labda uniambie unaelewaje wanafunzi wake wanapotakiwa kubatizwa kwa baba, mwana na roho mtakatifu? kwanini isiwe ubatizo kwajina la mungu?. yesu ananafasi gani kwa mwanadamu? na uhusiano wao unauelewaje?, ningependa maelezo yako then uweke andiko. kwasababu hata wanafunzi wake walichoshwa na maelezo ya yesu wakamwambia awaonyeshe baba, pale waliposema ''utuonyeshe baba yatosha..,'' akawauliza amekaa nao siku zote hawakumjua?. yesu ni nani mpaka aje kutoa hukumu, ninani mpaka aweze kufufua wafu, ni nani mpaka asiwe na dhambi, ni nani mpaka aje na amri mpya za upendo, na baba yake mzazi hasa ni nani ukiyajibu haya maswali kwa kuyaelewa then utakuwa unamwelewa yesu vizuri. zaidi ya hapo utakuwa mshabiki tu. na pengine kujaribu kumshusha yesu kama mitume na manabii wengine kitu ambacho hakitakusaidia kuijua kweli yake.fahamu tena ya kwamba huwezi kumwomba mungu bila kupitia jina la yesu. kwakuwa yeye ndiye njia. just imagine manabii wote, kuanzia musa, nathan, isaya, daniel, yohane, hajatokea nabii aliyewahi kusema yeye ndiye, isipokuwa ni yesu kristo pekee yake. kama ambavyo haijatokea nabii/mwamuzi ama mtume yoyote awaye yule aliyezaliwa na mwanamke pasipo baba yake kujulikana. je baba yake yesu atakuwa nani?tafakari.
elimu ya kujua utatu mtakatifu sio rahisi kama tunavyoijadili hapa, nachofanya hapa ni kukueleza just in a nut shell ili uelewe kwanini yesu ndiye ufunguo wa kuingilia mbinguni. pia tusijaribu kuwatenganisha kwani hata ubatizo unawahusisha wote watatu kwa umoja wao, swala la kusema kuna mdogo na mkubwa alitasaidia kwani tangu mwanzo mungu alijidhihirisha peke yake, lakini hapo baadae akamtoa mwanawe wa pekee ili amwaminie asipotee bali awe na uzima.na ndiye mwenye mamlaka duniani na mbinguni, trust me ndiye atakuja kuhukumu wazima na wafu.aliye na mamlaka duniani na mbinguni ndiye mungu wako wa kumtumaini ili uifikie mbingu ambayo utaishi milele na mungu. Emmanuel alikuja kutuonyesha mungu yukoje, na ndio maana maagizo yake yako 100% balanced, gender balanced, wealth balanced, race balanced, na upendo ndio nguzo kuu. so if you expect something else you are going astray. for god sake, wengine ni wevi na wanyang'anyi bali yesu ndiye wa kwanza na ndiye wa mwisho, atampa yule ashindaye maji ya uzima.
UTATU MTAKATIFU!
ndugu
2013 ! we unakubali kabisa kuwa "
utatu mtakatifu" ni suala la msingi kabisa la imani yako! na suala la msingi katika imani yoyote akili inakwambia kuwa,
linatakiwa kuwa NI RAHISI KUELEWEKA KWA WAUMINI WOOTE! BILA KUJALI ELIMU ZAO NA INTELIJENSIA YAO!!
SWALI- JE HUJIULIZI KWA NINI LEO KARIBU ULIMWENGU MZIMA WA WAKIRISTO SUALA HILI HALIJAPATA UFAFANUZI WA WAZI?? we kweli unakubali MUNGU MKUU ALIYE TUUMBA WOTE ATAFANYA KUSUDI KUTUWEKEA MSINGI WA IMANI YENU KUWA MGUMU NAMNA HII KUELEWEKA??
NA KAMA HIVYO NDIVYO UNAVYOTAKA KUAMINI HUONI KAMA MISTARI HAPA CHINI INAPINGANA NA IMANU HIO??
HEBU ANGALIA HAPA YESU ANASEMA NINI!!
Yohana 17:8. Hapa Yesu anasema:
"Mimi nimewapa ule ujumbe ulionipa; nao wameupokea; wanajua kwamba kweli
nimetoka kwako; na wanaamini
kwamba wewe ulinituma".
"Sikieni, enyi Israel: Bwana Mungu wetu ni Mungu Mmoja tu" (Marko 12:29)
Yohana 5:37, Yesu anasema:
"Naye Baba aliyenituma hunishuhudia. Nanyi hamjapata kamwe kusikia sauti Yake, wala kuuona uso wake".
TAZAMA HAPA KUYATHIBITISHA HAYO MANENO YA YESU KUUHUSU UONEKANO WA MUNGU!!
kitabu cha kutoka 33:20, Mungu anamwambia Musa:
"
Huwezi kuniona uso wangu, maana mwanadamu hataniona akaishi".
SWALI LA NYONGEZA!!
KAMA YESU NI MUNGU! IWEJE ASEME MUNGU HAONEKANI WAKATI YEYE ANAONEKANA NA WANAFUNZI WAKE KILA SIKU??
UBATIZO
tunajifunza ktk andiko kuwa
YESU alibatizwa mwaka wa 29 W.K., alipozamishwa katika Mto Yordani na Yohana Mbatizaji.
Yehova alikuwa akitazama na akamkubali. (
Mathayo 3:16, 17)
hapa tunaona kuwa wakati
YESU ANABATIZWA! YEHOVA PIA ALIKUWEPO ANATIZAMA! kwa maana nyingine HAPA KUNA YESU NA YEHOVA AU SIO?
SWALI- KAMA YESU NI MUNGU MMOJA! HUYU YEHOVA ALIYEKUWA ANATAZAMA NA AKAMKUBALI NI NANI??
MUNGU KUMTOA MWANA WA PEKEE ILI WANAADAMU WAOKOKE!!
SOTE TUNAJUA KUWA KUMUUA MWANAO AU MTU YYT ILI UFANIKISHE JAMBO FULANI NI KUMTOA KAFARA HUYO MWANA AU MTU
BIBLIA INATUFUNDISHA KUWA MUNGU HAKUPENDA IBADA YA KUTOA KAFARA YA DAMU!
Wakati baadhi ya kafara hizi zilizotolewa na Wayahudi zilifanywa kwa ajili ya maondoleo ya dhambi, Mitume waliokuja baadaye walikataza jambo hili.
Katika Hosea 6:6, kwa mfano, tunasoma:
"Kwa kuwa Ninataka upendo thabiti na sio kafara".
Mungu alitaka upendo - ambao husababisha kumwamini Yeye na utii wa sheria yake - kwani hii ni bora kuliko damu ya kafara. Hata Yesu mwenyewe aliusisitiza ujumbe huu tena,
katika Mathayo 9:13, ambapo anasema:
"
Nendeni na mkajifunze maana ya maneno haya: Ninataka rehema sio kafara."
Paulo aliyaweka yote haya pembeni akasema kwamba Yesu, kiumbe mkamilifu, alikuwa "Kafara (muhanga) wa mwisho" alipoyatoa maisha yake msalabani.
katika Ezekiel 18:20 -22:
"- - Mtoto hatabeba dhambi za baba, wala baba hatabeba dhambi za mtoto."
SASA WEWE NDUGU YANGU UNAKUBALI KABISA KUWA!
Kutokana na suala zima kwamba Mwenyezi Mungu alimtaka Yesu ayatoe maisha yake kwa ajili ya dhambi za wanadamu, Paulo alimchukua Mwenyezi Mungu anayewapenda na kuwajali viumbe wake akamfanya kuwa ni katili na aliye mbali sana ambapo kitu kingine chochote kisichokuwa damu ya Yesu hakiwezi kumfikia wala kumridhisha.NA WEWE KWELI UKAKUBALI HILI??
NA HAPO NYUMA UTAONA MTU ANAEIFANYA BIBLIA IGONGANE NI PAULO NA ALIYEKUWA KARANI WAKE LUKA!! BAASI
KWA SABABU BIBLIA INASEMA!!
Wakorinto wa kwanza 14:33 kwamba:
"Mungu sio mwanzilishi wa utatanishi na migongano". (Mysteries).
SASA JE UTAENDELEA KUAMINI IMANI AMBAYO INA MPARAGANYIKO KIASI HIKI?? NA UACHE KUAMINI ALICHO KIAMNI YESU AMBAYE ALIABUDU MUNGU MMOJA??
UAMUZI NI WAKO!!