EricMan
JF-Expert Member
- Oct 5, 2017
- 3,050
- 5,420
Achana na mambo ya kuchapwa lipia Free internetNipo natumia huduma ya Tigo postpaid, nalipia elf 60 kupata gb 80 kila mwezi (mikataba kwa wateja wapya imebadilika unapewa gb 72)
Kifurushi hiki huwa kinajiunga chenyewe kila tarehe 1 ya mwezi mpya saa sita usiku siku inapoanza.
Nilitaka kufanya utafiti wa kujua kama pana upigaji maana ni kawaida sana kwa mitandao yetu kusikia haya malalamiko kutoka kwa wateja, nikaona nami nifanye research yangu. Yani mwezi huu wote nimetumia internet kwenye router ya Tigo naunga wifi kwenye vifaa vingine, router hii ina ukurasa wa kuonyesha kiasi cha data ulichotumia kwa muda wote.
Tarehe 31 mwezi wa tano May mida ya jioni nilimaliza kifurushi line nikaingiza kwenye simu ya kitochi, nika reset router ya Tigo ili ianze upya kabisa kuhesabu matumizi, data used ilikuwa inasoma 0.00 GB, ilipofika saa sita na dakika tatu mesej ikaingia kwenye kitochi nimeungwa gb 80 nikaingiza line kwenye router.
Hatimae leo ni siku ya mwisho ya research yangu.
Tarehe za mwanzo matumizi na salio vinawiana ila tarehe zikisogea taratibu unaanza kuona difference.
Leo siku ya mwisho usiku huu wakati router inaonyesha nimetumia GB 78.440, internet ikawa ngumu kuconeect, hali hii ni kawaida zikibaki MB chache, nilipocheki balance zilikuwa zimebaki MB 28.
Nikarestart router ili nizimalizie hizo MB ila internet ikawa inasua sua, nikaamua nifunge hesabu za research,
screenshot nimeziweka kwenye router matumizi ni GB 78.450, salio ni MB 18.35
View attachment 2674561
View attachment 2674564
Nimefikia muafaka kwamba tigo wanachapa asilimia 0.195x % - almost asilimia 2%
Kupigwa hakuepukiki, siwezi kujutia sana kuchapwa asilimia 2, I can handle it.
Niliwahi kutumia mtandao flani nao wana mabando bei chee ya mwezi, bando la 8 gb lilipukutika baada ya kutumia GB 4.8, sijutii kuchapwa 2%.
Uwaweze habar ya kuchapwa