gfsonwin umeongelea kitu ambacho sikuwahi kukitilia maanani sana but very important. Maana nakumbuka enzi zetu O Level tulikuwa tunakutana na wanafunzi kutoka sehemu mbalimbali za nchi na pia kutoka dini tofauti.
Hata ukisoma kwenye wilaya yako bado ilikuwa unakutana na watu kutoka sehemu mbalimbali za nchi. Lakini kwa hizi shule za kata sidhani kama hiyo kitu ipo tena. Hakuna tena kuwachanganya wanafunzi mashuleni.
Badala ya kutoa "elimu kombo" tunatoa "elimu kimbizi." Katika sehemu ya hotuba yake aliyoitoa mwaka 1985 mjini Dodoma wakati akifunga Mkutano wa Chama Cha Elimu ya Watu Wazima (CHAWATA), Mwali Nyerere alisema:
Chanzo:
Nyerere:-Wasomi wameiharibu Elimu; Wafungua shule kwa pupa; Watoa
yap Nyerere had a point hapa na ukiisoma hii article yake utagundua kwamba aliona jinsi ambavyo elimu tuipatayo inavyotuandaa kuwa tegemezi.
let me tell you, the days naanza shule education for self relience was key issue. na hata madarasani we had shambaz, and bustaniz plus other vocational skills and on top of that the home economics classes.
ilikuwa wakati wa msimu kama ni shamba tunapanda tena tukiwa supervised na waalim wetu, kisha tunapalilia paliz zote mbili halafu tunakuja kuvuna na kuhifadhi. yote haya tuliyafanya na yalitufunza kuwa independent kiasi kwamba ukirud home wewe ndo mwl wa shamba.
madarasa ya home economics tulifundishwa kuanzia personal hygiene, usafi wa mazingira na hata mapishi na utunzaji wa vitu. nakumbuka mimi kufua nimefundishwa darasani nikiwa class 3, hata jins ya kuosha viatu, kupika kadhalika. ukitoka hapo ukirudi nyumban wewe kazi yako ni kupractice tu ulichojifunza yani hadi mzazi hapati shida manake anajua utajifunza tu.
mashuleni tulikuwa na vocational skils kufuma mikeka, vitambaa, kutengeneza mafagio, kuchonga mwiko, panga, visu vigoda et al tulifunzwa kuanzia darasa la tano.
sasa turudi kwenye elimu ya kileo, mwanafunzi toka anaingia shule hadi anatoka anafundishwa kusoma na kuandika tu, hana ujuzi mbadala anaoupata ili hata kama atafeli basi aweze kuwa na cha kufanya hakuna. tunatengeneza mambumbumbu zaid kuliko wasomi. hakuna anayejali mwanafunzi akitoka form 4 katoka nanini cha ziada zaidi ya scores zake kwenye masomo. na hapo ndipo utakuta mtu akipata div 4 inakuwa ni tatizo.
let me tell you, ingekuwa kwamba shulen wanafunzi wetu wanafunzwa kuyatumia mazingira yao kikamilifu, kiasi kwamba wanatoka wakiwa na elimu ya maisha na elimu ya darasani basi ni wazi kwamba hata kama wangefeli ungekuta wamejiendeleza zaid kifani kuliko kuhangaika mtaani miaka 3-4 kuresit na wasifaulu.
kwanza kabisa sioni hata maniki ya kuresit hii mitihani wanayofeli manake kama alifeli kwa mara ya kwanza basi angetakiwa system yenyewe imchagulie alternative solution lkn sio kumfanya mwanafunzi asote kitaa na re sitting mwaka hadi mwaka pasi la msingi na hela zinazidi kuisha. niliwah kujenga logic kwamba hii resitting ni njia ya baraza la elimu kula hela za watu nikashambuliwa kama mpira wa kona but huo ndio msimamo wangu manake tuambiwe leo hii imekuwa na tija kwa watu wepi?? zaid ya kuzidi kuwa frustrae tu hawa wanafunzi?? na je maisha ni mapaka ufaulu tu form 4 ama 6?? why not looking for an alternative means??
Hope you will agree with me kwamba elimu ya self reliance ingebaki hadi leo hii, basi tungeona vikundi vingi sana vya vijana vya kimaendeleo kuliko hali ilivyosasa?? na tungeona almost kiwango cha uzalishaji kimeongezeka kuliko ilivyo hivi sasa. watu kukaa na kuonyesha projection ya number of youths pasi kutafuta the real and valid solutions ni bure kabisa.
vijana wangeweza kuwa mobilized wakawa na vikundi ambavyo watafanya kazi na kupewa training ili kuboresha ujuzi wao na maisha yakasonga mbele. kuliko kumkopesha kijana mmoja mmoja, basi kwenye kikundi ni rahisi aid na wakafanya vitu ambavo hata serikali inge wasapoti kwa kuwa tafutia masoko usingewakuta wengi wako jobless kitaa. kwa Kiongozi mwenye akili njema wingi wa vijana kwake ni hazina kwani anajua hii ndio nguvu kazi na injini ya utendaji kwenye taifa lake. Lakini kwa taifa kama Tanzania vijana ni mzigo na hata wengine wakadiriki kusema ni bomu linalosubiri kulipuka jambo ambalo ni kashfa sana.