Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Naona tatizo lipo hapa.
Mkuu wangu siku nyingine jitahidi kufwata hii kanuni[emoji116]

9. Epuka kumhonga mchumba vitu vya thamani kubwa, kumsomesha nk.
Usiwekeze Sana kwa mchumba. Lakini Kama unadhani uchumba ukivunjika hutaumia mpe ila Kama unaona uchumba ukivunjika utaumia usimpe.

Simaanishi wachumba wasisaidiane, kuna viwango vya kusaidiana wachumba. Mengine hayo ukitaka kuyafanya weka ndani.

Sent using Jamii Forums mobile app
Huyu jamaa ndo atakua role model wangu nkiwa mkubwa

Hamna kuuendekeza upuuzi shubaamit!!
 
Kwani ye ndio wa kwanza kudhurika???
Wengi sana wamedhurika...atapata haki yake mbinguni
[emoji23][emoji23][emoji23]
Kumbe ataipata mbinguni haki yake.
Ni kweli kabisa ataipata mbinguni maana Mungu anajudge kwa haki.

Ikiwa huko mbinguni watu hupata stahiki zao,Je,kulikuwa na haja gani ya yeye kumlipa huyo dada kwa wakati huu tukiwa duniani?
Kwanini asimuachie Mungu tu amlipe huko mbeleni?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Huyu jamaa ndo atakua role model wangu nkiwa mkubwa

Hamna kuuendekeza upuuzi shubaamit!!
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu Mimi sisapoti upuuzi.
Nachukia sana upuuzi na huwa nakararishwa na watu wanaofaya upuuzi.

Lakini kwenye kulipa upuuzi ndipo hapo tunapopishana,,kazi ya kulipa ni ya Mungu,siyo yetu wanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
MREJESHO....

Naomba kwanza niwaombe radhi wote mliokuwa mnasubiria mrejesho hadi mkachoka, niwashukuru pia wale waliokuja PM kunishauri na polen maana ushauri wenu haukuzingatiwa.

Tarehe 07 january kila mwaka itakuwa ni siku yangu ya kumbukumbu.

Kwanza nianze kwa kusema kisasi ni haki ya mtu aliyefanyiwa ubaya pasipo yeye kufanya ubaya, siku tajwa hapo juu ni siku niliyeachana na mwanamke wangu ambaye ndo tulikuwa kwenye hatua muhimu za kuoana, mwanamke aliyenifanyia ushenzi wa kishenzi na mim nikawa sina namna zaidi ya kumfanyia ushenzi wa kishenzi kama yeye.

Siku ilianza vema kwa safari ndefu kuelekea kwa wazazi wake, nikiwa na mshenga na mzazi wangu na baadhi ya ndugu, njian stori zilikuwa za kunipongeza kwa kuchukua uamuzi huu wa kuoa, wakati wote mim nilikuwa kimya nikizid kutafakari zaid jinsi nitakavyopeleka kilio kikuu kwa yule binti, nikiri kwamba nilifikiria pia kuhusu wazazi wake na wangu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki watakaokuwepo ila bad luck ni kwamba option ilikuw moja tu.

Majira ya saa 2 hv usiku tukawasili nyumbani kwa binti, tulipokelewa kwa bashasha na shamra shamra sana, tukapikiwa chakula kisha tukapelekwa sehemu ya kupumzika na kesho saa 4 asubuhi ikawa ndo muda muafaka wa tukio la mahari ili pia sisi tuweze kurudi mapema.

Asubuhi ilikucha vema sana, nikiwa nimeprint messages zote na zile picha tayari kwa kumpiga mtu tukio, muda wa kwenda sehemu iliyoandalia ya mazungumzo ukafika, kama mnavyojua muoaji huwa anaitwa mwishoni baada ya wazee kukabidhiana mahari waliyokubaliana, ikabidi mimi niombe kuvunja utaratibu kwa kuomba niwepo kwenye kutoa mahari hiyo km haitakuwa shida sana, mshenga akasema sio shida inawezekana tu, kweli niliruhusiwa na mshenga akapiga maneno maneno pale ikawa uwepo wangu pale wala sio shida.

Baada ya kukaribishwa na upande wa kikeni ukafika muda wetu sasa wa kujimwambafy kwa kutoa mpunga then taratibu zingine zifuate hapo mim nikainterven kwa kuomba niongee kdg, baba wa binti akasema niruhusiwe maana ile ni kwa ajili yetu, basi nikaomba binti aitwe pale kwenye kikao, ni km walitaka kudadisi kitu ila mim nikaomba binti aje kabla hatunaendelea, niliongea politely sana wala sikuwa na hasira, binti akaitwa na kumbe alikuwa kwenye kuandaa chakula hivyo ikabidi akimbie bafun faster kisha akaja.

Pamoja na wazazi wa binti lakin pia kulikuwa na wajomba, baba wadogo shangazi yake mmoja na kaka zake. Sikua na maneno mengi nikasema straight tu, nimeghairi kuoa na mahari isilipwe na nimeona niliseme hili mbele ya binti na kikao hiki kikubwa ambacho kinahusisha familia zote mbili, watu wakabaki na butwaa, walitaman kuhis nimechanganyikiwa lakin kwa jinsi nilivyokuwa naongea ikabid wafute hayo mawazo, wakawa buzy sasa kunisikiliza.

Nikamwita binti kwa jina lake, nikamuomba binti aweke wazi kila kitu pale kuhusiana nayeye kuwa na mwanaume mwingine, mama wa binti jasho likamtoka akaanza kumuuliza binti yake km ni kweli alikuwa anafanya ushenzi ule, binti akakana akasema sio kweli na hajawahi kujihusisha na mwanaume yeyote tangu nimchumbie huku machozi yanamtoka akaanza kuapa kwa majina yote ya mungu wake, akaanza kujifanya anataja vifungu vya biblia, asee walokole ni wanafiki nafiki sana.

Kikao kikawa kimebadilika sura, kila mtu akabaki ana hamu ya kuujua ukweli, mshenga akaniita tutoke nje kidogo nikakataa, nikamwambia binti aache kupretend aseme ukweli, akaendelea kukataa pale, basi baba wa binti akasimama akasema yeye km mzazi wa binti na mkuu wa ile familia ile ni aibu kubwa na km nitashindwa kuthibitisha basi ataenda kwenye vyombo vya sheria kudai fidia ya binti yake, kwanza ya kumpotezea muda na pili ya kumdhalilisha na kumuumiza kisaikolojia binti yake.

Baada ya kuona binti anakomaa kwamba sio kweli na mzee wangu akawa yupo tu haelewi aseme nini sasa, nikazama kwenye begi na nikatoa picha na printing za screenshots za msg, nilikuwa nazo za kutosha, nikamkabidhi mzee wake nyingine nikampa yeye mwenyewe na zingine mshenga wangu, nikamwambia aendelee kubisha sasa, kukawa kimya kwa muda baadaye binti akakosa nguvu akaanguka na kuzimia, ikabidi akambizwe hospital.

Baba yangu alinilaumu sana kwa kitendo kile, hata mshenga akasema nilitakiwa niseme mapema tungepiga simu tu kwamb tumeahirisha kuliko nilichokifanya, nikawajibu tu moyo wangu usingeridhika kufanya kirahis vile lakn pia binti angepata nafasi ya kuwaongopea wazazi wake na wangemwamin kwa kuwa ni binti yao, namim kwa wazazi wa yule binti ningebaki kwenye kumbukumbu mbaya milele, nikawaomba wanielewe tu hakuna namna.

Ikapangwa jion tuwe ni kikao tuone nini kinafuata sasa.

ITAENDELEA...

Mrejesho: Sehemu ya pili
HUU NDIO UANAUME.

Ungesema uyamalize.kimya kimya..Uongo wake wangeuamin sanaa na wewe ungeonekana mkosaji

UONGO USIUACHR UWE MKUBWA


UBAYA UBAYA

JICHO KWA JICHO


BIG UP MKUUUU MAAMUZI YA KIUME


pengine kuna dada anafanya huu ujinga, hivo basi kwa kusoma hili tukio, kamoyo kake kataanza badilika

Alaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
 
Kwamba atapata ajali kweli?..acheni upuuzi"kwa sauti ya mleta mada"

Sent using Jamii Forums mobile app
Jamaa hajasema kwamba atapata ajali kweli.
Mimi sijasema kwamba atapata ajali kweli.

Jamaa amesema kwamba maneno huumba
Na mimi nimesema kuwa kusingizia mambo ya ajali si vizuri.

Hakuna sehemu tumesema atapata ama hatapata,acha upuuzi[emoji23][emoji23](in Koroe's voice)

Sent using Jamii Forums mobile app
 
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Mkuu Mimi sisapoti upuuzi.
Nachukia sana upuuzi na huwa nakararishwa na watu wanaofaya upuuzi.

Lakini kwenye kulipa upuuzi ndipo hapo tunapopishana,,kazi ya kulipa ni ya Mungu,siyo yetu wanadamu.

Sent using Jamii Forums mobile app
Vyovyote vile iwavyo

Inabidi alichofanya uyu mwamba kiingizwe kwenye mtaala wetu wanaume vijana wapatiwe misingi ili heshima iwepo mtaani huku

Maana Kuna watu wakiona unampenda basi unaonekana boya sasa tiba yao hao wapuuzi imepatikana huu ushuuda wa jamaa ni mwongozo tosha kabisa tutaelewana tu
 
HUU NDIO UANAUME.

Ungesema uyamalize.kimya kimya..Uongo wake wangeuamin sanaa na wewe ungeonekana mkosaji

UONGO USIUACHR UWE MKUBWA


UBAYA UBAYA

JICHO KWA JICHO


BIG UP MKUUUU MAAMUZI YA KIUME


pengine kuna dada anafanya huu ujinga, hivo basi kwa kusoma hili tukio, kamoyo kake kataanza badilika

Alaaaa[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]
Halafu ukute wewe ndio yule mwamba ulikuwa ukimchatisha binti wa jamaa kule fb[emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787][emoji1787].

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mwanamke anayetunzwa na mumewe kwa kiasi kikubwa hana haki hata 0.0002 ya kuchepuka..ni either aombe takala au akimbie ndoa ili akafanye kwa kujinafasi huko kwa huyo mwingine..the same applies to wachumba walioko kwenye stage ya mwisho ya kuingia ndoani..ni bora uvunje uchumba.

Mwanaume anayeweza kuvumilia usaliti wa hivi ni mpumbavu.
 
TUENDELEE...


Nikaona mambo yasiwe mengi, nikamwambia poa aende akamrudishe rafiki yake kwenye ndoa yake and mimi nitamfkiria kuhusu ombi lake, nilishajua tayari ashakuwa dhaifu kwangu so hawezi kunizid maujanja, hata km anasema uongo bado hauwez kuniathiri maana lazima nimzid akili, kwanza ananipenda kimapenz hivyo tayari yupo kwenye ugonjwa wa akili hawezi kushindana namimi mwenye akili timamu, and nikapanga kabisa kwamba siwezi kuwa naye yule manzi.

Akaenda akamdanganya kwamba nimepata ajali na nina hali mbaya nimekimbizwa India, na kwa jinsi hali ilivyo sijui km nikipona nitabaki na uwezo wa kufanya chochote Kwahiyo akamwambia rafiki yake akakomae tu na ndoa yake, na akaishi na yule mwanaume maana kwangu tena maji yameshamwagika, binti akaona hakuna jinsi akarudi kwa mume wake, jamaa ndo hivyo akampokea maana ndo km anakopatia ridhiki, nasikia kumbe kipindi anakuja huku alikuwa tayari kanasa ujauzito wa mshikaji, ndo huyu rafiki yake akawa ananiambia alikuja kugundua baadaye km ni mjamzito means km mimi ningejichangnya kuwa naye kipind hiki basi ningetupiwa hilo zigo kumbe la mume wake huko.

Japo binti hana amani kwenye ndoa ile so dizain km anapanga mbinu amtoroke aende akaishi maisha yake peke yake. Huyu rafiki yake akaniambia yupo kwenye process ya kutoa ile mimba maana hataki kuzaa na mshkaji wake, then apotee kokote akaishi mwenyewe. By the way hainuhusu hiyo sasa, azae asizae, aishi au aondole anajua yeye.

Maisha yangu yameanza upya na dizain km yule demu karidhika na kuamin kwamba sipo nchini nipo India kwa matibabu, maana baadaye ikanilazimu nibadili tena namba za simu, sasa mtihan ninao kwa huyu rafiki yake maana ananipenda na anataka nitimize ahad maana kazi ameshaifanya. Hadi leo sijamla na sitamla, na hili kwangu ni dogo sana na nitalimaliza tu kirahisi.

Nimepata aman sana na sikumbuki ubaya na maumivu yote aliyonitendea yule binti, nimeridhika kwa hiki.

Yapo mambo mengine nimeyaexclude maana stori ingekuwa ndefu sana, ahsanten kwa kunifuatilia tangu mwaka 2017 hadi leo 2021.

MWISHO,
Ningekuwa na roho kama yako ningefurahi sana. Aisee mkuu nakuonea wivu walahi.... Wewe umebarikiwa asee kwenye uanaume umetimia 100%
 
Vyovyote vile iwavyo

Inabidi alichofanya uyu mwamba kiingizwe kwenye mtaala wetu wanaume vijana wapatiwe misingi ili heshima iwepo mtaani huku

Maana Kuna watu wakiona unampenda basi unaonekana boya sasa tiba yao hao wapuuzi imepatikana huu ushuuda wa jamaa ni mwongozo tosha kabisa tutaelewana tu
[emoji23][emoji23][emoji23]
Kwahiyo unapingana na maagizo ya Mungu juu ya kisasi?

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Unajua mimi sikubaliani na binti kufanya usaliti,amefanya udanganyifu na udanganyifu ni dhambi.
Na jamaa alikuwa na haki ya kumuacha kabisa, hata ingekuwa mimi..mtu msaliti siwezi kuendelea naye hata iweje.

Shida ni namna alivyomuacha,
Kulikuwa kuna haja gani ya kwenda kumdharirisha hivyo?
Kwanini asimuonyeshe tu vithibitisho na kumuacha pasi na kwenda hadi kwao kama baba yake alivyosema kwamba kwanini hakusema tu ili wapige simu kwamba hawataenda kuonekana.

Namna alivyomuacha ndicho kitu tunakiongelea hapa.
Imemgharimu binti na matokeo yake hayo madhara naye anaanza kuyasuffer..si yeye kwamba yupo salama.

Sent using Jamii Forums mobile app
Alikuwa hana budi kuthibitisha umma ujue uchafu wa binti..kama mbele ya watu binti aliambiwa aeleze wazi alikuwa na mahusiano na raia gani akagoma kuwa mkweli vipi kama angembiwa kimya kimya..nani angesadiki kama ni kweli binti mlokole anafanya uhuni huo

Hakuna ambaye angemuamini jamaa kama anasema ukweli..hiyo ndio dawa yake msaliti amefanya kichakani unumuumbua hadharani tena naona kama jamaa ana moyo wa upole sana adhabu zangu ninazotoa kwa huyu mwamba naweza kusema kwangu ni mwanafunzi wa chekechea
 
Mwanamke anayetunzwa na mumewe kwa kiasi kikubwa hana haki hata 0.0002 ya kuchepuka..ni either aombe takala au akimbie ndoa ili akafanye kwa kujinafasi huko kwa huyo mwingine..the same applies to wachumba walioko kwenye stage ya mwisho ya kuingia ndoani..ni bora uvunje uchumba.

Mwanaume anayeweza kuvumilia usaliti wa hivi ni mpumbavu.
Cha ajabu mnaotoa haya maneno nyie wenyewe ni wachepukaji wazuri.
Mngekuwa waaminifu kama mtoa mada angalau maneno yenu yangesound ukweli.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Alikuwa hana budi kuthibitisha umma ujue uchafu wa binti..kama mbele ya watu binti aliambiwa aeleze wazi alikuwa na mahusiano na raia gani akagoma kuwa mkweli vipi kama angembiwa kimya kimya..nani angesadiki kama ni kweli binti mlokole anafanya uhuni huo

Hakuna ambaye angemuamini jamaa kama anasema ukweli..hiyo ndio dawa yake msaliti amefanya kichakani unumuumbua hadharani tena naona kama jamaa ana moyo wa upole sana adhabu zangu ninazotoa kwa huyu mwamba naweza kusema kwangu ni mwanafunzi wa chekechea
Huyo binti mlokole na kama kweli ameokoka na Roho mtakatifu yupo ndani,,nafsi ingemshuhudia tu!
Hakuna haja ya kutumia nguvu kubwa kutoa proof... Mungu huwa anawasuta watu nafsini.

Kwani kama hujafanya kitu na unajua kama unafanya na Mungu anajua hujafanya ila watu wanabisha na kukutuhumu kuwa umefanya..
Ikiwa Mungu mwenyewe anaujua ukweli na anakuamini,kwanini uwajali watu ambao hawaamini ?


Nje ya mada:
Tuhadithie visa vyako mkuu,tuone na tujifunze.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Back
Top Bottom