Revealed: Government development projects are underfunded

Revealed: Government development projects are underfunded

Hapo kiukweli hali si nzuri na taaluma ya uchumi na fedha BOT,Wizara ya Fedha na TRA inahitajika kutumika ipasavyo.

Kinyume na hivyo hali inaweza kuwa more worse.

Au kuna sabotage mahali maana hata haiingi akilini kabisa ukisoma hiyo taarifa ya Citizen Sunday.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Ukata mifukoni wafikia pabaya
www.ippmedia.com/sw/habari/ukata-mifukoni-wafikia-pabaya

pochi-jpg.437013


Uchunguzi uliofanywa na Nipashe kwa siku kadhaa, umebaini kuwa miongoni mwa waathirika wakubwa wa uhaba huo wa fedha zilizokuwa zikipatikana kirahisi kupitia ‘dili’ nyingi, zilizokuwapo walau mwaka jana kulinganisha na sasa, ni pamoja na wajasiriamali mbalimbali ambao sasa wamejikuta wakiwa katika hali mbaya kiuchumi.

Kwa mujibu wa uchunguzi huo, umebaini kuwa baadhi ya wajasiriamali wamejikuta wakifilisika baada ya biashara zao kuyumba na mwishowe kushindwa kulipa mikopo waliyoipata kutoka benki na taasisi zingine za fedha.

Hatua hiyo imesababisha kutwaliwa mali walizoziweka dhamana, zikiwamo viwanja, majengo kama ya shule na nyumba za makazi, nyumba za kulala wageni, hoteli pia magari.

Aidha, Nipashe imebaini kuwa mbali na wenye benki na taasisi za fedha kupiga mnada mali za wakopaji ili kufidia mikopo waliyoitoa, athari zingine zitokanazo na uhaba wa fedha mifukoni ni pamoja na kuongezeka kwa ulaji wa mboga za majani kulinganisha na nyama choma; baadhi ya wanywaji kuacha pombe rasmi na kugeukia zile za kwenye pakiti za nailoni maarufu kama ‘viroba’ na za kienyeji zinazouzwa bei poa na pia kuyumba na hata kufungwa kwa baadhi ya maeneo maarufu ya starehe.

Tangu Serikali ya awamu ya tano chini ya Rais John Magufuli iingie madarakani, imekuwa ikisisitiza umuhimu wa watu kufanya kazi ili kujiingizia vipato halali na kuachana na mazoea ya kutegemea fedha rahisi kwa mtindo maarufu wa ‘kupiga dili’.

Katika utekelezaji wa jambo hilo, ambalo lengo lake ni kuihakikisha uchumi wa nchi unaimarika kupitia shughuli halali za kiuchumi na kuokoa matumizi holela ya fedha za umma ili mwishowe zitumike kuwanufaisha wananchi wa kawaida kupitia miradi mbalimbali ya maendeleo, hatua kadhaa zimechukuliwa na ndizo zinazoonekana kuchangia kwa kiasi kikubwa kuwapo kwa uhaba wa fedha mitaani.

Miongoni mwa hatua hizo zinazodaiwa kusababisha ukata ni kudhibitiwa kwa matumizi holela ya fedha za umma kupitia warsha, semina, vikao, makongamano, maadhimisho, sherehe na safari za nje.

Aidha, nguvu kubwa imeelekezwa katika kukusanya kodi, hatua ambayo hadi sasa imetibua pia mipango mingi haramu ya kujiingizia fedha katika maeneo kama ya bandari ambako mamia ya makontena yalikuwa yakipitishwa kwenye Bandari ya Dar es Salaam bila kulipiwa ushuru.

Ujanja huo uliwanufaisha wachache huku fedha zingine pia zikiangukia kirahisi kwa watu waliokuwa wakiingia mikataba tata ya kutoa huduma mbalimbali kwa halmashauri za miji, manispaa, wilaya, majiji na hata wizara.

Akizungumza wakati akilizindua Bunge la 11 Novemba 20, mwaka jana, Rais Magufuli alisema zaidi ya Sh. bilioni 356.3 zilitumiwa na Serikali kugharimia safari za nje katika mwaka wa fedha 2013/2014 na 2014/2015, kiasi ambacho wakati huo kingeweza kufanikisha ujenzi wa mtandao wa barabara safi za lami zenye urefu wa kilomita 400.

“Fedha zimepotea mitaani kwa sababu mianya mingi ya kupiga dili imezibwa…matokeo yake, wale waliokuwa wakizitumia bila hiyana kwenye maeneo ya starehe na kuzipa nafasi ya kujaa kwenye mzunguko hivi sasa hawana tena jeuri hiyo,” mmoja wa wafanyabiashara walioyumba kwa sasa kiuchumi baada ya kulazimika kuifunga baa yake jijini Dar es Salaam kutokana na wateja kupungua sana aliiambia Nipashe.

“Mambo yamekuwa magumu kwa sababu serikali imebana maeneo mengi. Kuna watu walikuwa wakiingiza mamilioni kila siku pale bandarini na wengine wamekuwa mamilionea kupitia dili za uuzaji pembe za ndovu na dawa za kulevya.

Wengine walikamata dili za kila mara za kutengeneza vipeperushi, fulana, kofia na bidhaa nyingine nyingi wakati wa maadhimisho ya sherehe mbalimbali.

“Hawa wote, fedha walizokuwa wakipata walizitumia mitaani kwa fujo ikiwa ni pamoja na kuzimwaga kwenye jukwaa wakati wa maonyesho ya bendi za muziki.

Yote hayo yamebaki historia na ndiyo maana baadhi ya biashara zimeyumba sana, alisema.

MINADA YA NYUMBA, MAJENGO

Miongoni mwa dalili za wazi za ukata mifukoni ni kuyumba kwa biashara za wajasiriamali wengi ambao wamepoteza wateja waliokuwa nao ‘enzi za dili’ mwaka mmoja uliopita na sasa kujikuta wakifilisiwa mali zao kwa kasi ya kutisha na taasisi za fedha.

Baadhi ya majengo maarufu yaliyopigwa mnada kwa sababu ya mikopo ya benki hadi sasa ni pamoja na ghorofa la kisasa la hoteli ya Tamal, lililoko Mwenge jijini Dar es Salaam. Jengo hilo liliuzwa katika mnada kwa Sh. bilioni 1.1 huku thamani yake halisi ikitajwa kuwa Sh. bilioni 2.2, chanzo ikiwa ni deni la benki la Sh. bilioni 1.6.

Katika uchunguzi wake, Nipashe ilifuatilia matangazo ya madalali wa benki mbalimbali walioteuliwa kupiga mnada mali za wakopaji walioshindwa kulipa madeni.

Magazeti matatu ya Nipashe, Mwananchi na Habari Leo ndiyo yaliyotumika kufanya mlinganisho wa upigaji mnada wa nyumba na majengo ya wakopaji katika kipindi cha miezi mitatu ya Agosti, Septemba na Oktoba, mwaka huu na mwaka jana.

Matokeo yalionyesha kuwa kwa mwaka jana, nyumba za makazi na majengo 105 yalipigwa mnada kufidia madeni ya benki, lakini kwa mwaka huu, kipindi kama hicho kinaonyesha kuwa mnada ulihusisha kuuzwa kwa nyumba na majengo 405.

Kwa hesabu hizo, maana yake kuna ongezeko la nyumba na majengo 300 yaliyopigwa mnada baada ya wakopaji kushindwa kulipa mikopo yao.

VIWANJA VYALIZWA
Uchunguzi wa Nipashe umebaini pia kuwa viwanja ni miongoni mwa mali zinazoendelea kupigwa mnada kwa kasi na madalali halali wa benki.

Kwa mfano, juzi (Novemba 17, 2016), viwanja 16 vilitangazwa kupigwa mnada na madalali wa benki kupitia gazeti la Habari Leo, chanzo kikiwa wamiliki kushindwa kulipia mikopo yao.

Aidha, katika kipindi cha miezi mitatu ya Agosti, Septemba na Oktoba, mwaka jana, viwanja 15 vilitangazwa kupigwa mnada katika magazeti ya Nipashe, Mwananchi na Habari Leo.

Idadi hiyo imeongezeka mwaka huu hadi kufikia viwanja 127 kutokana na takwimu za matangazo ya madalali kwenye magazeti hayo matatu ndani ya kipindi hicho cha Agosti hadi Oktoba.

Aidha, zaidi ya magari 100 ya wakopaji kwenye benki na taasisi mbalimbali za fedha pia yamepigwa mnada mwaka huu katika kipindi cha Agosti, Septemba na Oktoba .

ULAJI MBOGA, UNYWAJI ‘VIROBA’
Wakati baadhi ya biashara zikipata misukosuko kutokana na kile kinachoelezwa kuwa ni kukosekana kwa fedha za ‘dili’ mitaani, hali ni tofauti kwa biashara nyingine, mojawapo ikiwa ni ya mboga kama mchicha, spinachi, kisamvu, majani ya kunde, mnavu na majani ya maboga.

Katika mahojiano yake na baadhi ya wafanyabiashara wa mboga, Nipashe imebaini kuwa hivi sasa mboga zimekuwa zikipata wateja wengi zaidi kulinganisha na vile ilivyokuwa hapo kabla.

“Kwa kweli biashara hivi sasa imekuwa nzuri. Binafsi naona walaji wa mboga wameongezeka kwa sababu siku za nyuma nilikuwa nikipata wastani wa Sh. 8,000 kwa siku kama faida… lakini hivi sasa nimeongeza mzigo na faida imepanda hadi Sh. 12,000.

Pia kuna siku nyingine napata hadi Sh. 15,000 kwa siku,” alisema mjasiriamali anayetembeza mboga mitaani aliyejitambulisha kwa jina la Mama Jay.

Mam Jay alisema hana uhakika sababu ya wateja wa mboga kuongezeka, lakini amesikia wenzake wakisema miongoni mwa sababu ni pamoja na baadhi ya walaji wakubwa wa nyama na samaki kupunguza bajeti zao katika kununua vitoweo.

Aidha, imebainika kuwa baadhi ya wanywaji wa bia na pombe zingine za bei mbaya, hivi sasa wamegeukia pombe zinazouzwa bei poa, zikiwamo za viroba na za kienyeji kama wanzuki na mataputapu baada ya mifuko yao kukumbwa na ukata.

“Hili liko wazi ndugu yangu… baadhi ya baa siku hizi ni kama hazina watu, tena hata katika tarehe za mwisho wa mwezi.

Hela imetoweka, matokeo yake wengine wamekuwa wateja wakubwa wa viroba na baadhi wanaunga mkono utamaduni kwa kunywa pombe za kienyeji,” mmoja wa wauzaji wa pombe za kienyeji maeneo ya Tandale jijini Dar es Salaam aliiambia Nipashe.

WAFANYABIASHARA WANENA

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wafanyabiashara, Johnson Minja, alikiri kuwa hali ya kifedha imeyumba na kwamba, minada mfululizo inayofanywa na madalali wa benki na taasisi za fedha ni ushahidi kuwa wananchi hawana tena fedha za kutosha mifukoni kununua bidhaa kwa wafanyabiashara kama ilivyozoeleka na matokeo yake ni kuyumba kwa biashara husika na mwishowe kufilisiwa mali pindi mikopo isiporejeshwa kwa kuzingatia mkataba ulioridhiwa baina ya mkopaji na taasisi husika.

“Takwimu za Benki Kuu ya Tanzania (BoT) zimeeleza wazi kuwa hali ya uchumi si nzuri.

Sasa kama BoT inasema hali ya uchumi siyo nzuri, itawezekana vipi mifuko ya wananchi iwe imejaa fedha?” alihoji Minja.

“Hakuna mzunguko wa fedha sokoni. Kama sisi wafanyabiashara tunategemea kuuza na uwezo wa wanunuzi kununua umeshuka.

Unakuta watu walikopa kwenye taasisi za benki ili kuendesha biashara zao lakini mwisho wa siku wanajikuta wanapoteza zaidi baada ya mali zao kupigwa mnada baada ya kushindwa kulipa madeni,” alisema.

Minja alisema kutokana na hali hiyo kuwa mbaya, ni wakati mwafaka sasa kwa Serikali na taasisi za fedha kushauriana namna ambavyo wataweza kumkwamua mwananchi.

“Wito wangu kwa taasisi za fedha ni kwamba lazima waone hali ya sasa ya uchumi ilivyo na waendane nayo kwa sababu haiwekezani mtu akakopa halafu kuwepo na idadi kubwa ya wadeni… wanatakiwa kuliangalia suala hili kwa mapana yake badala ya kujinufaisha wenyewe,” alisema.

WENYE BENKI WASEMA “NO WAY”

Mmoja wa maofisa wa juu katika benki moja kubwa nchini aliiambia Nipashe kuwa pamoja na kutambua kwao kuwa mzunguko wa fedha umeyumba hasa baada ya Serikali pia kuamua kupeleka fedha za taasisi zake BoT, bado wanakosa namna nyingine ya kurudisha fedha walizowakopesha watu bali kufuata kile walichokubaliana wakati wakiwapatia.

“Ni kweli urejeshaji mikopo umepungua kwa sababu baadhi ya biashara za wateja wetu zimeyumba… lakini katika hili hakuna namna. Kila mtoaji mkopo lazima afuate taratibu zilizopo kuhakikisha kuwa anarudisha chake.

Ndivyo na sisi tunavyofanya… No way (hakuna namna), kwa sababu vinginevyo na hizi taasisi za fedha pia zitakufa,” alisema ofisa huyo wa juu wa benki sharti la kutoandikwa jina kutokana na sababu za kibiashara.

*Imeandaliwa na Romana Mallya, Thobias Mwanakatwe
 
Narudia tena Uchumi liwe somo la lazima....Ukisoma uchumi topic ya kwanza kabisa ni Choice and scale of preference....Scarcity and Economic problems.....hakuna hata siku moja utaacha kuwa na economic problems ambazo kutatua lazima ufanye choice hii yote ni kwa sababu wants are unlimited....umeelewa...tatizo wengi mkakimbilia kusoma HKL mnaona mnavyotupa shida kuwaaelewesha...mtaani wanaosema hawapati ajira za ualimu wamesoma HKL/HGK wakati mashuleni walimu wa hayo masomo wamejaa, unakuta shule moja inawalimu wa History 40 wakati wanafunzi ni 200 shule nzima, walimu kama hawa watasota tu mtaan
usitukane mamba wakati MTO hujavuka , kesho ZAmu yako kufukuzwa kazi ili tubane matumizi
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Hiki ndiyo kitu cha kushangaza sana Mkuu. Huyu Majaliwa kakazana kusema uongo hadharani kwamba uchumi wa nchi ni mzuri pamoja na kuwa there is so much evidence out there to show that Tanzani's economy is in very bad shape. Anaendelea kusema uongo kwa faida ya nani? Hivi wanadhani Watanzania wote ni wapu.mbavu tukubali uongo wa hii Serikali wakati hali halisi ya uchumi tunaijua!? Lini wataamua kuwa wakweli kuhusu hali ya uchumi wa nchi yetu!?
Mkuu BAK heshima Kwako

Mimi na wewe sana tunakuta hapa jukwaani, na mirengo yetu iko sawa Kila mara,
Huyu majaaliwa anajua mfalme anataka kusikia mapambio gani, Ndio sababu habadilisha aina ya mapambio kama anavyofanya makonda,
Ila siku zote huwa nasema hapa namba huwa haidanganyi, Muda huwa ni jibu tosha kwa Kila ulaghai, tuombe uzima tu
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Inashangaza sana Mkuu kuona huyo jamaa ambaye kuwa ndiye "msomi" kuliko Marais wote wa awamu nne zilizopita kuwa na maamuzi ya ajabu kiasi hiki halafu kujiona yeye ndiye anayejua kila kitu hata pale ambapo namba zinaonyesha ukweli wa hali halisi. Ni kweli tuombe uzima Mkuu labda kuna siku atakuja kukubali kwamba maamuzi yake mbali mbali tangu aingie madarakani yameuagusha uchumi wa Tanzania kwa kasi ya kutisha. Tuendako Mkuu kama nchi kumetanda giza nene la kutisha.

Mkuu BAK heshima Kwako

Mimi na wewe sana tunakuta hapa jukwaani, na mirengo yetu iko sawa Kila mara,
Huyu majaaliwa anajua mfalme anataka kusikia mapambio gani, Ndio sababu habadilisha aina ya mapambio kama anavyofanya makonda,
Ila siku zote huwa nasema hapa namba huwa haidanganyi, Muda huwa ni jibu tosha kwa Kila ulaghai, tuombe uzima tu
 
Kama hazipikwi Mkuu kwanini basi Serikali itoe 387 billion tu(46.9% ya pesa zilizostahili kutolewa) badala ya 824 billion zilizostahili kutolewa tofauti ya 437 billioni? Kwanini wanashindwa kulipa deni la bilioni 100 kwa MSD ili kuondoa upungufu wa madawa muhimu nchini? Kwanini idadi ya waliopata mikopo ya elimu ya juu mwaka huu imepungua sana ukilinganisha na ile ya mwaka wa fedha 2014/2015? Kwanini wanashindwa kuajiri zaidi ya mwaka sasa na pia kuongeza mishahara na kuwapa promotions zao wote wanaostahili kupata promotions Serikalini?

Je,taarifa za TRA za kukusanya na kuvuka malengo ni za kupikwa???[emoji15] [emoji15] [emoji15]
 
Kama hazipikwi Mkuu kwanini basi Serikali itoe 387 billion tu(46.9% ya pesa zilizostahili kutolewa) badala ya 824 billion zilizostahili kutolewa tofauti ya 437 billioni? Kwanini wanashindwa kulipa deni la bilioni 100 kwa MSD ili kuondoa upungufu wa madawa muhimu nchini? Kwanini idadi ya waliopata mikopo ya elimu ya juu mwaka huu imepungua sana ukilinganisha na ile ya mwaka wa fedha 2014/2015? Kwanini wanashindwa kuajiri zaidi ya mwaka sasa na pia kuongeza mishahara na kuwapa promotions zao wote wanaostahili kupata promotions Serikalini?
Maswali magumu.
Hukuti team Lumumba wanajibu hoja kama hizi. Binafsi nakubaliana na wanaosema uchumi wa nchi yetu umeyumba sana, kwa sababu ushahidi wa kimazingira (sio wa takwimu za kupikwa) tunao. Arrears ambazo JK na utaawala wake walikuwa wanazilipa kwa wakati sasa zimesitishwa, eti hadi uhakiki wa watumishi hewa uishe. Hizi zoezi gani linachukua mwaka mzima? Ilhali serikali ina wafanyakazi wasiozidi 500,000?
 
Kama hazipikwi Mkuu kwanini basi Serikali itoe 387 billion tu(46.9% ya pesa zilizostahili kutolewa) badala ya 824 billion zilizostahili kutolewa tofauti ya 437 billioni? Kwanini wanashindwa kulipa deni la bilioni 100 kwa MSD ili kuondoa upungufu wa madawa muhimu nchini? Kwanini idadi ya waliopata mikopo ya elimu ya juu mwaka huu imepungua sana ukilinganisha na ile ya mwaka wa fedha 2014/2015? Kwanini wanashindwa kuajiri zaidi ya mwaka sasa na pia kuongeza mishahara na kuwapa promotions zao wote wanaostahili kupata promotions Serikalini?
Nchi hii imewekwa rehani...[emoji15]
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Kama hazipikwi Mkuu kwanini basi Serikali itoe 387 billion tu(46.9% ya pesa zilizostahili kutolewa) badala ya 824 billion zilizostahili kutolewa tofauti ya 437 billioni? Kwanini wanashindwa kulipa deni la bilioni 100 kwa MSD ili kuondoa upungufu wa madawa muhimu nchini? Kwanini idadi ya waliopata mikopo ya elimu ya juu mwaka huu imepungua sana ukilinganisha na ile ya mwaka wa fedha 2014/2015? Kwanini wanashindwa kuajiri zaidi ya mwaka sasa na pia kuongeza mishahara na kuwapa promotions zao wote wanaostahili kupata promotions Serikalini?
Au la wachina wanamiliki sehem kubwa ya serikali,haiwezekani Kwa uchakachuzi huu.
 
  • Thanks
Reactions: BAK
Sidhani kama ni Pigo sana maana miaka yote tulikuwa tunashauriana wenyewe kwa wenyewe kuwa tusitegemee sana kazi za kuajiliwa... wengine waliweza kujiongezea vipato wakafanikiwa na wengine waliweza hata kuacha kazi zao nzuri na kijukita kwenye issue tofauti... Sasa nadhani ndio tunaelekea hali ngumu na kila hali ngumu imtokeapo mtu ile akili ya asili hufunguka ili aendelee kuishi akili hizo sometimes huwa zinatuma vizuri au vibaya mbaya ni uwizi.. Nchi zilizoendelea zimepita kwenye vipindi hivi matokeo yake wakavumbua njia nyingi za kuwawezesha kuishi kwa maisha ya hali ya juu sana... ila wenzetu walikuwa na elimu sio sisi elimu za kuajiliwa unasomea hiki unaenda kufanyia kazi kingine....

Kwa Nchi kama Yetu am sure tutaabika Sana... Huyu Baba Speed yake kaikosea hesabu so mwishowe Engine itaknock tu maana hatizami kama Oil hamna.... Unakusanya kodi kwa watu wasio na kitu... atatufunga tu ajue kama mimi Load Licence ya Basi langu moja nililolikata kata sitolipa aminia...

Kuhusu Ushauri huyu Baba yetu wa sasa haambiliki na ukiweka Ushauri unashambuliwa na wapambe hii inaonesha wapambe kweli ni Nuksi... Kiufupi nataka Jamaa aumbuke sana kwa aina yake ya kuendesha Nchi... Tushapoteza vyetu vingi hivyo we have nothing to loose wala kuogopa... tumebanwa kila kona... Mikutano,Maandamano,Kwenye vyombo vya Habari... makazini yaani acha tu... Mkombozi wa Tanzania Atatoka Nje ya Tanzania
We're together brother!
 
Mbona TRA wanasema makusanyo yameongezeka?
Kwani tangia baba jesca afike mahali pale Kuna anayesema hali ni mbaya?

Subutu: kila mtu lazima asifie hata kama Kuna hatari mbele Yake,hii yote ni kutetea matumbo yao yasitetemeshwe.


Huku mitaani hali ni mbaya sana.
 
Back
Top Bottom