Rice cooker 1.8 l itaweza tumia umeme wa units 14 sawa na 5000 kwa siku 30

HABARI WANDUGU

NAPENDA ULIZIA MATUMIZI YA RICE COOKER YA 1.8L , IKIWA INAPIKIWA MCHANA NA USIKU YAANI INATUMIKA MARA 2 KWA SIKU , JE UMEME WA 5000 UTAFAA KWA SIKU 30 ?

AU NI KUBWA SANA , MAANA NAHITAJI SET BUDGET YA KI GHETO GHETO .....
Inaelekea Mama/Baba Mwenye nyumba wako mtata sana.
 
Kama hauna pressure cooker ndiyo utawaza itatoka tope
Pressure cooker ni zaidi ya rice cooker. Ina option zote za vyakula hadi tambi unapika
Ndiyo nimeitumia kupika wali, umeiva vizuri.
inawezekana hata jagi la maji kuchemsha marange ndugu

upo sawa
 
Nyingi zina watts 700 izo, kama inapika mara 2 kwa siku tu assume unatumia dakika 45 45 kwa io mara mbili ni lisaa na nusu

700watts*1.5hours unapata 1050watts hapo kwa kwa siku Moja

1050w*30=31500watts=31.5 watts kwa mwezi....
natumia dakika 20 , kupika kipunga mkuu vipi units ngapi zinaenda kwa dakika 20 ?
 
natumia dakika 20 , kupika kipunga mkuu vipi units ngapi zinaenda kwa dakika 20 ?
Iko hivi Dogo, Unit moja ni sawa na Megawatt 1000 used per 1 hour.
Kwa hiyo kama una Device labelled 700watts maana yake ukiiwasha for 1 unatumia 0.7unit ≈ 1unit......so unaweza kuhesabu kama utatumia dakika 20 badlaa ya dakika 60.
 
Pressure cooker ya umeme (multi cooker) inatoa wali mzuri kuliko wa rice cooker. Na ukipata ambayo ni intelligent matumizi ya umeme yanashuka sana...
multi cooker sawa usinambie Pressure cooke
 
Iko hivi Dogo, Unit moja ni sawa na Megawatt 1000 used per 1 hour.
Kwa hiyo kama una Device labelled 700watts maana yake ukiiwasha for 1 unatumia 0.7unit ≈ 1unit......so unaweza kuhesabu kama utatumia dakika 20 badlaa ya dakika 60.
Unamlisha matango pori huyo kijana. 1KWHr equals 1 unit.

Afanye hivi 700/1000*(20*2)/60*30* *5000/14.
 
Iko hivi Dogo, Unit moja ni sawa na Megawatt 1000 used per 1 hour.
Kwa hiyo kama una Device labelled 700watts maana yake ukiiwasha for 1 unatumia 0.7unit ≈ 1unit......so unaweza kuhesabu kama utatumia dakika 20 badlaa ya dakika 60.
Kwa hesabu hizi bwawa la Nyerere linazalisha unit 2 Kwa siku sio?
 
W700 hio cooker inayo,
Kwa kawaida wali unapikwa nusu saa hadi dakika 40,
Kwa kuwa utapika mara mbili, maana yake ni saa moja hadi na nusu,
Means kwa siku utatumia 1 Unit kwenye rice cooker, sawa na unit 30 kwa mwezi,
Unit moja inauzwa 357Tsh,
Kwa mwez utatumia

357 X 30 = 11,000/- Tsh kwa ajiili ya umeme wa cooker
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…