Religious people are less intelligent than atheists, according to scientific studies

Huko kutokuwa na dini,ndio dini yenyewe,dini maana ni mfumo wa maisha,sasa iweje mtu aseme hana dini.Hao wanaosema hawana dini,hawajuwa nini maana ya dini.Dini,maana yake ni mfumo wa maisha unaojichagulia,huko kusema huna dini ndio dini yenyewe.

Wewe pia unaendelea kuthibitisha kuwa theists wako likely zaidi kuwa na uwezo wa chini wa kufikiria kulliko atheists! Unaposema Dini ni "mfumo wa maisha" unaojichagulia kisha unaishia hapo tu haujaeleweka hata kidogo! Kikundi cha watu kikiamua kuwa na mfumo wa maisha ya wizi hiyo ni dini?

Kikundi cha watu kikiamua kuishi kwa mfumo wa ujamaa utaiita na yenyewe ni dini? Dini ni jamii ya watu inayoishi kwa kuamini kuwa kuna "muumba" au deity, super power, hasa nafsi yenye nguvu na yenye kuweza kuinfluence maisha yao hapa duniani. Kwa ujumla dini ni kuamini kitu kisichokuwapo, na kukitetea kwa nguvu zote, na hata kufikia kuwacharanga mapanga wasioamini!
 

Lakini unaweza kumfundisha kuwa kuna Mungu ambaye ni baba wa wote, mungu aliyeumba kila kitu kwa udongo wa mfinyanzi, Mungu huyo huyo anaishi Juu mbinguni?

Kwamba Mungu ana mwanaye anaitwa Yesu, Yesu ambaye pia ni mungu ambaye alijituma duniani akajiingiza tumboni kwa mwanadamu baadaye akazaliwa na kuwa mkorofi kwa kwenda kinyume na sheria zilizowekwa, baadaye akajitoa muhanga na kuruhusu wanadamu aliowaumba wampige mawe na kumuuwa ili awasamehe dhambi ambazo walizaliwa nazo (dhambi za asili)!!! Hivi unafikiri kati ya EVOLUTION na hizo HADITHI ni kipi atakachoamini kirahisi?

Tusiwalishe watoto sumu tulizolishwa sisi, watoto wangu mimi nawafundisha vyote, nawaonesha kitabu cha hadithi za "Mungu" na kuwafundisha stori zake, nawafunulia vitabu vya sayansi na kuwafundisha evolution, wao wakikua watafikia muafaka wa nini wanachoona ni ukweli na kipi ni uwongo.
 
Waache tu wajitetee hao wasiomtambua Mungu. Mungu anawaona vizuri tu na ameahidi kuwa atawanyooshea maisha yao ili wajione kwamba hivyo wanavyoamini nisawa ila siku ya hukumu hawatakua na pakukimbilia!!!

Jadili mada mkuu, acha hadithi!
 
Kimsingi hapa mimi nadhani kusema tu kuwa watu wa dini wana matatizo fulani kama haya ya kufikiri na wasio na dini hawana bila kutuambia hiyo dini inwafanyaje wasiwe na uwezo mzuri wa kufikiri ni tatizo pia

Mimi nasema kuwa kuna dini ambazo ni tatizo,mtu ukiwa muumini wake unakuwa na matatizo fulani hivi lakini unapozijumlisha dini zote unakuwa hujatenda haki

Matatizo yanayosababishwa na watu kuzifuata dini za hovyo ni mengi sana lakini pia ukiangalia kwa makini utagundua kuwa matatizo hayo sio ya dini ila ni watu

Kumbuka kuwa unapokuwa mtu mzima unaanza kufikiri kwa makini kama umeshindwa kufikiri na kujua kuwa dini hii ni ya hovyo hapo dini ndo inakuwa na matatizo kweli?Sidhani!
Hapa matatizo ya kufikiri ya wanadamu yamesababisha watu kuanzisha mambo ya hovyo[ikiwemo baadhi ya dini] hapa nadhani ndipo penye tatizo kubwa

Haya mabo ya kusema kuwa mtu wa dini hafikiri vyema au dini inamuondolea mtu uwezo wake wa kufikiri ni tusi kwa dini ambayo haipo hivyo

Hata wasiokuwa na dini wana mambo mengi sana ya hovyo lakini hatuwezi kusema kwa kuwa wamekuwa hivyo kwasababu hawana dini

Kuna mambo mengi sana kwenye sayansi ambayo ukifikiri vyema unaona ni hadithi za kutunga tu!!!
 
Lakini unaweza kumfundisha kuwa kuna Mungu ambaye ni baba wa wote, mungu aliyeumba kila kitu kwa udongo wa mfinyanzi, Mungu huyo huyo anaishi Juu mbinguni?

Kwa ufahamu wako wewe Mungu ni nani/nini?

Kuwa baba maana yake nini?

Kuumba maana yake nini?

Mbinguni ni wapi/nini?
Kwamba Mungu ana mwanaye anaitwa Yesu

Kuwa mwana wa Mungu maana yake nini?

, Yesu ambaye pia ni mungu ambaye alijituma duniani akajiingiza tumboni kwa mwanadamu baadaye akazaliwa na kuwa mkorofi kwa kwenda kinyume na sheria zilizowekwa

Kwanza leta ushahidi wa madai ya Yesu wenda kinyume cha sheria zilizowekwa,halafu niambie ni nani aliziweka hizo sheria

Pili kuwa mkorofi maana yake nini?
, baadaye akajitoa muhanga na kuruhusu wanadamu aliowaumba wampige mawe na kumuuwa

Mosi:Si kweli kuwa Yesu aliuwawa kwa mawe,huu ni uongo mkubwa
Pili:Niambie ni nini maana ya kujitoa muhanga


ili awasamehe dhambi ambazo walizaliwa nazo (dhambi za asili)!!!

Naomba ushahidi wa madai yako haya kuwa Yesu aliuwawa ili watu wasamehewe dhambi ya asili
Kisha uniambie dhambi ya asili maana yake nini
Hivi unafikiri kati ya EVOLUTION na hizo HADITHI ni kipi atakachoamini kirahisi?

Evolution maana yake nini?
Hadithi ni nini?Maana yake nini?

Kama ataamini chochote kirahisi huyo atakuwa na matatizo ya akili
Yoyote anaeamini au kutafuta kuamini kirahisi au anatafuta mabo ya kumwaminisha mtu/mwanae mambo kirahisi,mada hii itakuwa inamuhusu bila kujali ni mwenye dini ama laa

Halafu unajua nini maana ya kuamini wewe?
Tusiwalishe watoto sumu tulizolishwa sisi

Sumu ni ipi wewe?

Kwanza hujasema sumu ni ipi na kama kuna sumu iweje useme kuwa utampa mwanao kama ulivyosema hapa chini:

, watoto wangu mimi nawafundisha vyote, nawaonesha kitabu cha hadithi za "Mungu" na kuwafundisha stori zake, nawafunulia vitabu vya sayansi na kuwafundisha evolution, wao wakikua watafikia muafaka wa nini wanachoona ni ukweli na kipi ni uwongo.

Yaani wewe ndo kilaza hasa

Unampa mwanao "sumu" halafu unasema akikua atakuja kujua ukweli ni upi na uongo ni upi,si atakua ameshakufa kifikra kama wewe ambae umelishwa sumu na hata baada ya kujua ni sumu bado umempa mwanao?

Halafu unajikinza
Kwanza umesema sumu halafu unakuja tena kusema nitampa vyote ili ajue ukweli ni upi inamaana pamoja na kuja hapa kuandika haya hujui ukweli ni upi kiasi kwamba mwanao ndio aje akuambie

Una maana gani kusema sumu?

Au hujui ulichokisema???
 
THE RELIGIOUS PEOPLE ARE MORE INTELLIGENT:
GLORIFIED AND EXALTED IS ALLAH, PRAISED BE TO ALLAH:-
THERE IS NO GOD BUT 'ALLAH'

ALLAH IS ALONE, HAS NO PARTNER, FOR HIM IS THE DOMINION AND FOR HIM IS THE PRAISE HE IS OVER ALL THE THINGS OMNIPOTENT. THERE IS NO POWER AND NO MIGHT EXCEPT BY ALLAH, AND NONE IS WORTHY OF WORSHIP. HE HAS THE FAVOURS, AND THE BOUNTY AND TO HIS MIGHTY IS THE BEST GRATEFULNESS.
NO GOD BUT ALLAH WE DEVOTE OUR RELIGIOUS CONVICTION TO HIS MIGHTY , EVEN IF THE DISBELIEVERS(KUFAAR/ MAKAFIRI) HATE THAT.
Allah granted us very slightly knowledge...
 

Hivyo ndivyo jinsi wewe huwa unajadili hoja? TOO LOW!:tape:
 

BASI, hivyo tu?:bored:
 
Oh? Pitia signature yangu huenda ujumbe ukaupata kidogo....:tape:


Kama umeshindwa kujibu maswali yangu hapo juu wewe ndo huna brains

Kwako wewe mtu akiwa hana dini ana akili

Na asiekua na dini ndio ana akili

Hii maana yake nini?

Hata kufafanua nini maana ya kuwa na dini kwanini mwenye dini awe hana akili umeshindwa

Sasa hapo ni nani hana akili

Hiyo signature yako haielezi chochote

Mtu yoyote akiisoma haelewi kitu labda awe hafikirii kama wewe


Ok, hebu angalau nifafanuie dini ni nini

Kisha uniambie kutokuwa na dini ni nini

Halafu uniambie ni kwanini mtu akiwa na dini awe hana akili

Na kwanini mtu asipokuwa na dini awe ana kili
 
You are better off with an ignorant person who is conscious of his ignorance. It becomes a problem when you assume your ignorance is wisdom and lead people into trouble.

Pathetic ignoramus non-theists.
 

Habari za Yesu sio story ni facts, sasa wewe kama unaweza kushindwa kumfundisha mtoto historia ya kweli na kile ambacho kilinenwa na kutendwa,kwa kisingizio chochote ni udhaifu tu wa kibinadam,lakini kumfundisha mtoto kwamba kenge,binadam,panya,punda, twiga,tembo,macho,masikio na midomo ni vitu ambavyo vilitokea kkutokana na uhitaji wa viumbe kimazingira,viumbe vilipohitaji kula,mdomo ukamea ili viumbe viweze kula,viumbe vilipohitaji kuona,macho yakamea,lakini hili tendo linaitwa evlotion,kwa sasa hivi huwezi kuona evolution inayoendelea au iliyonusu kwa kuwa evolution inachukua mamilioni ya miaka kutokea,mfano unakumbuka malaria ilikuwa inatibiwa kwa klolokwini ?

klolokwini ilishindwa baada ya wale wadudu wa malaria kuevolve na kuwa ngedere kwenye damu,hivyo klolokwini ilikuwa watu wanapomeza kuua plasmodiamu ikifika kwenye damu inawakosa plasmodiamu kwa kuwa wali-evolve na kuwa vingedere vidogo,hivyo wataalam wakagundua kwamba dawa ya kuuwa vingedele ambavyo vimerithi uambukizaji wa malaria ni kutumia SP, lakini bado Sp inasusua kwa vile vile vingedere sasa hivi ni aina ya binadam waitwao Atheist,dawa ya kuwauwa ndiyo kwanza inafanyiwa majaribio.

Hiyo sumu ya evulution at Macro level hata vichaa hawawezi kuiamini inahitaji zaidi ya kichaa,zaidi ya mpumbazu,zaidi ya zezeta...Lakini ilisemwa na mzungu tutafanyaje na tunaaamini hakuna Mungu ? maana ukikubali kwamba evolution (Macro)si kweli,bali ni chaka la kuhalalisha imani ya kutokuwepo kwa Mungu, utatakiwa ulete nadharia nyingine,kwani iliyobaki ambayo sisi wenye akili kidogo tunaijua na ina mantiki ndani yake ni uumbaji,huku tukiamini juu ya evolution at micro level. ipo evolution kwenye viumbe vyenye nasaba moja,alkini si kwa viumbe vyenye nasaba tofauti.
Kama wewe ni mmoja wa Atheist na ukimaanisha ni mwenye akili,no wonder waafrika tupo hapa tulipo kama wenye akili wenyewe ni pamoja na wewe...MAJANGA
 

Nilitaka nishanga mtu wa dini ajadili hoja bila kuwaza kuuwana, mbona tunawaona kila siku mnatupiana mabomu na kutukanana, ni kawaida yenu wala hamshangazi! Hivi kwa akili ya kawaida kabisa unashindwa mpaka kuelewa impact ya wamisheni katika kuleta ukoloni katika bara la Africa?

Sijawahi kuona vidence yoyote ya uwapo wa Mungu, na siwezi kuamini kuwa niliumbwa sijui na jamaa gani wakati naelewa kabisa nilizaliwa na wazazi baada ya sperm ya baba kukutana na yai la mama, hiyo itakuwa ZAIDI YA KUJITOA AKILI! Naamini miungu ipo, Eli naye ni labda ni mmojawapo tu wa miungu hiyo, na mtu yeyote anaweza kuwa Mungu, hata mimi naweza kuwa mungu, lakini hakuna Mungu mwnye mamlaka yoyote juu yangu.
 
Yote yaliyoandikwa humu yanamuhusu Ponda. Kwa bahati mbaya hata kusoma kiswahili hajui maana inasemekana hakwenda shule na mufti amethibitisha hili, sembuse lugha vya kiingereza tena! Aidha, yupo selo sasa kwa upumbafu wake! Loh!Ujumbe haujafika.
 

ndio pale unaambiwa "Only sheep need a shephard..by Carlos Mora" hii nimeitoa #Atheists_Quotes
 
Huu ni ukweli ingawa ni mgumu kumeza mkuu,...check walokole na wavaa visuruali vifupi then you will understand what i mean.

Ukweli ni kwamba, kuna watu huwa wanachagua kuacha kufikiri. Na hii haina uhusiano na dini tu, ndio maana kuna watanzania wengi tu wameamua kuacha kufikiri ingawa hawafuati sana dini.

Nafikiri "problem statement" iwe hivi, "Ni sababu zipi hupelekea baadhi ya watu kuamua kuacha kufikiri?". Hapo ninaamini tunaweza kupata majibu ya kushangaza sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…