Revenue Intelligence Bureau (RIB) suluhisho la upotevu wa mapato ya Serikali

Naona umekuja na ID yako nyingine ile unepumzisha. Haya kafanye kazi uondokane na maadui wa Taifa ujinga, umaskini na maradhi.
Tushatoka miluzi mingi ya mbwa wasio ng'ata, mtu analala ana amka na ka idea mfano iundwe polisi nyingine ya kufanya msako wa kodi tu iwe na askari waliobobea [emoji23][emoji23][emoji23] non sense .....boresha hao hao askari mlio nao mtaunda taasisi mpya ngapi sasa zifanye kazi ile ile inayofanywa na taasisi nyingine

Sent from my SM-P901 using JamiiForums mobile app
 
Watanzania tunafikiri kuunda taasisi mpya kila siku wakati zilizopo hazifanyi kazi kwa ufanisi.

Aliyefuta SUMATRA sasa hivi TASAC na LATRA wametatua changamoto zilizokuwepo ?
 
Naona sana umuhimu wa kuwa na idara kama hii ambayo itakuwa independent na TRA, Itakayokuwa na uwezo wa kubaini hata madudu yanayofanywa na maofisa wa TRA, pia kuchunguza tuhuma zozote zinafanywa na maofisa wa TRA kupoteza mapato ya serikali, pia kama kuna mbinu zozote zinazofanywa na Wafanyabiashara kukwepa kodi, na pia Ukiangalia kwa umakini uanona kuwa kuwa na kitengo kama hiki ndani ya TRA kutafanya kisiwe independent na Objective, Pia kitalinda interest za watu walio ndani ya TRA na mfumo mzima wa mlipa kodi, mathalani tumeona watendaji wengi wa TRA wakijajilisha muda mfupi mara baada ya kuajiriwa, Hivyo kuwa haja ya Kuwa ni kitu kama hicho, japo Kuna ile idara ya Investigation ndania ya TRA Lakini sioni kama ina impact kubwa kwenye makusanyo.
 
Wewe Una akili kubwa SANA. Hata umewaza mbali zaidi na zaidi, na nyie ndo mnatakiwa kuwa kwenye vitengo lkn Kwa bahati mbaya unaweza ukawa hata ajira huna am very sorry for that. Wewe ndo ungetupaisha Taifa letu sana
 
Wewe Una akili kubwa SANA. Hata umewaza mbali zaidi na zaidi, na nyie ndo mnatakiwa kuwa kwenye vitengo lkn Kwa bahati mbaya unaweza ukawa hata ajira huna am very sorry for that. Wewe ndo ukapaisha Taifa letu sana
Ahsante nashukuru.Kwa kweli kazi ninayo Kazi moja kwa 3 na ina impact kubwa.
 
Ahsante nashukuru.Kwa kweli kazi ninayo Kazi moja kwa 3 na ina impact kubwa.
Afadhali, maana tofauti na hapo ingalikuwa ni matumizi mabaya SANA ya rasilimali watu. Endelea kumpiga adui umaskini, ujinga na maradhi. Tutashinda
 
Kwa heshima yako tena, naomba ukatoe mchango wako kwenye pdf za jamaa tuone mawazo ya watu yanaonaje. Zote nimebandika Mimi humu
 
Kwahio suluhisho la upotevu wa mapato ya serikali (ambayo mapotevu mengi ni matumizi mabaya na ufujaji) ni kuunda tume / taasisi ambayo nayo itaongeza matumizi ?

Hizo taasisi zilizopo kama hazifanyi kazi kwanini zisivunjwe na kuundwa upya au kuwa replaced..., It's a no brainer upotevu mwingi mbali na wizi ni ufujaji..., na hiyo Taasisi ikiundwa ni wale wale watatoka huku kwenda kule (the only difference ni kuongeza matumizi)
 
hii project inabidi iwahusu TAKUKURU mkuu! pawe na kitengo maalum
 
Hivi ukiingia CCM huwa wanawakata vichwa msifikiri ama?.
 
Haina impact una takwimu?

mje na Stats kwanza ndo mlaumu jmn
 
Anatengeneza na ka pdf

Sent from my SM-P901 using JamiiForums mobile app
Basi aandike 'Paper' kweli
Hata wenye hizo Taasisi wakisoma waone Yes kuna gap hapa...

mana mtu lazma uje na uchambuzi wa mandate na utendaji wa Taasisi zilizopo na uonyeshe vivid weakness kuwa wameshindwa katika eneo hilo.,ili sasa baada y hapo ndo uje kujistify/kuhalalisha wazo lako na kuonyesha itakuwaje Taasisi mpya unayowaza itakavyofanya na impact/potential yake, Na itawork vipi na Taasisi zilizopo etc etc.,

Sasa bila ku'deduce vizuri utam'convince vipi Mh.Rais?.,

sijui CCM nani huwa anawakata vichwa baadhi ya watu.,i dont get it
 
" what if waliokabidhiwa vitengo wana perspective kama yako"

well that is "what if" not a reality.
huwez kujua kama you are not within the system.
hizo taasisi ulizozitaja zina vitengo vinavyo deal na financial issues ulizozitaja..

vingi vikiwa vimeanzishwa wakati wa mkapa.

unadhani kuanzisha taasisi mpya ambayo itafanya the same same work ambavyo hivi vitengo vimekuwa vikifanya for years?

My question is why? taasisi mpya itabadilisha nini?
 
Mitaasisi miiingi ni sawa na mapaka weeengi wasio kamata mapanya!! kwenda zako mzee!!!.... kalale mzee!!.... umechoka mzee!!
Taasisi zenyewe zimekaa kilaji laji tu!!! haya mambo ya wizi na ufukunyu nyuku... serikali yeyote Dunaiani hayata kaa yaishe kamwe!!!

kwa taarifa yako yalianzia mbinguni ndo maana shetani akawa Muasi wa jumla mpaka leo!!! akitaka kila kitu kiwe kwa mstari!! na sasa hivi yuko kuzimu usidhani Mungu anamchukia km wewe unavodhani tena wale wanapiga story mno!! kisa cha ayubu km unakijua kasome tena!

yote haya ajili ya ugonjwa wa Perfectionism km yako! inakufanya mpaka uhesabu finyango za nyama inapoletwa mezani unamuhesabia kila mwana fmilia....km ungekuwa mbinguni leo wewe ungejiunga na shetani moja kwa moja!!!

Haya yoote unayo yasema na kudhania!!! Jua kuwa hayako ivo!! hiyo kazi hata Waziri mmoja tu anajua ku i trend process nzima ya wizi!! unasikia? hata Baba ndani ya nyumba anajua anapompa Mama hela ya matumizi anapigwa sana!

Watoto wanapopewa matumizi ya shule wanakula cha juu!! Baba anajua vizuri tu siyo mpaka aunde tume!! eti shuleni nimepoteza Bunsen burner!! na test tube set kumi!!! wananitaka nilipe bila hivyo nisirudi baba anajua vyema ni uongo tena mno!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…