Roulette nadhani watoto na vijana wana interests zao which should be recognised and respected. They have people and things which they perceive to be relevant to them. Nilipokuwa mtoto nilikuwa hivyo hivyo. Lakini umri unavyokwenda interests and perceptions zinabadilika.
Inawezekana kabisa mtoto/kijana akajifunza kutoka kwa Wema kuliko kwa Naibu Spika wa bunge, maana hata mimi mzee mzima sina cha kujifunza kutoka kwa Naibu Spika kama kiongozi. Lakini kuna baadhi ya mambo ningependa kuyaongea hasa katika hoja ya kuwaanda watoto na vijana kuwa viongozi wa kesho.
Tunakoelekea kutahitaji more creativity, kuwa mjuzi kwenye teknologia, na uwezo wa kuunganisha watu na ideas. Tena kulingana na jinsi uchumi wa duania unavyoenda, watoto wa nchi kama zetu wanatakiwa kuyajua haya mambo mapema na kwa haraka zaidi. Kwa hiyo, nadhani watoto na vijana wasiandaliwe tuu kwa ajili ya leadership roles, bali kwa kila kitu ili wawe na competencies za kukabiliana na dunia inayokuja.
Kwanza, watoto waandaliwe ili wawe na tabia nzuri kama binadamu regardless of whether or not they want to be leaders (though naamini kila mtu ni leader). Hilo lenyewe ni muhimu sana. Kwa dunia ijayo itamchukua mtu miaka mingi sana kujenga reputuation, lakini hiyo reputation inaweza kuangamizwa na social media kwa siku moja tuu.
Story kama hii inasema mengi:
BBC News - Paris Brown: Kent youth PCC resigns after Twitter row. Alichanguliwa na wapiga kura kama the youngest police commissioner in the United Kingdom at the age of 17. Baada ya hapo watu wakaja kuibua tweets ambazo ali-tweet wakati akiwa na umri wa miaka 14 na 16 na kumlazimisha kujiuzulu. Social media is a powerful tool for the youth, but it can also be powerless.
Siku hizi nasikia pia waajiri wengi huwa wanapitia pages za Facebook na Twitter kabla ya kuwaajiri watu. Many employers now want to know the character of potential employees. Probably kuna wengine would specifically ask for them. Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa makini with what they post on social media, they may come to hunt them in future siyo kikazi bali kwenye nyanja nyingine pia. Unamkumbuka yaliyompata yule shahidi kwenye ile kesi ya Charles Taylor? Inawezekana bado Tanzania, lakini tunaelekea huko.
Pili, concept nzima ya jamii inabadilika. Siku hizi kuna online community. Watu hamjakutana lakini mko so close on the internet. Kama alivyosema mmoja Facebook is for the people you know. Twitter [and JamiiForums] is for the people you wish you knew and Myspace is for the people you wish you NEVER met.
Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa responsible katika kujenga online communities. Kwa mfano, they should not add someone as a friend simply because that person sent them a friend request. Waangalie kama kuna connection yoyote in terms of interests and what can be learned from each other. Quality rather than quantity ya friends and who you follow is much better.
In addition, viongozi wengi wa sasa nao wanaongezeka kwenye social media. So, badala ya watoto na vijana kuishia kuwambia tuu viongozi kwenye social media Go go kiongozi wangu, nakuaminia Mkuu wangu, Youre my role model, "You're always right, Mkuu wangu", "I trust you, Boss wangu", n.k., waelimishwe kuwa na tabia ya kuchangia as thought or future leaders kwenye mijadala inayoendelea social media. Wawe na tabia ya kutaka kuhoji kinachoandikwa na viongozi kwa kufuata hoja zao badala ya viongozi wenyewe.
Viongozi nao wawe na tabia ya kuwa-engage vijana kwenye social media. Nimeshaandika sana hapa juu ya tabia ya baadhi ya viongozi kutundika status au tweet na kusepa huku wakisubiri watu wa-like au wa-tweet status zao au kumwagiwa masifa. Hii inaweza kuwadumaza vijana, kwa sababu watadhani social media works just like conventional media.
Hapa ndipo social media inapokuwa powerless kwa watoto na vijana maana wanapowauliza hawa viongizi maswali, mengi hayajibiwi. Kuwa interactive means to engage people, testing their understanding, listen to them, etc, hata kama hukubaliani nao. Nilishasikia kuwa kuna watoto na vijana ambao hawasikilizwi majumbani mwao, kwa hiyo wanaona social media ni tool ya kusikilizwa. Kama na huko hawasikilizwi na wanaowaamini kuwa ni viongozi wao, then we are not doing any better for them.
Tatu, dunia inaangamizwa kwa njia mbalimbali kama uharibifu wa mazingira. Watoto na vijana waelimishwe maana ya sustainability. Tembo wetu wanaangamia. Waelimishwe athari na impact yake kwenye maisha yao ya baadae.
Nne, siku hizi kuna information nyingi sana. Pia it is becoming easier and easier to access the information. Watoto na vijana waelimishe kuwa not all information out there is correct. Vijana wafundishwe kuwa pro-active katika kuunganisha data na kufikia conclusions za muafaka. Huko tuendako hakutakuwa tena maswali ya kujaza sehemu zilizo wazi kama vile Rais ya Tanzania ni Jakaya Kikwe__ (a) we, (b) ta (c) te. au yale maswali ya false and true.
Hakutakuwa tena na kukremisha mambo. Kwa hiyo, watoto na vijana waelimishwe kuwa na fikra tunduizi. Kwenye homework zao na hata kwenye mazungumzo ya kawaida tuu, wazazi wawe na tabia ya kuwauliza watoto maswali siyo ya kufikiri tuu bali ya kufikiri critically na ku-reason.
Kama mtoto au kijana anapenda kufuata sana habari za Wema au Diamond badala ya news za Dkt Slaa au Rais Kikwete sidhani kama kuna haja ya kumkataza kufanya hivyo. Best way ni kumshauri au kumfundisha jinsi ya kufikri critically. Inawezekana kuna mambo mazuri wanayofanya akina Wema na Diamond (of course yapo) and these kids will want to take the good ones (na kuacha mabaya yao) and build on them na kuwa artists wazuri zaidi. We need artists as well na siyo politicians tuu!
Watoto na vijana wafundishwe jinsi ya kutumia common sense kutatua matatizo yao madogo madogo. Siyo kila tatizo anatafuta ushauri kwa mama na baba. Tunaona sana hapa JF jinsi baadhi ya vijana wanavyoanzisha threads ambazo wengi tunaona kama jibu lipo wazi kabisa. Huko baadae waajiri hawatawa-train tena waajiriwa, bali wataajiri tuu watu ambayo tayari wanajua kufikiri na kutumia rasilimali vizuri.
Tano, tunakoelekea teknologia itaongeza ubora wa multi-tasking. Wengi tunajua kuwa multi-tasking inaongeza distraction na usahaulifu. Hapa sina maana ya kuwafundishwa watoto na vijana wa kiume kuongea huku wakipiga mswaki, though I am sure haitakuwa shida kwa Matesha wa
Asprin. Lakini watoto na vijana wafundishwe jinsi ya ku-priotise mambo, jinsi ya kuwa focused na kujenga na kudumisha mahusiano na watu wengine.
Jukumu la nani? Kila mtu, kuanzia, mzazi, ndugu, rafiki, viongozi, taasisi na jamii kwa ujumla.