Unajua mimi sikubaliani na binti kufanya usaliti,amefanya udanganyifu na udanganyifu ni dhambi.
Na jamaa alikuwa na haki ya kumuacha kabisa, hata ingekuwa mimi..mtu msaliti siwezi kuendelea naye hata iweje.
Shida ni namna alivyomuacha,
Kulikuwa kuna haja gani ya kwenda kumdharirisha hivyo?
Kwanini asimuonyeshe tu vithibitisho na kumuacha pasi na kwenda hadi kwao kama baba yake alivyosema kwamba kwanini hakusema tu ili wapige simu kwamba hawataenda kuonekana.
Namna alivyomuacha ndicho kitu tunakiongelea hapa.
Imemgharimu binti na matokeo yake hayo madhara naye anaanza kuyasuffer..si yeye kwamba yupo salama.
Sent using
Jamii Forums mobile app