Restaurant gani au wapi wanapika chakula kizuri kwa Dar es Salaam?

Tuliofika Dar kwa sababu ya CHUO tu kwa mama zinduna nyuma ya Mabibo hostel mpango mzima asee 1300/= tulikuwa tunamalizia siku!!!

Typed Using KIDOLE
Nasikia mlikuaga mnavitafuna vibinti vykae. Ni kweli?
 
Hawa wamefunga siku hizi.
Ila pamoja na uzuri wa chakula walikuwa na reasonable price
 
Muanzisha Uzi inategemea unataka chakula cha aina gani. Ukiacha Chef's Pride sehemu nyingine nyingi za kula inategemea ni watu wenye asili ya wapi
Ukienda Zahir, Zitta, Golden Fork, White Rose, Mishi(tmk) utakuta vyakula kama Pilau, Biryan, Wali Nazi, Samaki na kadhaalika vinavutia
Ukienda Break Point, Chang'ombe Village, Rombo Greenview, Mary's, na Miami Ilala hapa utakuta vyakula kama Michemsho, Kuku choma, Nyama choma, Mbuzi Choma, Mtori na Kongoro ndio mwake
Kwa hiyo ukiuliza Restaurant lazima ueleze unapendelea nini ?
Uzuri wa Chef's Pride wanapika vyakula vya aina zote kwa weledi mkubwa sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…