Mkuu kama uko vizuri kwenye mambo haya hebu tusaidie, kwa mfano mtu akikopeshwa 30m kwa riba ya 3% kwa mwezi at reducing balance, marejesho yake yatakuwaje kwa mwaka? Je! Hii riba ina unafuu wowote au ni mauaji? Mkopo unatakiwa urejeshwe ndani ya miezi 12. Hao ni Finca
Mkopo 30 m, riba 3%, on reducing balance, muda miezi 12,,
Marejesho yatakuwa sh 3,007,520.00 kwa @ mwezi,
Jumla malipo yote sh 36,090,034,, Riba pekee sh 6,090,034,
Unafuu au Ughali inategemea vitu vingi, kwa kulinganisha na Bank km CRDB, NMB, NBC, hao wako ghali sana kwani hao niliowataja kwa mtindo huo huo wa Reducing Balanca riba ni 1.5% hadi 2 % @ mwezi,,,,
Pia kwa kulinganisha na MICROFINCE Zingine Finca wanaweza kuwa wa kawaida au nafuu kdg kwani wengi wako 3% hadi 10% on reducing balance kwa mwezi. Yategemea wepesi wa kupata mkopo, kiasi cha mkopo, muda wa kulipa, dhamana, lengo halisi la mkopo n.k.
NI MATUMAINI YANGU KUWA NIMEKUJIBU.