Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Revenge: Napeleka kilio kwa binti fulani siku ya kupeleka barua

Safi sana Mkuu KOROE wewe upo kama 100% ila mimi nimekuzidi kidogo. Mimi ningeshusha na kipigo ili kuweka alama ambayo ataikumbuka milele ningekata hata sikio moja ili kila akijiangalia kwa kioo akumbuke! Ulitakiwa umalize na kipigo cha Mbwa Koko
Loohh!!!
 
Na umemkuta tu huyo demu ni mhuni ila yuko soft hearted mwingine wala asingejali.na hizo drama zako za kupeleka picha kwa wakwe
tena ndo ungeumia balaa!
Ningekua mimi ningekujibu yes nilichepuka na yule ulieona text zake coz nampenda yule sio wewe na afadhali umejua ili tuachane!
Ungenyooka tu!hizo korean drama usijaribu pelekea wengine hutaamin macho yako!
Unajidai kusema hvyo ila hujui kuhusu binadam na ndo maana unaongea upuuzi tu, au we ni malaya anaejiuza ndo mana huna staha,
Huwez sema hvyo kwa mtu.uliemtambulisha kwa wazaz wake na huwez kuacha dhahabu kwa kumpamba mtu usiempenda na mwenye familia kama unampenda zaid, na hakuna kibaya zaid kama kukatisjwa ghafla moyo wa furaha, inachanganya moyo ghafla,
Mfano mzr ni kipind mko shule mshamaliza mitihan mmekaa shule wiki mkingojea matokeo mwende hom, ghafla cku ya mwisho kukaa shule mnaambia mmeongezwa wiki
 
MREJESHO....

Naomba kwanza niwaombe radhi wote mliokuwa mnasubiria mrejesho hadi mkachoka, niwashukuru pia wale waliokuja PM kunishauri na polen maana ushauri wenu haukuzingatiwa.

Tarehe 07 january kila mwaka itakuwa ni siku yangu ya kumbukumbu.

Kwanza nianze kwa kusema kisasi ni haki ya mtu aliyefanyiwa ubaya pasipo yeye kufanya ubaya, siku tajwa hapo juu ni siku niliyeachana na mwanamke wangu ambaye ndo tulikuwa kwenye hatua muhimu za kuoana, mwanamke aliyenifanyia ushenzi wa kishenzi na mim nikawa sina namna zaidi ya kumfanyia ushenzi wa kishenzi kama yeye.

Siku ilianza vema kwa safari ndefu kuelekea kwa wazazi wake, nikiwa na mshenga na mzazi wangu na baadhi ya ndugu, njian stori zilikuwa za kunipongeza kwa kuchukua uamuzi huu wa kuoa, wakati wote mim nilikuwa kimya nikizid kutafakari zaid jinsi nitakavyopeleka kilio kikuu kwa yule binti, nikiri kwamba nilifikiria pia kuhusu wazazi wake na wangu pamoja na ndugu, jamaa na marafiki watakaokuwepo ila bad luck ni kwamba option ilikuw moja tu.

Majira ya saa 2 hv usiku tukawasili nyumbani kwa binti, tulipokelewa kwa bashasha na shamra shamra sana, tukapikiwa chakula kisha tukapelekwa sehemu ya kupumzika na kesho saa 4 asubuhi ikawa ndo muda muafaka wa tukio la mahari ili pia sisi tuweze kurudi mapema.

Asubuhi ilikucha vema sana, nikiwa nimeprint messages zote na zile picha tayari kwa kumpiga mtu tukio, muda wa kwenda sehemu iliyoandalia ya mazungumzo ukafika, kama mnavyojua muoaji huwa anaitwa mwishoni baada ya wazee kukabidhiana mahari waliyokubaliana, ikabidi mimi niombe kuvunja utaratibu kwa kuomba niwepo kwenye kutoa mahari hiyo km haitakuwa shida sana, mshenga akasema sio shida inawezekana tu, kweli niliruhusiwa na mshenga akapiga maneno maneno pale ikawa uwepo wangu pale wala sio shida.

Baada ya kukaribishwa na upande wa kikeni ukafika muda wetu sasa wa kujimwambafy kwa kutoa mpunga then taratibu zingine zifuate hapo mim nikainterven kwa kuomba niongee kdg, baba wa binti akasema niruhusiwe maana ile ni kwa ajili yetu, basi nikaomba binti aitwe pale kwenye kikao, ni km walitaka kudadisi kitu ila mim nikaomba binti aje kabla hatunaendelea, niliongea politely sana wala sikuwa na hasira, binti akaitwa na kumbe alikuwa kwenye kuandaa chakula hivyo ikabidi akimbie bafun faster kisha akaja.

Pamoja na wazazi wa binti lakin pia kulikuwa na wajomba, baba wadogo shangazi yake mmoja na kaka zake. Sikua na maneno mengi nikasema straight tu, nimeghairi kuoa na mahari isilipwe na nimeona niliseme hili mbele ya binti na kikao hiki kikubwa ambacho kinahusisha familia zote mbili, watu wakabaki na butwaa, walitaman kuhis nimechanganyikiwa lakin kwa jinsi nilivyokuwa naongea ikabid wafute hayo mawazo, wakawa buzy sasa kunisikiliza.

Nikamwita binti kwa jina lake, nikamuomba binti aweke wazi kila kitu pale kuhusiana nayeye kuwa na mwanaume mwingine, mama wa binti jasho likamtoka akaanza kumuuliza binti yake km ni kweli alikuwa anafanya ushenzi ule, binti akakana akasema sio kweli na hajawahi kujihusisha na mwanaume yeyote tangu nimchumbie huku machozi yanamtoka akaanza kuapa kwa majina yote ya mungu wake, akaanza kujifanya anataja vifungu vya biblia, asee walokole ni wanafiki nafiki sana.

Kikao kikawa kimebadilika sura, kila mtu akabaki ana hamu ya kuujua ukweli, mshenga akaniita tutoke nje kidogo nikakataa, nikamwambia binti aache kupretend aseme ukweli, akaendelea kukataa pale, basi baba wa binti akasimama akasema yeye km mzazi wa binti na mkuu wa ile familia ile ni aibu kubwa na km nitashindwa kuthibitisha basi ataenda kwenye vyombo vya sheria kudai fidia ya binti yake, kwanza ya kumpotezea muda na pili ya kumdhalilisha na kumuumiza kisaikolojia binti yake.

Baada ya kuona binti anakomaa kwamba sio kweli na mzee wangu akawa yupo tu haelewi aseme nini sasa, nikazama kwenye begi na nikatoa picha na printing za screenshots za msg, nilikuwa nazo za kutosha, nikamkabidhi mzee wake nyingine nikampa yeye mwenyewe na zingine mshenga wangu, nikamwambia aendelee kubisha sasa, kukawa kimya kwa muda baadaye binti akakosa nguvu akaanguka na kuzimia, ikabidi akambizwe hospital.

Baba yangu alinilaumu sana kwa kitendo kile, hata mshenga akasema nilitakiwa niseme mapema tungepiga simu tu kwamb tumeahirisha kuliko nilichokifanya, nikawajibu tu moyo wangu usingeridhika kufanya kirahis vile lakn pia binti angepata nafasi ya kuwaongopea wazazi wake na wangemwamin kwa kuwa ni binti yao, namim kwa wazazi wa yule binti ningebaki kwenye kumbukumbu mbaya milele, nikawaomba wanielewe tu hakuna namna.

Ikapangwa jion tuwe ni kikao tuone nini kinafuata sasa.

ITAENDELEA...

Mrejesho: Sehemu ya pili

Mamamamamamae wewe sasa ndo mwanaume na nusu kama wasemavyo vijana wa istagram
Hard decisions tu k*m*nyok* unathaminiwa unaleta ujuaji tunadeal na wewe jinsi unavyokuja.
 
We chepuka tu kisha mumeo ajue ndio uje utusimulie,.

Mimi ilinitokea tena kwa mke niliefunga nae ndoa na kumsomesha chuo. Ni ishu ya miaka mitano huko nyuma lakini hasira zangu hata hapa naona zinataka kujirudia upya. Inatosha Siendelei kukuhabarisha.
pole sana mkuu
Tena mtu unayemthamini ujue amechapwa au anachapwa ki lose ball inauma sana
 
Unajidai kusema hvyo ila hujui kuhusu binadam na ndo maana unaongea upuuzi tu, au we ni malaya anaejiuza ndo mana huna staha,
Huwez sema hvyo kwa mtu.uliemtambulisha kwa wazaz wake na huwez kuacha dhahabu kwa kumpamba mtu usiempenda na mwenye familia kama unampenda zaid, na hakuna kibaya zaid kama kukatisjwa ghafla moyo wa furaha, inachanganya moyo ghafla,
Mfano mzr ni kipind mko shule mshamaliza mitihan mmekaa shule wiki mkingojea matokeo mwende hom, ghafla cku ya mwisho kukaa shule mnaambia mmeongezwa wiki
Wala usifafanue sana mkuu huyo hajielewi yaani mbele ya wazazi wako,wakwe wajomba shangazi mshenga utasema yes nimechepuka na nilikuwa naenda kutoa tigo kama ni kweli ungesema hivo hata hatua ya kutambulishwa wewe usingeifikia
 
Kuna watu humu wananiita mimi katili lakin wanasahau ukatili niliifanyiwa na huyu binti, mazee huyu binti nimewahi kumpa million 1 na laki 2 kwaajili ya kumsaidia kweny msala fulan, nikiona itafaa nitaujumuisha huko mbele. Nilimpenda na kumpa good life la viwango vya juu. Acheni nyie

Ni sawa waache wakuite majina ya ajabu sababu hawajui kiasi gani ulininvest kumpa huyo binti furaha

Mjinga mjinga ambaye hata kumpa mwanamke 10k hajawahi lazima akuone katili lakini mwanaume kamili ambaye anasimamia majukumu yake yote kwa mwanamke hawezi kuvumilia udhalilishaji kiasi hicho.Mtu ajitoe kwa yote halafu wewe unawaza kwenda kuf*rwa na mwanaume mwingine ila hali nimekutangazia ndoa tayari!!!!!Hili halivumiliki linahitaji moyo wa kikekike kulivumilia .

Mungu atawasamehe wote kwa wakati wake huyo binti kwa ungese wake na wewe kwa ungese wako ila kwanza kila mtu apate uchungu kwa matendo yake..
 
Back
Top Bottom