Rich Mavoko kwenda kusign WCB ni jambo la aibu

Rich mavoko msela wa kigogo...hata body language yake ilikuwa inaonyesha yuko kimwili tu dabriuu sii biii
 
Uliona mbali sana hopefully waliokuzodoa na kukupinga kiana wamekiri
 
Rich Mavoko ana mwimbo mpya unaitwa "Wamoto". Uko poa tu na style yake ile ile ukisikiliza unajua huyu mesi. Cha ajabu promo ndogo, kiki hamna. Kwa hiyo wewe kama ni fan wake msaidie kupush. Hata uzi sijaona kuhusu hizi ngoma zake mpya.
Sasa naona upo trending #37. Msaidieni apate moyo ile video si ya ku trend #37 wiki moja!!
 
Huo utabiri wa lara 1 ni wa 4 years back aisee!!!
She spoke her mind and laid her views tu!
Mavoko atabakia tukisema mkali tu ila hana maajabu kama vigezo ni Kiki na promo!
 
Nimefuatilia nyimbo alizotoa mavoko za hivi karibuni zote zipo poa pia kaja na taste mpya ya mziki akipata wawekezaji wakubwa watakuwa kwenye pik kama kina diamond
 
HAWEZIIIIIIIIII! Maana Dai ndo anamchagulia wimbo wa kutoa. Wakiona wimbo mkali wanaubania. Hairuhusiwi kumpita boss. Yale yale ya Lil Wayne na Cashmoney
Nadhani hivi sasa anatoa nyimbo kali tupu manake Diamond hawezi tena kumbania!
 
Here we are..... Waliomtukana mtoa mada mnaombwa murejee tena hapa.
Kwani kuna kipi kipya?! Mavoko wa WCB na wa sasa yupi alikuwa ana-trend?! Kilichompoza Mavoko ni thread za aina hii na zikamvimbisha kichwa kwa kwamba yeye ni mkubwa kweli kweli, na bila shaka huo ukubwa wake hivi sasa unaonekana baada ya kujiondoa WCB!
 
Wanyonyaji wale
Hivi sasa hakuna anayemnyonya na bila shaka yupo juuuuuuu, juu kabisa ingawaje hata ukimuuliza mtoto mdogo atakuambia kwa sasa hana ubavu wa kushindana hata na Zuchu aliyeingizia kwenye muziki mieizi kadhaa tu iliyopita!
 
Nimefuatilia nyimbo alizotoa mavoko za hivi karibuni zote zipo poa pia kaja na taste mpya ya mziki akipata wawekezaji wakubwa watakuwa kwenye pik kama kina diamond
Ungekuwa unamfuatilia Mavoko sidhani kama ungeongea hoja ya wawekezaji kwa sababu yule jamaa ni kama huwa anataka kushindana na kichwa! Kuna wakati alikuwa chini ya management moja huko Kenya na watu wakaamini hatimae angetusua! Alikaa muda gani kwenye ile management? Na kwenye biashara yoyote, kufanikiwa kwake kunategemeana sana kama una timu inayoifahamu vema biashara husika. Kwa maana hiyo, anaweza kupata mwekezaji lakini kama mwekezaji mwenyewe haijui biashara ya muziki basi atabaki kuwa msindikizaji tu huku akiendelea kupotea siku baada ya siku!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…