Rich Mavoko aishtaki WCB kwa ‘mkataba wa kinyonyaji’

Shark

JF-Expert Member
Joined
Jan 25, 2010
Posts
29,775
Reaction score
29,746
By Nasra Abdallah, Mwananchi. nabdallah@mwananchi.co.tz

Msanii Rich Mavoko amefikisha malalamiko yake serikalini kwa kutoridhishwa na mkataba aliopewa na uongozi wake wa WCB.

Hayo yamesemwa na Katibu Mtendaji wa Baraza la Sanaa la Taifa (Basata), Godfrey Mngereza alipozungumza na MCL Digital kufafanua kuhusu madai ya mwanamuziki huyo kwa lebo hiyo inayoongozwa na Diamond Platnumz.

Mavoko ameonekana katika ofisi za Basata leo Agosti 9. Kuhusu tukio la yeye kuonekana katika ofisi hizo, Mngereza amesema alikwenda kwa ajili ya kujisajili kwani hakuwa amepitia utaratibu huo.

"Naomba ieleweke kwamba hakuna kesi yoyote tuliyoletewa na Rich na alichokuja leo ofisini kwetu ni kwa ajili ya kujisajili,” amesema.

Akifafanua kuhusu suala la mgogoro wake na WCB Mngereza amesema, “Tunachokijua hadi sasa kuna malalamiko alishayaleta kuhusu kutoridhika na mkataba alioingia na WCB na tayari tumepeleka kwa kamati iliyoundwa na Waziri ya kufuatilia mikataba hiyo.”

Akizungumzia madai hayo mmoja wa viongozi wa lebo ya WCB, Babu Tale amesema hayupo katika nafasi ya kumzungumzia Rich Mavoko akitaka waulizwe Basata. “Mimi siwezi kulizungumzia hilo waulizeni Basata,” amejibu kwa kifupi.
 
Hakuridhika mwanzo au alipokuwa ana renew 🤷🏼‍♀️
 
Yaani badala ya kwenda mahakamani yeye anaishitakia serikali, chombo chenye mamlaka ya kutoa uamzi ktk mambo ya kisheria ni mahakama tu.

Halafu kwani kipindi anausaini huo mkataba hakuuona kama ni wa kinyonyaji anakuja kuuona leo au akili zake hazikua timamu kipindi anausaini(mwezi mchanga) au umri wa kuingia mikataba ulikua bado kwa hyo mtu alimsainia badala yake leo kakua ndio kagundua mkataba ulikua wa kilaghai.

Nyie wasanii mkome kabisa maana mnawaona wanasheria kama walipoteza muda wao kwenda shule, hapa ungekua na mwanasheria angekushauri kuhusu huo mkataba kabla hujausoma, wanasheria wanatumia technical terms ktk mikataba ambayo mara nyingine layman ni ngumu kugundua unakuja kugundua kumekucha.

Ninauhakika sasahivi umeahauriwa na lawyer na ishakuwa too late boy, pambana tu na hali yako unless you have to prove the opposite.
 
Anataka kutembelea nyota ya WCB.....ubavu anao? mwenzake kakimbilia kwenye soka now.
 
Avumilie tu ukiisha basi aanze kivyake.
 
Wasanii wa Kibongo wanapenda sana kulia lia na kutafuta huruma kwa Makosa yao wenyewe!
Muda mwingine waache wapambane kwanza ili Wajifunze..,
 
Tatizo mkuu hawa wasanii hawapo serious wewe mtu unaingia mkataba wa miaka kumi hiyo si muongo mzima huo?

Sasa alichobaki nacho ni ama avunje mkataba alipe hayo mamilioni au aendelee kukaa WCB asubiri miaka kumi iishe.

Sidhani kama angekuwa na mwanasheria qngesaini mkataba wa miaka yote hiyo sidhani hata kidogo. Katika dunia ya sasa yenye fursa kibao huwezi kujifunga kwenye mikataba ya aina hiyo maana mambo yanabadilika unaweza kughairi anytime.

Mikataba mizuri ikizidi sana miaka mitatu lakini mara nyingi miwili au mmoja muda ukiisha mnarenew upya kila baada ya mwaka.
 
zile pupapupa na kudhani atapata mafanikio fasta au kuongopewa atapata kitu flani halafu kumbe hata kwenye mkataba hakipo yeye anakimbilia kuanguka saini tu. Acha wakome tu
 
Inabidi Diamond akamatwe kwa utapeli. Ndio maana Mavoko amekonda sana kwasababu anakosa hata hela ya kula hela zote Diamond anajirusha na wakina Mobetu
[emoji23][emoji23][emoji23][emoji23][emoji23]khaaa
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…