Biggs
JF-Expert Member
- May 3, 2014
- 2,068
- 2,314
Hizi riba zilitakiwa angalau ziwe single digit.Sababu mojawapo ya Tanzania kuwa na ajira ndogo ni riba kubwa za mikopo ya bank zetu. Imefika wakati hata Kimei ambaye alikuwa mkurugenzi wa CRDB kasema bungeni.
Nitoe tu mfano unaweza kupata mkopo wa gari 3% nchi nyingine kwa miaka mitano .Kwa gari hilo hilo Tanzania unapata mkopo wa asilimia 15% kwa miaka miwili tu. Hivyo mfanyabiashara pesa nyingi inaenda kwenye kulipa mkopo na habaki na pesa ya kukuza biashara yake. Bank kuu yetu itafute utaratibu wa kupunguza riba tukizingatia mfumuko wa bei umeshuka mpaka 4% tu kwa mwaka.
- Riba ikiwa kubwa biashara ndogo ndogo hazitaweza kukopa hivyo haziwezi kuwekeza kwenye ukuaji wa biashara. Hii inasababisha ajira ndogo na kodi ndogo
- Riba kubwa zinaongeza gharama za uzalishaji na uuzaji wa vitu. Mfanyabiashara inabidi aongezee gharama za bank kwenye maligafi anazotaka kuuza na kusababisha malighafi kuwa na gharama kubwa na kushidwa kabisa kushindana na malighafi za nchi ambazo wana riba ndogo
Kwa sasa riba ni kubwa sana na lots of Hidden Costs zingine zikiwa na ukakasi wenye lengo la kumkamua mkopaji.