingine za TAZARA na Tanga hadi Arusha zijengwe. Tunakoelekea hata usafiri wa mabasi hautahitajika tena maana hakuna sababu ya kusafiri siku mbili wakati unaweza kutumia masaa 7 tu kwa njia ya train.
 
Mkuu Rwanda anachukua mizigo kupitia either kenya's au tz's ports. Kisha yanasafirishwa kwa malori to rwanda. Hvyo basi, kama nchi mshindani wetu mkuu ni kenya. Unahtaji mambo mawili.
1. Kuimarisha bandari(usalama wa mizigo na muda wa clearance)-hili hata kenya wanaweza kulifanya.
2. Kufupisha muda na kuondoa kero & cost za usafiri-kutoka dar to kigali.-hapa ndipo SGR umuhimu wake ulipo. Na kenya tutawashnda hapa.

Kumbuka sisi ni lango, hvyo lengo la SGR ni kuongeza ufanisi. Muda ukiwa mfupi, option ya trader's wa kigali itakua dar na si nairobi tena.
 
Ni wazo zuri sana.
 
Chuki nyingine hazifai kabisa. Afrika ni moja.
 
Mleta post atakuwa mhutu mwenyechuki kaliii sanaa,bahati mbaya nimeshindwa kumuelewa ana maanisha nini na nini lengo lake?pyuuu
 
Reli iliyopo ilijengwa miaka 100 iliyopita. Imezeeka na inahitaji kuwa replaced...
Kama hii iliyokuwepo haikuwa na tija ijayo itakuwaje na tija. Shirika la reli lilitakiwa kujiendesha na kujenga lenyewe, nchi ina friska hata kuweka nchi juu ya hiyo reli haitwezekana
Chama hicho hicho kila kiongozi akija na lake. Wanauza wee badae anukuja mwingine maneno ya kupiza kibao
 
Huyo jamaa mna mu over rate sana...hana uwezo huo.
 
Mleta post atakuwa mhutu mwenyechuki kaliii sanaa,bahati mbaya nimeshindwa kumuelewa ana maanisha nini na nini lengo lake?pyuuu
Endelea kuniita mi mhutu kwa sababu mnajua mlivyowaua 1994.
Naipigania nchi yangu Tanzania, naitetea isiliwe kihuni na wahuni wengine walioiharibu Congo hadi isionekane sehemu ya amani duniani.
Endelea kuinamishwa ili usihoji lolote.
 
Sikuwahi kujua kama JF imebaki na low, poor poor profile thinker hivi.

Hivi wewe jamaa unajenga reli toka Dodoma to Arusha unataka kufanikisha kitu gani? Kuna mizigo mikubwa ya kusafirisha?

Unajenga sgr kwenda Kenye, man are you crazy.... Kenya wana banadari yao, unawapelekea nini?

Rwanda na Congo mashariki ni maeneo yanayoitegemea bandari ya Dar kwa mizigo yao yote. Pia wanaweza wakaitegemea Kenya.

Uganda wanaitegemea Tanzania na Kenya kwa mizigo. Je kati ya Kenya na Tanzania ni nani ana Miundo mbinu bora ya kuwezesha kupata hilo dili la kusafirisha mizigo ya Rwanda, Burundi, Uganda na Congo mashariki?

Ndio maana reli inaenda ziwa Victoria kwanza ili kuikamata mizigo ya Uganda na kuizimq Kenya. Pia kwendq Rwanda kuikamata Rwanda na Congo.

Yaani ulichoandika na upuuzi wa hali ya juu na nimetambua hautambui Micro na Macro economy.

Rudi darasani ndo utajua umuhimu wa huu mradi na uzembe wa JK kushindwa kujenga hii reli mpaka Kenya akataka kuijenga toka Mombasa hadi Kigali. Huu uzembe wa JK ungeua biashara ya bandari ya Dar.

Yaani mkuu nakusikitikia kwa ulichoandika.
 
Unaongelea macro na micro hapa wakati macro za kilimo kwanza tu mmeingiza siasa hakuna kitu. Reli zimeozeana hazipitiki barabara mbovu, viwanda mmeua kwa ulafi wenu. Mmeingia mikataba kihuni then inavunjwa kihuni tunalipa fidia ambazo watu wengine wana interest kwazo.
Hatujasoma uchumi lakini haihitaji kuwa na masters kutambua uhuni wa kagame na magu kwa sgr.
Kwanini msijenge kwa hela zenu wenyewe ili muwe na nguvu.
Kama ni ujenzi wa miundo mbinu anzeni kuimarisha reli hizi tulizonazo. Fufueni reli ya tanga. Acheni uhuni hizo macro economy na micro economy haziwezi kujioperate bila kutengenezwa.
Unatoka micro kwenda macro kama tu umeimarisha micro ambayo hasa ni uchumi wa ndani. Leo tukuyu mwakareli huko hakuna barabara viazi haviuziki ni km 50 tu hamsemi tunafanyeje huko kuna gesi imeanza kuchimbwa miaka nenda rudi, kuna utalii wa kila aina, kuna kilimo cha tija chai hakuna anayejali kuboresha barabara hata ya vumbi tu then mnakuja hapa macro micro sijui nini huko hv mnadhani elimu zenu za kukariri hizo hatuzijui.
Hamjui priorities mnajifanyia tu. Chunya hakuna barabara kuna migodi ya dhahabu, nenda Lindi kule barabara shida hakupitiki hamsemi tupeleke sgr mmekalia kwa kagame kwa kagame.
Hv kusini ikijengwa hakuna nchi tunapakana nazo zitafaidika na kutupa faida.
Mambo mepesi kabisa yanawashinda mtayaweza makubwa. Mnachojua ninyi ni kupiga wapinzani tu mabomu. Huo uchumi unaouongelea ni mfupa mgumu kwenu hamuuwezi.
Ask your self why to invest, to whom shall we invest, when to invest, which investment shall start, among a, b and c which is profitable to us.
Nakushauri wewe ndo urudi shule mie nimesoma uchumi wa wahenga wewe hunikamati hata chembe. Unachokijua ni minor sana ktk uchumi bado unaelea.
Hata tukizama kwenye calculations za kiuchumi bado wewe uko shallow. Usijibie mihemko ya mapenzi ktk vyama zama ktk ukweli.
Kwa akili yako unadhani magu uchumi anaujua hata chembe anachojua ni properties za compound tu. Angekuwa mtu anayeamini mawazo huru kweli tungefika mbali but not to this extent.
Asubuhi njema mkuu acha niwahi kutegua mitego yangu ya panya kujipatia kitoweo.
 
Usiuvae ujinga halafu ukatamba nao hadharani!Mikoa ya kanda ya ziwa na magharibi kama Kigoma bidhaa huwa juu kwa sababu ya usafirishaji,halafu wewe kwa akili yako unaiona Rwanda tu badala ya kuona mikoa kama Singida ,Tabora,Shinyanga,Mwanza,Kigoma,Kagera n.k.Sehemu zote hizi zitafaidika na mizigo kwa bei nafuu.
Nakumbuka wakati train linapita na mizigo zamani mikoa hii ilifaidika sana kibiashara.
 
Sasa hilo treni lililokuwa linapita na mizigo enzi hizo nani kaliua. Tumia akili kidogo tu kuelewa siyo kutafuta kiki za ovyo. Waha, wasukuma, wahaya, wanyamwezi ni ndg zetu sote tunawapenda ila tunsema sgr si kwa ajili yao na msitegemee cheap kwa hilo. Huyu rais ndiye aliyesema kama mtu hana mia mbili aogelee kuvuka kule kigamboni. Unadhani atakuwa na huruma nawe hata chembe. Acha kujipa matumaini.
 
Mkuu naheshimu mchango wako kutokana na uelewa wako. But naamini hii SGR ni sahihi na imekuja kwa wakat sahihi katika ushindani wa kikanda. Hizo changamoto zingine zinatatulika kwani hazina ushindani ndani yake.

Magufuli sio mchumi na kati ya rais watano waliopita na wa sasa ni Kikwete pekee ndio mchumi lakini amefanya nin?

Magu is right towards taking the country into EA Region power katika uchumi na wacha watu walielie lakini tutafika tu.
 
Je kuna ulazima wa kufanya partnership ktk ujenzi?. Ni lazima?. Kwann tz wasijenge pekee yao ili yule asiwe kero baadaye. Nani kashinikiza hiyo partnership?.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…