Pamoja na namna unavyojionyesha ulivyodhaifu katika kutafakari ni wajibu wetu sisi ambao tupo kwenye nuru kuwasaidia ninyi mnaoenenda gizani kwa kutokutaka kweli.nuru ili mtende kwa kadri ya udhaifu wa KIBINADAMU '' Mkipewa nguvu na kiburi cha uzima''
Naomba wewe au mwenzio ambaye ni muumini wa ATHEISM anijibu maswali yafuatayo ili nielewe namna ambavyo ninyi naweza kuwafundisha na kuwatoa gizani au kujifunza kutoka kwenu.
1. kwa mtu asiyejua ATHEIST ni mtu wa namna gani waweza kutotelea maana ya Mtu kuwa ATHEIST ?
2. Ni kwa kiwango gani madai ya ATHEIST juu ya kuwepo au kutokuwepo kwa mungu yanawakilisha ukweli ?
3. UKWELI kwa Tafsiri ya ATHEIST ni nini ?
4. Je kwa ATHEIST uwepo wa Mungu ni lazima uthibitiswe kisayansi ?
5. Ni ushahidi wa aina gani ATHEIST anataka ili kuthibitisha kuwepo kwa MUNGU ?
6. Ushaidi unaotakiwa kuthibitisha uwepo wa Mungu mnataka uweze kupimwa maabara ?
7. Nini wewe binafsi unahitaji ili kuamini kwamba Mungu yupo ?
8. Unaamini nadharia ya Evolution na kutanuka kwa dunia kusiko mwisho ? vipi kuhusu moyo wako, baada ya muda mrefu kupita na Moyo wako kuendelea kutanuka kwa sababu ya evolution itafika kipindi kifua chako kitashindwa kuufunika na kutoka nje na kutengeneza kitu kingine ?
9. Unaamini kwamba baada ya muda mrefu,hii kutokana na evolution,manowali za kivita zitakuwa zinachumwa kwenye mipera ? lala salama Atheist ukiamka naomba jibu hayo maswali ili nithibitishe jinsi ulivyo Zu.Zu
:bored::bored::bored:
1) Atheist, mtu asiyekubali uwepo wa "a supernatural being", yani mtu mwenye nguvu zisizo za kawaida, AMBAYE NI MTAKATIFU, kama wanadini wanavyodai.
2) Kwa kiwango kikubwa kwa kuwa throughout history hamna aliyeweza kuthibitisha uwepo wa kiumbe kama huyo, zaidi ya kupeana moyo kuwa ana sababu zake za kujificha na kuwa kimya, ikiwemo ile ya 'mungu ni mkuu sana kuliko wewe so ahitaji kukuthibitushia chochote"!!!
3) ona number moja
4) Labda kwakuwa sayansi kwako ni kitu cha ajabu, lakini jibu ni ndio. Kuna mambo watu wanaona "ya ajabu" na "ya kiroho" wakati yana maelezo "perfect" ya kusayansi. Mfano meditation. Hata mungu akijitokeza siku moja kila jicho likamwona, nayo ni sayansi. Na kwani mungu na ukuu wake wote anaona ugumu kutoa uthibitisho rahisi tu ambao hamna wa kupinga????! Kwanini kang'ang'ania kuwa 'tumwamini tu' na wale 'wachache' aliowatuma/anaowatumia? We hushituki tu!!! Au ndo hivyo, ni moyo sana hapaswi kuulizwa chochote?
5) wowote usiohusisha imani ya dini fulani; ambao hautapingwa hata miaka elfu ijayo; ambayo iko kifacts zaidi ya kiimani; ambayo either umeishi kwenye misitu ya Amazon miaka yako yote au pale New York, utajua; ambao kwa "uwezo wa kibinadamu" YAANI kisayansi utafunga mioyo yote inayothubutu kukataa uwepo wa mtu huyu MKUU , MWENYE NGUVU ZA AJABU.
6) sio lazima maabara......kuna njia zingine ni ndogo sana ukilinganisha na ukuu wa huyu, mfano, sali chungwa litokee mkononi just to prove he's there.
7) mungu siku aongee dunia nzima imsikie na imuelewe, aongee either kama mtu mkatili na mwenye mamlaka kama tulivyomzoea, mfano aseme "BADO HAMTAKI KUNIAMINI, MOTO NI WENU", au aongee kama yule mungu aliyekuja dunuani, "EEEENYI WANAANGU, MBONA MNA MIOYO MIGUMU KUAMNI? KILA KITU UTHIBITISHO TU. BASI KWAKUWA NAWAPENDA SANA, LEO NIMEWAPA UTHIBITISHO MKUU KULIKO YOTE"...dah, itabidi siku hiyo kila mtu afunge na kusali na kuvaa magunia. BTW angekuwa anatupenda sana angeondoa mateso toka miaka mia elfu iliyopita....jamaa either ana moyo mgumu kweli, au hawapendi tu na anafurahia mateso yenu, au HAWEZI, au HAYUPO.
8) the fact kwamba the universe inatanuka ni FACT na sio UNABII, so uhitaji kuamini unahitaji kujua.
Tatizo watu wengi wanajifanya wanajua evolution wakati hawajui....mimi kwenye mijadala ya evolution huwa mkweli kuwa sijasoma evolution hasa katika macro-level. Evolution katika micro-level uhitaji hata ufike darasa la saba. Nani asiyejuwa vijidudu hugeuka na kuwa resistant kwa dawa? Ingawa ukifikiria utajiuliza hivi vidudu vitakuwaje miaka hata elfu tu ijayo? Hence, macro evolution.....
Kutanuka kwa moyo???
Maswali mengine ni ya kichokozi tu, sasa wewe kama unaona vitu vinabadilika baada ya muda kwa nini unauliza tena kama mtu anaamini atabadilika? unless the process stops, organisms WILL go on changing.
9)unamaanisha advance in technology ndo evolution au?
Ndio maana atheists got to work, wanajua ni juu yetu kutunza hii dinia na si kusubiri kiama....kwanza kuwa mkweli, katika historia yote ya mwanadamu, watu walipigana kwa misingi ipi kama si mungu na imani....hata waliogombania mali na wanawake walisema ni mungu ametupa.
Atheisism, kama Theism, ikitumiwa vibaya italeta maafa.
:wave::wave: