Master Legendary
JF-Expert Member
- Apr 28, 2013
- 576
- 876
Kiukweli hili ni kundi kubwa sana sema kisiasa Wapinzani hawalipi Umuhimu unaostahili.
Kundi hili limeathirika kwa muda mrefu sana toka kipindi cha Magufuli takribani Miaka 10 kuna watu hawajapata Nyongeza yoyote ya maana zaidi ya hizo elf 20 ilihali kiuhalisia Gharama za Maisha zimepanda katika kiwango cha kutisha.
Kuna Mishahara ya Watumishi ambayo ukiambiwa utajiuliza huyu mtu anaishije hupati majibu,wakati huo kuna Mshahara wa Mtumishi wa siku 30 ni posho ya siku moja ya Mbunge, Na sasa hivi kuna Tetesi kwamba Wabunge wamejiongezea Mishahara na Posho zao wenyewe.
Kundi hili lina Maumivu makubwa sana Moyoni na halina Mtetezi kwasababu limekandamizwa sana, na kwasababu ya kuathirika kisaikolojia na kupata Matatizo ya Afya ya akili kundi hili limejaa hofu na haliwezi tena kuacha hiyo kazi ya Utumishi, hata haya mambo mnayoona kwamba kati yao wengine wanatumika kuisaidia CCM ni matatizo tu ya kisaikolojia na hofu ila siyo kwamba wanaipenda CCM.
TUCTA ni kama wamecompromise na wanashirikiana na Dola kuingia Madarakani na kuendelea kukandamiza kundi hili kwasababu kiuhalisia wanajua kinachoendelea ila wamechagua kuwa upande wa Serikali.
Kwasababu Kura ya Mtu iko Moyoni nashauri CHADEMA kwenye Retreat waazimie kulitetea kundi hili kwa nguvu zote wachukue hizo Kura za Moyoni waongeze kujenga Chama chao Mioyoni mwa watu baadae watanishukuru.
Povu linaruhusiwa,nimetega Miamvuli ya kutosha.
Soma: Pre GE2025 - Special Thread: Mijadala na Matukio ya Uchaguzi Mikoa yote Tanzania Bara na Zanzibar kuelekea Uchaguzi Mkuu 2025