Remigius: Secretarieti ya Chama Makao Makuu ilizuia majimbo 78 yasipewe printer za kadi , Laptop 254 na Video Camera 10 bure kisa janjajanja

WanaCHADEMA wanaosema Lissu hafai wanaweza kuwa na hoja lakini zote hazina mashiko.

Wengi ni waoga wa mabadiliko, ni sawa na wale watu ndani ya mfumo wanaoamini CCM haipaswi kuachia madaraka, wakihofia uongozi wa chama kipya utawatendea vipi? Utavumulia madudu yao kama CCM inavyovumulia?

Nashangaa kuona baadhi ya WanaCHADEMA wanaogopa mabadiliko ambayo wamekuwa wakiyahubiri kila mahali.
 


Ninapoonaga kigogo anasema ufipa kuna wahuni kumbe ni kweli. Wavuliwe nguo chama kipone haraka.
 
Mmeanza sasa. Hakuna taasisi itakuruhusu kugawa vifaa kama hivi bila kuishirikisha maana wao ndio wanajua mahitaji haswa yako wapi. Hauwezi kuwa na mradi wa Chadema, na ukatafutia hela kwa ajili ya Chadema na pengine ukapata msamaha wa kodi kwa kutumia jina la Chadema halafu mwisho wa siku ukasema ule ni mradi wako sio wa Chadema. Haukuwa na nia ya kusaidia Chadema bali ulikuwa unatafuta umaarufu. Ndio maana umeibua leo ishu ya 2022 kwa matumaini kuwa Lissu atakukumbuka katika ufalme wake. Hebu fikiria kwa mfano Chadema wangekubalia halafu akatokeza mtu akasema kuwa zilipatikana kwa nia isiyo halali, au ni sehemu ya mpango wa kutakatisha pesa n.k. watakaochafuka si watakuwa Chadema na sio wewe. Au hizo kompyuta na kamera zina uwezo wa kurekodi na kurusha mambo ya ndani ya Chadema.

Acheni hayo. Badala ya kujenga mnabomoa.

Amandla...
 
Hiyo sasa porojo. CHADEMA haina watu wajinga kiasi hicho. Hii habari haijakaa vyema.
Sisingizi mtu yoyote hapo,Mzee Mbowe,Lema,Wenje ,Sugu na mdude hakuana aliefaulu elimu ya sekondari wala kuweza kupata hata course ya certificate kwa masomo ya chuo.
 
Bila Mwamba Mbowe saa hizi huyo Lissu asingechukua fomu za kugombea uwenyekiti angekuwa shimo la Tewa !!
Nenda ka google nini maana ya shimo la Tewa !
 
Kwani simu hazidakuliwi? Ujinga mzigo printer ya kuprint kadi inadakuliwa ili iweje? Pumbavu Sana
Laptop haiwezi kuwa compromised? CCTV camera haziwezi kuwa compromised? Hata printer zinaweza kuwekwa recording devices. Hamna information isiyokuwa na thamani.

Amandla...
 
Walikuwa sawa kumzuia, ameifanya kama project binafsi, hiku akitumia mtandao wa Chama, na kila kitu cha Chama huku akikinyima Chama taarifa muhimu zikiwepo taarifa za anayefadhili hiyo 'project yake'.
Yaani alijianzishia project ndani ya Chama akapanga kila kitu mwenyewe bila kushirikisha Chama, huyo mbana fala?Ingegundlika ufadhili huo ulikuwa na nia iliyojificha si ni Chama ndiyo kingewajibika na kuchafuka?
 
Mkuu hivi hujui hata hizi ziara za mikoani Lissu alikua anatafuta pesa zake na Mbowe ana raise za kwake!! Yaani chama kimoja ila kila mtu atafute pesa zake kufanyia siasa!!. Mind you as much as its fake news ila unaweza kuta hata huyo IT alikua hana mshahara wala ofisi ila unapewa cheo tu ila namna ya kufanya kazi it's up to you.

Chadema ilipaswa itoke huko kwenye kulia lia shida 2015-2020 tulikua na ruzuku kubwa sana ingetosha kuwa na miradi mingi mnoo ya kukipa fedha chama. Huu uchaguzi mpka uishe, hata Mbowe akishinda itakua phyrric victory.
 
Bila Mwamba Mbowe saa hizi huyo Lissu asingechukua fomu za kugombea uwenyekiti angekuwa shimo la Tewa !!
Nenda ka google nini maana ya shimo la Tewa !
Yeye ndio dk bigwa siyo ,acha upuuzi ,mzee mbowe anamtegemea lisu kuliko Lissu anavyomtegemea Mbowe
 
Hata mim limenifikirisha hilo
 
Huyo jamaa hadi sasa bado ni IT wa chama????
Code of ethics.
 
Mbowe ni balaa na nusu
 
Mbowe angepisha tu huu upepo aisee
 
Sawa sawa mkuu
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…