Rich Mavoko achana na WCB huendani na kasi yao

Rich Mavoko achana na WCB huendani na kasi yao

Ni kweli kabisa kaka Rich Mavoko umepwaya kabisa kama tulivyotegemea ungefanya vizuri zaidi kumbe imekuwa kinyume chake.

Tatizo siyo kufanya wimbo na msanii wa Nigeria au popote pale hapana hata kipaji chako kimekufa kaka ni bora ukomae mwenyewe hao jamaa style yao huiwezi kaka nakuambia mapema kabisa.

Mwisho vijana wa WCB wote wako vizuri wewe umekwama wapi brother nadhani ni wakati wakutafakari kabla ya kipaji chako kupotea.


Wewe kama sio wivu ni nini haswa

Unapoongelea kufanya vizuri mbona umeshindwa kushusha nondo ukaeleweka dhamira ya uzi wako.. hata link ya youtube hujaweka ni wivu tu
 
Una chuki binafsi na rich haiwezekani
 
Mbona anafanya poa tu na ilo ngoma lake la Rudi
 
Binafsi kwenye hilo kundi lao ni mavoko pekee mwenye kipaji kikubwa cha uimbaji.Anajua kuliko hao wengine wote kwa mtazamo wa mimi
 
Nipe tofauti ya mavoko alivyokuwa ktk lebo ya king kaka ya Kenya ,baada ya kuachana na papa misifa (na kama kweli unamfuatilia mavoko nitajie nyimbo zake mbili alizozitowa akiwa chini ya hiyo lebo ya king kaka na zilifika wapi) na mavoko wa WCB ,ukilijua hilo ndio utajua kama mavoko anapanda au ameshuka muwe wafuatiliaji sio mnaropoka tu na kama hujui mavoko aliachana na papa misifa baada ya jamaa kumbambikia kesi ya kumdai milioni 500 (tafuta mahijiano kati ya soudybrown na papa misifa youtube) na ndio utajua jinsi gani WCB na mondi walivyoamua kubeba msalaba wa mavoko .
I think ilikuwa ni mil 50 na sio 500 kama nakumbuka vizuri kuhusu huo mgogoro.
 
Back
Top Bottom