"Hivi hawa watu wa UDOM hawana kazi au? kila siku UDOM, UDOM tumewachoka bwana na majungu yenu...Wewe huoni haya unatukana mabosi wako wanaokuweka mjini.
Kwa namna ulivyojibu, nadhani mamkwe wewe ni kiongozi na ni mtu mkubwa hapo UDOM. Pia unajua wazi hawa watu wa UDOM wanakazi za kufanya. Unapaswa uende mbali zaidi na ujiulize "kwa nini kila siku watu hao wanazungumzia UDOM?" Kama kiongozi (endapo hisia zangu ziko sahihi) unapaswa kufanya kila uwezalo kuwafanya watu hawa aidha waache kuizungumza UDOM kila siku, au waizungumzie kwa mazuri (yaani wawe positive kama inavyoonesha kwa baadhi yao)
Halafu ondokana na dhana kwamba "viongozi" au "mwajiri" au (nikitumia maneno yako) "mabosi" ndio wanaowaweka waajiriwa mjini (mathalani huyu unayemzungumzia). Hiyo ni dhana potofu kabisa na ndiyo inayoendelea kuitafuna nchi yetu. Viongozi wetu wengi wamefika mahali wakasahau kuwa "uongozi ni dhamana" wakadhani uongozi na taasisi wanazoziongoza ni mali zao au mali za familia au ukoo wao. Mathalani, UDOM sio mali ya yeyote aliye kiongozi leo. UDOM itabaki kuwepo na wote wanaiongoza leo siku moja wataondoka na kubaki historia kwamba fulani na fulani ndio walikuwa viongozi wake waanzilishi. Kila mtanzania (aliye na vigezo na sifa zinazotakiwa kuwa kiongozi wa taasisi kama hiyo ktk ngazi yoyote) anaweza kuwa kiongoza.
Watanzania tukumbuke enzi za mwalimu haya hayakuwepo. Dhana kwamba "bosi" ndiye anayemuweka mwajiriwa wake mjini inaleta hisia kwamba huyo mwajiriwa hakuwa na sifa na vigezo stahiki vya kuwa mwajiriwa katika nafasi husina. Hapo ndipo watu wataanza kujenga hoja za "watu kuajiriwa kwa misingi ya udini, udugu, urafiki, siasa, ukanda n.k, na sio kwa misingi ya sifa na uwezo wa mtu. Siwezi kuwa nimeajiriwa kwa sifa, kuitumikia taasisi katika nchi yangu na watanzania wenzangu halafu ukasema MWAJIRI ndiye anayeniweka mjini...SI KWELI...Huo utakuwa ni upotoshaji mkubwa. Kuajiriwa ni haki ya kila mtanzania ili mradi ana sifa zinazotakiwa. Kufanya kazi katika nchi yangu ni wajibu wa kila raia. Kwa hiyo mamkwe nadhani hapo unaongelea swala la "Haki na Wajibu", SIO kuwekana mjini.
Watanzania tukifika hatua tukalitambua hilo, tutaheshimiana kazini bila kujali mkubwa wala mdogo. Kwa sababu, hata ivo ukweli ni kwamba swala la kuwa kiongozi wakati mwingine ni swala la mda tu. Huyu anayedaiwa kuwekwa mjini na anayeitwa BOSI, si ajabu kesho akawa ndiye BOSI tena.
Rai yangu kwako mamkwe ni kwamba unapaswa kuyatafakari yanayosemwa juu ya UDOM kwa jicho la kiuongozi. Tena uongozi wa taasisi ambayo hata wewe ni mpitaji tuu. Hivyo njia bora ingekuwa kwanza ni kujiridhisha kwamba yanayosemwa hayana ukweli wowote, na usaidie katika kuutoa ukweli huo ili uondoe hisia zao ambazo zitaendelea kuwa za kweli miongozi mwa wenye hisia hizo hadi pale wewe kama kiongozi kwa kushirikiana na viongozi wenzako mtabainisha ukweli wenyewe SIO kwa MANENO tu, na kwa VITENDO pia.